• Hizo Picha hapo zinakumbusha siku ya Muhimu sana katika Maisha yangu siku AMBAYO nimezaliwa upya YOHANA 1:12-13,Pia ni siku niliyozikwa na kufufuliwa katika Kristo Yesu.Kolosai 3:1-4,Efeso 2:4-7,.Bwana amenivusha Toka misri vyote vya misri vimezikwa,mimi sasa ni kiumbe kipya yakale yamekuwa mapya.Nami nitashinda ulimwengu huu uliojaa kila namna ya uovu.Neema ya Bwana inanipa uwezo wa kushinda ulimwengu kwasababu nimezaliwa upya Tito 2:11-12,Kila kilicho zaliwa na Mungu kitaushinda Ulimwengu.
    1 Yohana 5
    ⁴ Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.
    ⁵ Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu?
    ⁶ Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika maji na katika damu.
    ⁷ Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli.
    ⁸ Kwa maana wako watatu washuhudiao
    [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.TUMAINI LANGU LOTE NIMEWEKA KWAKO YESU
    MUNGU AWABARIKI SANA
    Hizo Picha hapo zinakumbusha siku ya Muhimu sana katika Maisha yangu siku AMBAYO nimezaliwa upya YOHANA 1:12-13,Pia ni siku niliyozikwa na kufufuliwa katika Kristo Yesu.Kolosai 3:1-4,Efeso 2:4-7,.Bwana amenivusha Toka misri vyote vya misri vimezikwa,mimi sasa ni kiumbe kipya yakale yamekuwa mapya.Nami nitashinda ulimwengu huu uliojaa kila namna ya uovu.Neema ya Bwana inanipa uwezo wa kushinda ulimwengu kwasababu nimezaliwa upya Tito 2:11-12,Kila kilicho zaliwa na Mungu kitaushinda Ulimwengu. 1 Yohana 5 ⁴ Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu. ⁵ Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu? ⁶ Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika maji na katika damu. ⁷ Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli. ⁸ Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.TUMAINI LANGU LOTE NIMEWEKA KWAKO YESU MUNGU AWABARIKI SANA
    Like
    Love
    6
    8 Kommentare 0 Geteilt 5KB Ansichten 0 Bewertungen
  • JE, KUNATOFAUTI KATI YA KUPUNGA PEPO NA KUTOA PEPO?

    Katika nyakati hizi za mwisho kumekuwa na roho nyingi zidanganyazo binadamu. Roho hizi za mpinga Kristo zinawadanganya wengi na kuwafanya wengi wajione kana kwamba wako na Mungu, kumbe Mungu hayupo kati yao na/au ndani ya maisha yao.

    Katika soma hili, tutajifunza tofauti iliyopo kati ya Kupunga Pepo na Kutoa Pepo kwa ushaidi wa aya takatifu za Biblia.
    ( TIMOTHEO 4:1 ).
    “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza  roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani”. Miongoni mwa mambo ya siku hizi za mwisho ni roho hizo kuwafanya watu wadanganyike na kufuata mafundisho ya uongo. Hao ni wale wanaoikataa ile kweli.

    (2 TIMOTHEO 4:3-5 )
    “Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia walimu makundi makundi kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo”.

    (2 WATHESALONIKE 2:7-12 )
    Watu ambao hawataki mafundisho ya utakatifu lakini wanataka kuona nguvu za Mungu maishani mwao, watadanganywa kwa ishara na ajabu za uongo.
    Katika nyakati hizi tunaweza kuona jinsi watu wanavyofanyiwa maombezi kwa kuangushwa chini na hatimaye kusimama bila kupokea muujiza wa uponyaji. Utaweza kuona watu wamejazana madhabahuni wakigaagaa chini na baadaye husimama na kuondoka lakini wakati mwingine huchukua muda mrefu kwao kusimama na kuondoka.

    Jambo la kushangaza ni siku zote kuonekana watu haohao , mapepo yao hayatoki. Miujiza hii imeenea kote duniani, uatakuta watu wanapiga kelele lakini pepo hawawatoki watu hao. Miujiza ya kimungu huondoa pepo kabisa ndani ya mtu tena kwa mamlaka na kumwacha akiwa mzima. Watu hawa hawafanyi miujiza ya uponyaji bali wanapunga pepo.

    Ni muhimu kujua kuwa  hata wapagani wanaweza kupunga pepo na kuwafanya wapige kelele. Waganga wa kienyeji wanaweza kupunga pepo lakini hawawezi kuwatoa. Tunawaona wapunga pepo wakitaka kutoa pepo lakini wanashindwa  ( MATENDO 19:13-16 ). Watu hawa walikuwa wa kawaida lakini leo tungewaita walokole kwa kuwa walikuwa watu wa dini.

    Jina jingine linalotumika kwa wapunga pepo ni” wapandisha pepo”. Mungu anasema kila anayepandisha pepo ni chukizo mbele zake ( KUMBUKUMBU LA TORATI 18:9-14 ). Waganga wa kienyeji ni wapandisha pepo au wapunga pepo. Kuna mazingira fulani  yanaandaliwa ili pepo wajidhihirishe kwao. Wanaimba na kuchezacheza ili nguvu hiyo ya shetani  iwe dhahiri kwa mfano  wetu tunavyofanya  katika kusifu au kuabudu ili nguvu ya Mungu ionekane  au idhihirike. Mfano Paulo na Sila gerezani walimsifu Mungu na nguvu za Mungu zikashuka milango ya gereza ikafunguka.

