WALAKA KWA FILEMONI.

0
4كيلو بايت

Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi,

Mtume Paulo alipokuwa kifungoni,aliandika walaka huu kwa Filemoni kama katika mwaka wa 62 baada ya Kristo. Felemoni alikuwa ni mmoja wa viongozi wa kanisa la Kolosai ( Wakolosai 4:9). Walaka unazungumza juu ya upendo wa Paulo,uthamani wa upya kwa Onesmo,Paulo kubeba mzigo wa Onesmo pamoja na ombi maalumu la Paulo kwa Filemoni. Hata hivyo;Walaka huu unaeleza kiundani maombi ya Paulo kwa rafiki yake Felemoni afanye mambo mawili muhimu kama yafuatavyo;

  1. Felemoni amsamehe Onesmo.
  2. Filemoni amkubali na kuanza tembea pamoja katika utumishi.
  •  Ombi la Paulo kwa Filemoni,amsamehe;

Onesmo alikuwa mtoto wa kiroho wa Paulo ambapo Paulo alimzaa kipindi cha vifungo vyake ( Filemoni 1:10). Lakini huyu Onesmo kabla ya kuzaliwa kiroho alikuwa ni mmoja kati ya watumwa wa Felemoni. Naye Onesmo alimkimbia bwana wake Filemoni,hata akawa hafai tena kwake (Fil.11).

Paulo anajaribu kuonesha kwamba Felemoni amebadirika na sasa anafaa,anaonesha uthamani wa Filemoni ( Fil.10-15). Hata hivyo Paulo anamuomba Filemoni katika hali ya kujishusha akimsihi ampokee aliyekuwa mtumwa wake yaani Onesmo. Tunajifunza kumbe,mtu anaweza akawa hakufai leo lakini kesho akakufaa zaidi kama ilivyokuwa kwa Onesmo.

Lakini pia Paulo anakufunza kwamba;kuna wakati unahitajika ujishushe sana katika maombi au kauli zako kwa watu hata pale ambapo una mamlaka ya kuamua,lakini usitumie mamlaka yako bali jaribu kuomba katika hali ya kusihi,maana Paulo anasema “kwa hiyo,nijapokuwa nina ujasiri katika Kristo kukuagiza likupasalo;lakini,kwa ajili ya upendo nakusihi…” Fil.8-9,Kwamba Paulo aliweza kumuagiza lakini hakuona vyema kuchukuliana na ujasiri wake isipokuwa atumie lugha ya upole kumsihi mtenda kazi Filemoni juu ya kumpokea Onesmo.

Katika eneo hili,emu jifunze kitu leo;kwamba hata kama una mtu aliyemkosa mtu mwingine,nawe unahitajika utumie lugha ya unyenyekevu kuhakikisha wanapatana vyema. Lakini cha ajabu wako watu ambao wanapenda kuona kwamba waliokosana waendelee kukosana muda wote;hapana wewe usifanye hivyo. Ninajaribu kumlinganisha ndugu Onesmo kama mmoja wa wadada wa kazi tulionao majumbani mwetu.

Ukiangalia kwa undani utagundua wapo wadada wa ndani wanaofanya mabaya kwa maboss wao kisha na kukimbia. Sasa chukulia mdada kama wa namna hiyo aliyekukimbia labda alikuaribia vitu vyako,chukulia anataka kwenda kufanya kazi mahali pengine au anataka kurudi kwako,Je wewe utafanyeje? Wengi watalipiza kisasi,labda watamkamata na kumuadhibu;Lakini kupitia walaka huu;hutakiwi kuwa na hasira naye bali umpokee kwanza maana inawezekana akawa amejirekebisha tayari.

  • Filemoni amkubali Onesmo ambaye sasa ni mtendakazi.

Paulo anazidi kumsihi Filemoni aweze kumpokea Onesmo,akisema kusudi lilopo. (Fil.15). Kwamba labda Onesmo alitengana na wewe kwa kitambo kwa sababu ya mambo ya kimwili,lakini sasa umpokee arejee kwako nawe uwe naye milele. Hivi unajua mfanya kazi wako wa ndani anaweza akaondoka kwako ili kusudi fulani litimie hapo baadae? Kwamba arejee akiwa anakufaa kwa mambo ya rohoni. Si wengi wenye kutafakari hili!!

