MFANO WA MPANZI NA MBEGU

0
5K

  LUKA 5;8-5

"Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake; naye alipokuwa akizipanda, nyingine zilianguka karibu na njia, zikakanyagwa, ndege wa angani wakazila. Nyingine zikaanguka penye mwamba; zilipoanza kumea zikakauka kwa kukosa rutuba.  Nyingine zikaanguka kati ya miiba, na miiba ikamea pamoja nazo ikazisonga. Nyingine zikaanguka penye udongo mzuri; zikamea, zikazaa moja kwa mia. Alipokuwa akinena hayo alipaza sauti akisema, Mwenye masikio ya kusikia, na asikie". 
 
Kama ilivyokuwa kawaida yake YESU KRISTO katika kile ambacho kinafahamika kuwa ni kutuachia mafunzo kupitia kwa wafuasi wake,ili kuwafunua waweze kufikiri kwa kina na kuweza kutambua kwamba ufalme aliokuja kuuanzisha ni wa mbingu wala si wa duniani.Lakini hapa mbele ya mkusanyiko wa watu mbalimbali waliomjia toka katika kila mji wakihitaji kuponywa na kufunguliwa,mwana wa mungu alinena maneno hayo,nasi kutokana na mfano huo tunaweza kupata somo lifuatalo.
 
 
Mbegu ni neno la Mungu. 
Ili kupata mazao,mkulima ni sharti apande mbegu na mazao yatatokana na mbegu yenyewe,katika mfano huu 'mbegu' aliyoipanda mpanzi ni neno la mungu,ni sheria na utaratibu wa maisha yanayompendeza mungu ulioainishwa wazi katika biblia yake takatifu.
 
 
Udongo ni mioyo yetu.
Mbegu ili iweze kuzaa matunda mengi na bora hutegemea sana ubora wa udongo ambao mbegu hiyo hupandwa,vivyo hivyo katika ufalme wa mungu ili neno liweze kufanya kazi yake ipasavyo ni lazima mioyo yetu iwe tayari kulipokea na kuliamini ndipo wokovu wa kweli huchukua nafasi na kubadili maisha yetu toka katika dhambi kwenda katika wokovu.
 
Wale wa karibu na njia.
kuna watu hubahatika kusikiliza mahubiri au kusoma neno la mungu katika biblia takatifu na kulipokea neno mioyoni mwao na kuanza kuishi maisha matakatifu katika KRISTO, lakini kabla hawajakua kiroho hupotoshwa na kurejea kuishi katika maisha yao ya uzinzi,ulevi,wizi,usaliti,uchoyo,ubinafsi hata ushirikina kama waliyokuwa wakiishi kabla ya kupokea wokovu wa YESU, hawa
ndio wasikiao, kisha huja Ibilisi akaliondoa hilo neno mioyoni mwao, wasije wakaamini na kuokoka,
 
Wale wa penye mwamba.
Kuna binadamu ambao katika hatua yao ya mwanzo kabisa kulipokea neno iwe ni kwa njia ya mahubiri,kusoma au pengine kwa njia ya nyimbo za kumsifu bwana faraja ya KRISTO iliwaingia na kufanyika furaha isiyo kifani ndani yao,lakini baada ya muda mfupi pindi wapambanapo na vikwazo na majaribu mbalimbali kama vile kuteswa,kutengwa,kushindwa,kukataliwa hata kuaibika.neno(mbegu) hukosa mizizi(imani) na kushindwa kumea.hawa ndio wale ambao wasikiapo hulipokea lile neno kwa furaha; nao hawana mizizi, huamini kitambo kidogo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga.
 
Zilizo anguka penye miiba.
Katika dunia hii ya leo,dunia iliyojaa chuki,wivu,tamaa na usaliti karibu robo nne ya wanadamu wametambua umuhimu wa kulipokea neno na kumwamini YESU KRISTO kama mwokozi wao,miongoni mwao wamelisikia neno labda kupitia mahubiri,televisheni,biblia,nyimbo za injili au kushiriki misa na matamasha ya kidini lakini kabla neno hilo(mbegu) halijaota mizizi na kuchipua(kukua kiroho) watu hawa wamedanganyika na starehe za kupita za hii dunia kama ulevi,uzinzi na tamaa ya pesa na kujikuta imani yao imetoweka.hawa ni wale waliosikia, na katika kuenenda kwao husongwa na shughuli na mali, na anasa za maisha haya, wasiivishe lo lote. 
 
 
Zile za penye udongo mzuri.
Kama vile ambavyo mbegu huchipua kukua na kuzaa matunda ipandwapo katika udongo mzuri,basi watu hawa wamepata kusikia habari njema na msamaha wa dhambi zao kupitia damu ya YESU KRISTO iliyomwagika pale msalabani na kuamua kulipokea neno mioyoni mwao,kulishika,kuliamini na kulitenda bila kujali mateso na vikwazo wanavyopambana navyo katika maisha ya imani kama vile kukashifiwa,kuchekwa,kudharauliwa na kudhihakiwa.hawa ndio wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno, na kulishika; kisha huzaa matunda kwa kuvumilia.
 
Sisi ni akina nani?
Mpendwa mkristo mwenzangu,kabla masiah hajafafanua mfano huu alinena na kupaza sauti akawaambia wafuasi wake "ninyi mmepewa kuzijua siri za ufalme wa Mungu; bali wengine kwa mifano, ili wakiona wasione, na wakisikia wasielewe".Japo alikuwa akizungumza na wafuasi wake,lakini hii inatuhusu moja kwa moja mimi na wewe ambao kupitia maandiko matakatifu kwa uwezo wa roho mtakatifu tumepata kuujua ukweli juu ya ufalme wa mungu basi tuupoke mioyoni mwetu na tusiwe kama wengine(wasioamwamini YESU) ambao pamoja miujiza,uponyaji na ufufuko wa bwana wetu YESU KRISTO hawaoni na pamoja na mahubiri,nyimbo na hata maombezi bado hawajafungua mioyo yao na kulipokea neno(mbegu) la mungu ili liweze kukua ndani yao na kufanya waishi maisha yanayompendeza muumba hapa duniani na mbinguni pia.
Buscar
Categorías
Read More
2 KINGS
Verse by verse explanation of 2 Kings 19
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 30 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-03-19 20:41:42 0 5K
GENESIS
THE BOOK OF GENESIS
  TY GENESIS 1 Verse by verse explanation of Genesis 1 Questions on Genesis 1 GENESIS 2...
By GOSPEL PREACHER 2021-08-26 05:35:22 0 5K
2 KINGS
Verse by verse explanation of 2 Kings 10
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 32 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-03-19 19:57:23 0 4K
OTHERS
Islam offers HELL and that is all
Allah Promised hell for his followers:  Sura 3:185, "Every soul shall have a taste of...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 10:08:53 0 5K
REVELATION
UFUNUO 10
Shalom…Karibu katika mwendelezo wa Kitabu cha Ufunuo..ambapo leo kwa Neema za Bwana...
By GOSPEL PREACHER 2021-10-30 11:05:02 0 5K