    Kazi tuliyoitiwa  ni ya kutoa pepo na siyo kupunga au kupandisha pepo ( MARKO 16:17 ‘Na ishara hizi zitafuatana nao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo”. MATHAYO 12:22-28 ). Kazi ya kupunga pepo ni ya shetani. Yesu aliuliza,” je, wana wenu huwatoa kwa nani?”. Swali hili la Yesu lilielekezwa kwa afarisayo walioishangazwa na mamlaka yake ya kuponya wagonjwa na kutoa pepo. Kimsingi hapo alikuwa akiuliza kuhusiana na wapunga pepo au wapandisha  pepo, kwamba wao wanatumia nguvu gain?

    Kuna madaraja katika majeshi ya pepo. Katika kutoa kafara tofautitofauti kubwa au ndogo ndipo Mganga anapoweza  kupata pepo wa daraja la juu au la chini. Huyo anayelipa  leseni kubwa yaani kafara , anapewa uwezo mkubwa wa kipepo. Anakuwa na mamlaka makuu kama kamanda wa Jeshi hivyo anaweza kuwaamuru pepo kumwingia mtu na kunyamanzisha pepo wadogo waliomo ndani ya mtu lakini hatimaye hari ya huyo mtu baadaye inakuwa mbaya zaidi kwa sababu idadi yao ( pepo ) imeongezeka.


    (MARKO 6:7 )
    “Akawaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu”. Pepo wachafu wanakaa ndani ya mtu mchafu. Ni mfano wa Inzi, hukaa katika uchafu. Kwa hiyo pepo wachafu hukaa ndani ya mtu mwenye dhambi. Dhambi ni uchafu ( ZEKARIA 3:3-4 ). Baba ( mwanzilishi ) wa maovu yote ni Ibilisi ( Shetani ) na huyo ndiye baba yao watendao dhambi ( YOHANA 8:44 ).

    (YAKOBO 4:4 )
    “Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu” Shetani ni mungu wa dunia hii ( 2 WAKORINTHO 4:4 ). Kuwa rafiki wa dunia ni kufanya yaleyale wanayoyafanya watu wa dunia hii ambao hawajaokolewa kwa kiumwamini Yesu Kristo. Watu wa dunui maisha yao ni maisha ya dhambi tu maana wao wanayafanya mapenzi ya mungu wa dunia ( baba yao ). Tukianza kuiga kuvaa kwao, kuongea kwao,  kucheza kwao, na mambo mengine mengi yasiyompendeza Mungu, Tutamfungulia Shetani mlango wa kuingia na kufanya maskani ndani yetu. Machizo yote tuwe mbali nayo ( YEREMIA 32:33-34; KUMBUKUMBU 7:26 ). Machukizo yanamfanya Mungu kutuacha kabisa ( 2 NYAKATI 36:14-16 ).

    Uweza wa Mungu wa kuponya unaweza usiwepo mahali kwa sababu ya kuwepo kwa machukizo. Makuhani nao wanaweza kutenda dhambi na kuingiza machukizo ndani ya nyumba ya Mungu kama tunavyoona katika andiko hilo juu. Watumishi wengi wanatamani kuziona nguvu za Mungu katika huduma zao kama wakati wa Mitume lakini gharama zake zinawashinda. Mungu hawezi kumtumia mtu mchafu ambaye siyo mtakatifu ( WAEBRANIA 1:9 ).

    Hivyo basi, vitu vyote tunavyovaa katika miili yetu ambavyo siyo vya mwili kwa asili yake  ni machukizo kwa Bwana. Kuvaa Mapambo na nywele za bandia ni machkizo kwa Bwana. Kama ingekuwa ni mapenzi ya Mungu tuvae Kwa mfano Heleni, Mungu angeweka tundu kwenye masikio yetu ili kutuandaa kwa ajili ya mapambo. (  1 TIMOTHEO 2:9-10; 1 PETRO 3;3-5;  ISAYA 29:16; WARUMI 9:19-21 ).

    Hatutaweza kuziona nguvu za Mungu katika maisha yetu kama nyakati za Mitume ni mpaka kanisa la sasa litakapotambua kuwa msingi wa Mitume na Manabii ulishaachwa ( WAEFESO 2:20 ). Mitume waliwafundisha watu kutokufuata fasheni ( namna ) za ulimwengu huu lakini leo hii mafundisho yamna hii ni dadra sana kuyasikia ( WARUMI 12:2 ).