Onesmo sasa amekuwa si mtumwa bali zaidi ya mtumwa kwa ajili ya kazi ya Bwana. Na ndivyo ilivyo sasa kwako wewe ambaye una watu uliowaajiri lakini watu hao wanaweza wakawa si watumwa tena kwako bali wakawa ni zaidi ya watumwa wa Bwana. Kile ambacho anakifanya Paulo katika walaka huu,ni kumfanya Filemoni asitizame mambo katika mwili bali katika roho;

kwa maana katika mwili ni kweli kabisa Onesmo alikuwa hafai,na ni mtumwa aliyemkimbia lakini kumbe katika roho Onesmo ni mtu mwingine kabisa. Ukimtazama mtu kimwili kamwe hatakufaa kabisa kwa maana utamuona kwamba ni mtumwa,au utamuona ni mtu wa kudharaulika,hana pesa,kachoka N.K lakini wewe hujui huyo unayemuona hivyo ni chombo kiteule kwa Bwana,naye ndiye atakaye kufaa kukusaidia kiroho.

Paulo anabeba dhamana ya Onesmo kwa maana sasa Onesmo ni kiumbe kipya (Fil 17). Moyo huu aliokuwa nao Paulo kwa mtoto wake wa kiroho,ni moyo wa wa ajabu sana na ndio ukristo wenyewe unavyotakiwa kuwa. Paulo alikuwa tayari kulipa deni yote ili tu Onesmo apokelewe ( Fil 18), Wewe Je,unaweza kubeba mzigo wa mtu mwingine aaliyekuwa muovu lakini sasa amebadilika? Ukifaulu hapo,basi ujue thamani ya wokovu wako itaonekana. Paulo amejawa na pendo kiasi kwamba hataki mtoto wake apotee,bali apokelewe vizuri.

Binafsi nimewiwa sana na huu ujumbe katika walaka huu. Ikiwa sisi tuliokoka tutafanikiwa kuishi maisha haya basi hakika tutamuona Mungu katika viwango vya juu. Ninalisema hili kwa maana ninajua wakristo wengi wa leo ndio wa kwanza kuwanyanyasa wadada na wakaka wa kazi za ndani. Wengine wanadiriki hata kuwakata mishaharaa yao tena kwa kosa dogo sana,mfano mdada kavunja glass ya maji ya kunywa basi boss wake anamkata mshahara wake. Kwani ukijaribu kumsaidia taratibu taratibu hatajirekebisha? Mungu akupe moyo huu wa kumrejesha mkosa aliyebadilika.

Paulo anatuambia pia kumbe;Filemoni alikuwa na utii ndani yake (Fil 21). Ni vyema nawe ukawa na roho hii ya utii ili ikusaidie kutekeleza maagizo yote uliyoagiziwa na wakubwa wako.

البحث
الأقسام
إقرأ المزيد
HOLY BIBLE
Comforting Bible Verses
Our God cares about us. No matter what is happening, he never leaves us. Scripture tells us God...
بواسطة MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 10:56:09 0 5كيلو بايت
DANIEL
DANIELI 10
Jina la Bwana wetu YESU KRISTO libarikiwe. Karibu katika mwendelezo wa kitabu cha Danieli,...
بواسطة GOSPEL PREACHER 2021-11-08 01:49:19 0 7كيلو بايت
REVELATION
UFUNUO 14
Kama tunavyofahamu baada ya wakati wa mataifa kuisha yaani unyakuo kupita itakuwa imebaki miaka 7...
بواسطة GOSPEL PREACHER 2021-10-30 11:47:48 0 5كيلو بايت
LEVITICUS
Verse by verse explanation of Leviticus 26
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 79 questions at the...
بواسطة THE HOLY BIBLE 2022-01-24 10:38:57 0 6كيلو بايت
JOSHUA
Verse by verse explanation of Joshua 14
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 30 questions at the...
بواسطة THE HOLY BIBLE 2022-01-25 08:11:35 0 5كيلو بايت