    Pia waliweka msisitizo juu ya kutokufuata mataifa kufanya hili au lile wafanyalo kwa sababu nia za Mataifa ni batiri ( WAEFESO 4:17 ). Kati ya mataifa kuna makahaba ambao kazi yao ya ukahaba inawafanya kutafuta mavazi ya kuvaa ambayo yatawafanya hao wanaotafutwa kuvutika na kuwafuata katika uchafu. Biblia yetu imetaja mavazi ya kikahaba ( MITHALI 7:10 ). Fasheni nyingi za kidunia zinadizainiwa  na mkuuwa dunia na mfalme wa uwezo wa anga  ( WAEFESO 2:1-3 ).
    JE, KUNATOFAUTI KATI YA KUPUNGA PEPO NA KUTOA PEPO? Katika nyakati hizi za mwisho kumekuwa na roho nyingi zidanganyazo binadamu. Roho hizi za mpinga Kristo zinawadanganya wengi na kuwafanya wengi wajione kana kwamba wako na Mungu, kumbe Mungu hayupo kati yao na/au ndani ya maisha yao. Katika soma hili, tutajifunza tofauti iliyopo kati ya Kupunga Pepo na Kutoa Pepo kwa ushaidi wa aya takatifu za Biblia. ( TIMOTHEO 4:1 ). “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza  roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani”. Miongoni mwa mambo ya siku hizi za mwisho ni roho hizo kuwafanya watu wadanganyike na kufuata mafundisho ya uongo. Hao ni wale wanaoikataa ile kweli. (2 TIMOTHEO 4:3-5 ) “Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia walimu makundi makundi kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo”. (2 WATHESALONIKE 2:7-12 ) Watu ambao hawataki mafundisho ya utakatifu lakini wanataka kuona nguvu za Mungu maishani mwao, watadanganywa kwa ishara na ajabu za uongo. Katika nyakati hizi tunaweza kuona jinsi watu wanavyofanyiwa maombezi kwa kuangushwa chini na hatimaye kusimama bila kupokea muujiza wa uponyaji. Utaweza kuona watu wamejazana madhabahuni wakigaagaa chini na baadaye husimama na kuondoka lakini wakati mwingine huchukua muda mrefu kwao kusimama na kuondoka. Jambo la kushangaza ni siku zote kuonekana watu haohao , mapepo yao hayatoki. Miujiza hii imeenea kote duniani, uatakuta watu wanapiga kelele lakini pepo hawawatoki watu hao. Miujiza ya kimungu huondoa pepo kabisa ndani ya mtu tena kwa mamlaka na kumwacha akiwa mzima. Watu hawa hawafanyi miujiza ya uponyaji bali wanapunga pepo. Ni muhimu kujua kuwa  hata wapagani wanaweza kupunga pepo na kuwafanya wapige kelele. Waganga wa kienyeji wanaweza kupunga pepo lakini hawawezi kuwatoa. Tunawaona wapunga pepo wakitaka kutoa pepo lakini wanashindwa  ( MATENDO 19:13-16 ). Watu hawa walikuwa wa kawaida lakini leo tungewaita walokole kwa kuwa walikuwa watu wa dini. Jina jingine linalotumika kwa wapunga pepo ni” wapandisha pepo”. Mungu anasema kila anayepandisha pepo ni chukizo mbele zake ( KUMBUKUMBU LA TORATI 18:9-14 ). Waganga wa kienyeji ni wapandisha pepo au wapunga pepo. Kuna mazingira fulani  yanaandaliwa ili pepo wajidhihirishe kwao. Wanaimba na kuchezacheza ili nguvu hiyo ya shetani  iwe dhahiri kwa mfano  wetu tunavyofanya  katika kusifu au kuabudu ili nguvu ya Mungu ionekane  au idhihirike. Mfano Paulo na Sila gerezani walimsifu Mungu na nguvu za Mungu zikashuka milango ya gereza ikafunguka. Kazi tuliyoitiwa  ni ya kutoa pepo na siyo kupunga au kupandisha pepo ( MARKO 16:17 ‘Na ishara hizi zitafuatana nao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo”. MATHAYO 12:22-28 ). Kazi ya kupunga pepo ni ya shetani. Yesu aliuliza,” je, wana wenu huwatoa kwa nani?”. Swali hili la Yesu lilielekezwa kwa afarisayo walioishangazwa na mamlaka yake ya kuponya wagonjwa na kutoa pepo. Kimsingi hapo alikuwa akiuliza kuhusiana na wapunga pepo au wapandisha  pepo, kwamba wao wanatumia nguvu gain? Kuna madaraja katika majeshi ya pepo. Katika kutoa kafara tofautitofauti kubwa au ndogo ndipo Mganga anapoweza  kupata pepo wa daraja la juu au la chini. Huyo anayelipa  leseni kubwa yaani kafara , anapewa uwezo mkubwa wa kipepo. Anakuwa na mamlaka makuu kama kamanda wa Jeshi hivyo anaweza kuwaamuru pepo kumwingia mtu na kunyamanzisha pepo wadogo waliomo ndani ya mtu lakini hatimaye hari ya huyo mtu baadaye inakuwa mbaya zaidi kwa sababu idadi yao ( pepo ) imeongezeka. (MARKO 6:7 ) “Akawaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu”. Pepo wachafu wanakaa ndani ya mtu mchafu. Ni mfano wa Inzi, hukaa katika uchafu. Kwa hiyo pepo wachafu hukaa ndani ya mtu mwenye dhambi. Dhambi ni uchafu ( ZEKARIA 3:3-4 ). Baba ( mwanzilishi ) wa maovu yote ni Ibilisi ( Shetani ) na huyo ndiye baba yao watendao dhambi ( YOHANA 8:44 ). (YAKOBO 4:4 ) “Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu” Shetani ni mungu wa dunia hii ( 2 WAKORINTHO 4:4 ). Kuwa rafiki wa dunia ni kufanya yaleyale wanayoyafanya watu wa dunia hii ambao hawajaokolewa kwa kiumwamini Yesu Kristo. Watu wa dunui maisha yao ni maisha ya dhambi tu maana wao wanayafanya mapenzi ya mungu wa dunia ( baba yao ). Tukianza kuiga kuvaa kwao, kuongea kwao,  kucheza kwao, na mambo mengine mengi yasiyompendeza Mungu, Tutamfungulia Shetani mlango wa kuingia na kufanya maskani ndani yetu. Machizo yote tuwe mbali nayo ( YEREMIA 32:33-34; KUMBUKUMBU 7:26 ). Machukizo yanamfanya Mungu kutuacha kabisa ( 2 NYAKATI 36:14-16 ). Uweza wa Mungu wa kuponya unaweza usiwepo mahali kwa sababu ya kuwepo kwa machukizo. Makuhani nao wanaweza kutenda dhambi na kuingiza machukizo ndani ya nyumba ya Mungu kama tunavyoona katika andiko hilo juu. Watumishi wengi wanatamani kuziona nguvu za Mungu katika huduma zao kama wakati wa Mitume lakini gharama zake zinawashinda. Mungu hawezi kumtumia mtu mchafu ambaye siyo mtakatifu ( WAEBRANIA 1:9 ). Hivyo basi, vitu vyote tunavyovaa katika miili yetu ambavyo siyo vya mwili kwa asili yake  ni machukizo kwa Bwana. Kuvaa Mapambo na nywele za bandia ni machkizo kwa Bwana. Kama ingekuwa ni mapenzi ya Mungu tuvae Kwa mfano Heleni, Mungu angeweka tundu kwenye masikio yetu ili kutuandaa kwa ajili ya mapambo. (  1 TIMOTHEO 2:9-10; 1 PETRO 3;3-5;  ISAYA 29:16; WARUMI 9:19-21 ). Hatutaweza kuziona nguvu za Mungu katika maisha yetu kama nyakati za Mitume ni mpaka kanisa la sasa litakapotambua kuwa msingi wa Mitume na Manabii ulishaachwa ( WAEFESO 2:20 ). Mitume waliwafundisha watu kutokufuata fasheni ( namna ) za ulimwengu huu lakini leo hii mafundisho yamna hii ni dadra sana kuyasikia ( WARUMI 12:2 ). Pia waliweka msisitizo juu ya kutokufuata mataifa kufanya hili au lile wafanyalo kwa sababu nia za Mataifa ni batiri ( WAEFESO 4:17 ). Kati ya mataifa kuna makahaba ambao kazi yao ya ukahaba inawafanya kutafuta mavazi ya kuvaa ambayo yatawafanya hao wanaotafutwa kuvutika na kuwafuata katika uchafu. Biblia yetu imetaja mavazi ya kikahaba ( MITHALI 7:10 ). Fasheni nyingi za kidunia zinadizainiwa  na mkuuwa dunia na mfalme wa uwezo wa anga  ( WAEFESO 2:1-3 ).
    0 Kommentare 0 Geteilt 5KB Ansichten 0 Bewertungen
  • JE YESU WA WAKRISTO NDIYE YULE ISA WA WAISLAM?

    Mara kwa mara, unaweza kuwasikia Waislamu wakisema kuwa Isa a.s. kama anavyotajwa ndani ya Qur’an tukufu, ndiye Yesu Kristo wa Nazareti, kama anavyotajwa ndani ya Biblia Takatifu. Wanafanya hivyo kwa kulinganisha baadhi ya aya zilizomo ndani ya Biblia Takatifu, na zile zilizomo ndani ya Qur’an.

    Kwa mfano, wanasema kwa mujibu wa Biblia mama yake Yesu Kristo anaitwa Mariamu. Wanasoma katika Injili ya Marko 6:3-4“Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose na Yuda na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake” . Wanafananisha aya hiyo na ile iliyomo ndani ya Qur’an katika Suratul Al-Maidah, 5:75 “ Masih bin Maryam si chochote ila ni mtume tu……”,

    Hoja nyingine wanayoitumia ni kusema kwamba eti jina Isa ni katika lugha ya Kiarabu. Jambo hilo siyo kweli. Kwa sababu katika lugha ya Kiarabu, Yesu anaitwa Yasu’a siyo Isa. Na ikumbukwe kuwa Biblia ndicho kitabu kilichotangulia kuwepo duniani miaka ipatayo 1500 kabla ya Qur’an. Hoja yetu kwa Waislamu ni hii nani aliyebadilisha jina Yasu’a kuwa Isa?.

    Jina Yasu’a linashabihiana zaidi na Jina Yehoshua ambalo hilo ni katika lugha ya Kiebrania, na katika Kiyunani lugha iliyotumika kuandika Agano Jipya anaitwa Iesous (tamka Yesu) tafsiri ya maneno hayo kwa lugha ya Kiswahili ni Mwokozi. Tunasoma hayo katika Math 1:21-23 “ Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana yeye ndiye atakaye waokoa watu wake na dhambi zao.

    Hayo yote yamekuwa ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa Nabii akisema Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.” Hoja yetu Je Isa a.s naye ni Mwokozi na Imanueli kama alivyo Yesu Kristo? Jambo jingine tunalopaswa kulizingatia tunapoangalia tofauti zao ni kuhusu mama zao. Mama yake Yesu Kristo ni Mariam anayetoka katika ukoo wa Yuda. Tunasoma hayo katika kitabu cha Mwanzo 49:10 “ Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake,Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki,Ambaye mataifa watamtii”. Unabii huu umetimia kwa Yesu Kristo.

    Tunasoma hayo katika Waebrania 7:14 “Maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambayo Musa hakunena neno lolote juu yake katika mambo ya ukuhani” Lakini tusomapo habari za Isa, yeye mama yake anatoka ukoo wa Imrani. Ambaye ni baba yao Haruni, Miriamu na Musa. Tunayasoma hayo katika Suratul Al-Maryam 19:28 “Ewe dada yake Haruni. Baba yako hakuwa mtu mbaya. Wala mama yako hakuwa hasharati”.

    fafanuzi unaoifafanua aya hii ya 19:28 uliyomo ndani ya Qur’an, tafsiri ya King Fahd uk. 405, unasomeka hivi “ This Harun (Aaron) is not the brother of Musa (Moses), but he was another pious man at the time of Maryam (Mary)” Tafsiri “Huyu Harun siyo ndugu yake Musa, bali alikuwa ni mtu mwingine tu mcha Mungu, aliyeishi wakati wa kipindi cha Maryam” Kwa mujibu wa Biblia, Haruni ni mtoto wa mzee Amran na mama yao anaitwa Yekobedi na kwao wamezaliwa watoto watatu Haruni, Miriam na mdogo wao Musa. Tunasoma hayo katika kitabu cha Hesabu 26:59 “Na jina la mke wa Amramu aliitwa Yokebedi binti wa Lawi ,ambaye alizaliwa kwake Lawi huko Misri; na huyo Yokebedi akamzalia Amram Haruni,na Musa,na Miriamu umbu lao” Tofauti nyingine ni kuumbwa kwao:

    1) ISSA KAUMBWA. Qur’an Suratul Imran, 3:59 “ Bila shaka hali ya Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama hali ya Adam; alimwumba kwa udongo kisha akamwambia: “Kuwa”; basi akawa” Lakini tusomapo kumhusu YESU, YEYE HAKUUMBWA BALI NI NENO LA MUNGU. Yoh 1 : 1,14 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu……..Naye Neno alifanyika mwili akakaa kwetu…….” Mika 5:2 “ Bali wewe, Bethlehem Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israel; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele” Yoh: 8:58 “ Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahim asijakuwako, mimi niko”. Zaidi ya hayo Biblia inatujulisha kuwa yeye ndiye Muumbaji mwenyewe Yoh 1:3 “Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika” Kol 1:16-17 “ Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana ; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake na kwa ajili yake”

    2) (A) ISSA A.S : BAADA YA KUONDOKA KWAKE, (KAMA WAISLAMU WANAVYOAMINI), HAJAWAHI KUTOKEA KWA NAMNA YOYOTE ILE. (B) YESU KRISTO: BAADA YA KUONDOKA KWAKE ALIMTOKEA PAUL (SAUL). Mdo 9:4 “ Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Saul, Saul, mbona waniudhi? Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema , Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe”

    3) (A) ISSA A.S: ALITABIRI KUJA KWA MUHAMMAD Quran Suratul As Saff , 61:6 “Na (wakumbushe) aliposema (Nabii) Isa bin Maryamu (kuwaambia mayahudi) enyi wana wa Israili! mimi ni mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu. Nisadikishaye yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati. Na kutoa habari njema ya mtume atakayewajia nyuma yangu ambaye jina lake litakuwa Ahmad(Muhammad). Na maana ya majina mawili yote haya ni moja. Maana yake Mwenye kushukuriwa kwa maneno yake mazuri na vitendo vyake vizuri na kila chake kwani vyake vyote ni vizuri).Lakini alipowajia kwa hoja zilizowazi walisema: “ Huu ni udanganyifu uliyo dhahiri”. (B)YESU KRISTO ALIMTUMA ROHO MTAKATIFU KATIKA SIKU YA PENTEKOSTE. Yoh: 14:26 “.Lakini huyo Msaidizi,huyo Roho Mtakatifu,ambaye Baba atampeleka kwa jina langu,atawafundisha yote,na kuwakumbusha yote niliyowaambia”. Katka Kiyunani anaitwa “Paracletos” yaani msaidizi au mfariji Yoh 15:26 “ Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia” Yoh 16:7 “Lakini mimi ninawaambia iliyo kweli; yawafaa nyinyi mimi niondoke,kwa maana mimi nisipoondoka huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu nitampeleka kwenu”.

    4) (A) ISSA A.S : JINA LAKE HALINA NGUVU WALA UWEZO WA KUOKOA BALI NI RANGI MBILI Katika Al-Lu’lu’war-Marjani, Juzuu na1, Hadithi na104 uk. 64 “ Hadithi ya Ibn Abbas (r.a) kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema, “Nilimuona Musa (a.s) katika usiku wa Al-Isra, niliopelekwa,naye ni mtu mrefu, mwenye nywele za hudhurungi zimejikunjakunja kama mtu wa Shanua.Na nilimuona Isa (a.s), naye ni mtu wa wastani wa umbo, unaelekea kwenye wekundu na weupe, ana nywele zilizonyooka……” (B) YESU KRISTO: JINA LAKE NI WOKOVU. Mdo 4:9-10,12 “ kama tukiulizwa leo habari ya jambo jema alilofanyiwa yule mtu dhaifu,jinsi alivyoponywa, jueni nyinyi nyote na watu wote wa Israel ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye nyinyi mlimsulubisha, na Mungu alimfufua katika wafu kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu…………………….Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” Baadhi ya aya ndani ya Qur’an zinaeleza kuwa Isa a.s aliwaponya wenye upofu. Ni akina nani hao tutajiwe angalau mmoja? Yesu alimponya kipofu Batromayo. Aya zingine zinasema Isa a.s alifufua wafu. Ni akina nani hao? Yesu alimfufua Lazaro. Jina tulilopewa ni jina moja tu lenye wokovu la Yesu Kristo. Jina la Isa a.s lisilo na wokovu limehusishwaje na jina la Yesu Kristo wa Nazareth lenye wokovu? Mdo 16:31 “ Wakamwambia , Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka wewe pamoja na nyumba yako.”

    5) (A) ISSA.A.S : YEYE SIYO MWANA WA MUNGU. Qur’ani Suratul Al An-Am,6:101 “Yeye ndiye Mwumba wa mbingu na ardhi. inamkinikanaje awe na mwana, hali hana mke. Naye ndiye aliye umba kila kitu (sio baadhi yake kavizaa). Naye ni mjuzi wa kila kitu”. Qurani Suratul At-Tawba (Kutubu), 9:30 “Na Mayahudi wanasema “Uzeri ni mwana wa Mwenyezi Mungu” na “Wakristo wanasema “Masihi ni Mwana wa Mwenyezi Mungu” Haya ndiyo wasemayo kwa vinywa vyao (pasi na kuyapima). Wanayaiga maneno ya wale waliokufuru kabla yao, Mwenyezi Mungu awaangamize. Wanageuzwa namna gani hawa! Fundisho la Uwana wa Mungu kama Biblia inavyofundisha, halimo katika mafundisho na itikadi ya dini ya Kiislamu kwa hiyo Isa a.s siyo mwana wa Mungu. (B) YESU KRISTO: YEYE NI MWANA WA MUNGU. Luka 1:30-31,35 “Malaika akamwambia usiogope Mariamu,kwa maana umepata neema kwa Mungu.Tazama utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Malaika akajibu akamwambia,Roho Mtakatifu atakujilia juu yako,na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli;kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu Mwana wa Mungu. Hivyo Isa siyo Mwana Mungu lakini Yesu ni mwana wa Mungu. Kwa hivyo Yesu siyo Isa. 6) (A) ISSA A.S: YEYE SIYO MUNGU ALIYEFANYIKA MWILI. Suratul Al- Maidah,(meza), 5:72-73 Bila ya shaka wamekufuru wale waliosema, “ Mwenyezi Mungu ni Masih (issa)bin Maryam”.(Na hali ya kuwa)Masihi alisema “Enyi wana wa Israel! Mwabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wenu. Kwani anayemshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharimishia Pepo, na mahali pake (patakuwa) ni Motoni. Na madhalimu hawatakuwa na wasaidizi (wa kuwasaidia siku ya Kiama) “Kwa hakika wamekufuru wale waliosema mwenyenzi Mungu ni mmoja katika (wale waungu) watatu (yeye ndiye watatu wao ) hali hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu mmoja ( tu peke yake) na kama hawataacha hayo wasemayo kwa yakini itawakamata wale wanaoendelea na ukafiri miongoni mwao adhabu iumizayo”. (B)YESU YEYE NI NENO LA MUNGU LILILOFANYIKA MWILI: Yoh 1 : 1,14 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu……..Naye Neno alifanyika mwili akakaa kwetu…….”

    7) (A) ISSA A.S YEYE HAJAWAHI KUSULUBIWA WALA KUUWAWA Qurani Suratul An-Nisaa (Wanawake) 4:157-158 “Na kwa (ajili ya )kusema kwao sisi tumemuua masihi Isa mwana wa Maryamu, mtume wa Mungu. Hali hawakumuua wala hawakumsulubu bali walibabaishiwa (mtu mwingine wakamdhani nabii Isa.) Na kwa hakika wale waliokhitalifiana katika (hakika)hiyo (ya kumuua nabii Isa) wamo katika shaka nalo (jambo hilo kusema kauwawa]. Wao (kabisa) hawana yakini juu ya (jambo)hili (la kuwa kweli wamemuua nabii isa) isipokuwa wanafuata dhana tu.Na kwa yakini hawakumuua. Bali mwenyenzi Mungu alimnyanyua kwake. Na mwenyenzi Mungu ni mwenye nguvu (na)mwenye hikima. (B)YESU KRISTO: YEYE ALISULUBIWA MSALABANI Yohana 19:18,31,33 “Wakamsulibisha huko,na wengine wawili pamoja,mmoja huku na mmoja huku, na Yesu katikati.Basi Wayahudi, kwa sababu ni Maandalio, miili isikae juu ya misalaba siku ya sabato(maana sabato ile ilikuwa siku kubwa), walimwomba Pilato miguu yao ivunjwe,wakaondolewe. Lakini walipomjia Yesu na kuona ya kuwa amekwisha kufa,hawakumvunja miguu”.

    8) (A) ISSA A.S HANA HADHI YA KUABUDIWA NA BINADAMU YEYOTE. Qur’an, Suratul Al-Maidah, 5:116 “ Na (kumbukeni) Mwnyezi Mungu atakaposema: “Ewe Isa bin Maryam! Je ,wewe uliwaambia watu: ‘Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu’?” Aseme (Nabii Isa): “Wewe umetakasika na kuwa na mshirika, hainijuzii mimi kusema ambayo si haki yangu (kuyasema, kwa kuwa ni ya uongo), kama ningalisema bila shaka ungalijua ; unayajua yaliyomo nafsini mwangu, lakini mimi siyajui yaliyomo nafsini mwako; hakika Wewe ndiye ujuaye mambo ya ghaibu. B) YESU ANASTAHILI KUABUDIWA NA WANADAMU NA MALAIKA Math 2: 2 “yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? kwa maana tuliiona nyota yake mashariki nasi tumekuja kumsujudia.” Yoh 9: 35 “ Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; naye alipomwona alisema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu? Naye akajibu akasema, Ni nani, Bwana, nipate kumwamini? Yesu akamwambia Umemwona, naye anayesema nawe ndiye. Akasema, naamini, Bwana, akamsujudia.” Filipi 2:10-11 “ili kwa Jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.” Ebr 1:6 “ Hata tena amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema, Na wamsujudu Malaika wote wa Mungu.

    9) (A) ISA HASTAHILI KUWA MWOMBEZI WA WATU KWA MUNGU Sahih Al-Bukhari, vol.6 ,Hadithi no 3, The Noble Qur’an, English Translation uk. 8 “…….Nenda kwa Musa, mtumishi wa Allah ambaye Allah alizungumza naye uso kwa uso na alimpa Torati. Hivyo watakwenda kwake naye atasema ‘ Mimi sistahili kwa jukumu hilo la uombezi, na atataja mauaji aliyoyafanya kwa mtu ambaye si muuaji, na hivyo atajisikia aibu mbele ya Mola wake, naye atasema nendeni kwa Isa, mtumishi wa Allah, Mjumbe wake neno lake na roho iliyotoka kwake. Isa atasema sistahili mimi kubeba jukumu la uombezi…….” B) YESU ANASTAHILI KUWA MWOMBEZI WA WANADAMU KWA MUNGU 1 Tim 2:5 “ Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu;” Ebr 7:24-25 “ bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka.Naye, kwa sababu hii , aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu Hai siku zote ili awaombee.

    10) (a) ISA NI NABII MWINGINE TU ASIYE TOFAUTI NA WENGINE Qur’an Suratul Baqarah, (ng’ombe)2:136 “ “Semeni nyinyi (Waislamu waambiwe Mayahudi na Manasara; waambieni): “Tumemwamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyoteremshiwa, na yale yaliyoteremshwa kwa Ibrahimu na Ismail na Is-haqa na Yaaqubu na kizazi (chake Yaaqubu); na waliyopewa Musa na Isa na pia yale waliyopewa Manabii (wengine) kutoka kwa Mola wao; hatutofautishi baina ya yoyote katika hao. (Wote tunawaamini); na sisi tumenyenyekea Kwake.” b) YESU YEYE YU JUU KULIKO VITU VYOTE Efeso 1:20-23 “ aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; juu sana kuliko ufalme wote, na malaika, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; akavitia vitu vyote chini ya miguu yake akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya Kanisa; ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.”

    11) (a) ISA ATAKAPORUDI, ATAOA NA KUZAA WATOTO Mishkat Al- Masabih, vol 2 uk.1159, Sahih Muslim, vol. 1 uk 92 “ Isa atakaporudi ataishi miaka arobaini (40), muda ambao atakuwa ameoa na kuzaa watoto, na atafanya ibada ya hija.” b) YESU ATAKAPORUDI ATAKUJA KULINYAKUA KANISA, YAANI BIBI ARUSI Efeso 5:25-26, 32-33 “ Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, Uf 19:7 “ Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana Kondoo imekuja na mkewe amejiweka tayari.akajitoa kwa ajili yake, ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;…..Siri hiyo ni kubwa ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa. Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mmewe.”

    12)(a) ISA ATAKUFA BAADA YA KUISHI MIAKA AROBAINI (40) Mishkat Al- Masabih, vol 2 uk. 1159,Sunan Abu Dawud, Hadithi 4310, Sahih Muslim, vol.1, uk.92 , “Isa atakaporudi ataondosha dini zote zisiwepo isipokuwa Uislamu. Atamharibu Masih Dajjal, na ataishi duniani miaka arobaini (40) na kisha atakufa. Na baada ya kufa atazikwa pembeni mwa kaburi la Muhammad.” B) YESU BAADA YA KUFUFUKA YU HAI SIKU ZOTE HAFI TENA Rum 6:9 “ tukijua ya kuwa Kristo akiisha kufufuka katika wafu hafi tena, wala mauti haimtawali tena.” Ebr 7:24-25 “ bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka.Naye, kwa sababu hii , aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu Hai siku zote ili awaombee.” Uf 1:17-18 “ Nami nilipomwona nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, mimi ni wa kwanza na wa mwisho, aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama , ni hai hata milele na milele nami ninazo funguo za mauti na za kuzimu.”

    13)(a) ISA ALIPOZALIWA SAUTI YA FARAJA ILITOKA CHINI YA ARDHI Qur’an Suratul Maryam,19:23-24 “ Kisha uchungu ukampeleka katika shina la mtende, (akawa anazaa na huku) anasema: “ Laiti ningekufa kabla ya haya, na ningekuwa niliyesahaulika kabisa.” Mara ikamfikia sauti kutoka chini yake (inamwambia): usihuzunike. Hakika Mola wako amejaalia (ameweka) kijito cha maji chini yako;” Mafundisho ya Kiislamu yanaeleza kuwa huko chini ya ardhi kuna mnyama. Na huyo mnyama anazijua aya za Qur’an. Qur’an katika Suratul Al-Naml, 27:82 “Na kauli (ya kuja kiyama) itakapowathibitikia Tutawatolea mnyama katika ardhi atakayewasemeza kwa sababu watu walikuwa hawaziyakinishi Aya Zetu” b) ALIPOZALIWA YESU SAUTI ZA MALAIKA ZILITOKA JUU Luka 2:13-16 “ Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu na kusema, Atukuzwe Mungu juu mbinguni na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia. Ikawa malaika hao walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji waliambiana, Haya na twendeni mpaka Bethlehemu, tukalione hilo lililofanyika alilotujulisha Bwana. Wakaenda kwa haraka wakamkuta Mariamu na Yusufu, na yule mtoto mchanga amelala horini”

    (14)(a) ISA HANA UFAHAMU WA MAMBO MBALIMBALI katika Al-Lu’lu’ war- Marjan,kitabu cha 3 Hadithi na 1528 uk.883 “Hadithi ya Abu Huraira (r.a) kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema “Issa Ibn Mariam (a,s) alimwona mtu anaiba akamuuliza umeiba? akasema hapana ,Naapa kwa Allah ambaye hakuna mola isipokuwa yeye .Issa (a.s) akasema nimemuamini Allah na limeniongopea jicho langu”. b) YESU ANAYAJUA YOTE Yohana 1:47-48 “ Basi Yesu akamwona Nathanael anakuja kwake, akanena habari zake “Tazama Mwizraeli kweli kweli hamna hila ndani yake. Nathaeli akamwambia umepataje kunitambua? Yesu akajibu akamwambia, Kabla Filipo hajakuita ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona” Yoh 2:24-25 “ Lakini Yesu hakujiaminisha kwao; kwa kuwa yeye aliwajua wote; na kwa sababu hakuwa na haja ya mtu kushuhudia habari za mwanadamu; kwa maana yeye mwenyewe aliyajua yaliyomo ndani ya mwanadamu”

    15) (a) ISA A.S MAMA YAKE ALIKUTWA PEMBEZONI MWA MSIKITI ALIPOLETEWA HABARI ZA KUZALIWA KWAKE. Qur’an Suratul Maryam,19:16-17 “ Na mtaje Mariamu kitabuni humu. Alipojitenga na jamaa zake, (akenda) mahali upande wa mashariki (wa msikiti) na akaweka pazia kujikinga nao. Tukampelekea muhuisha Sharia Yetu (Jibrili)- akajimithilisha kwake (kwa sura ya) binadamu aliye kamili b) YESU KRISTO, MAMA YAKE ALIKUTWA NYUMBANI KWAO NAZARETI Luka 1:26-28 “Mwezi wa sita malaika Gabriel alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti. Kwa mwana mwali Bikira aliyekuwa ameposwa na mtu jina lake Yusufu wa mbari ya Daudi. Na jina lake Bikira huyo ni Mariamu. Akaingia nyumbani kwake akasema, salamu uliyepewa neema Bwana yu pamoja nawe.”

    16)(a) MIMBA YA ISA ILIKUWA NI YA SIKU MOJA Qur’an Suratul Maryam,19:21-22 “ (Malaika) akasema: “ Nikama hivyo (unavyosema; lakini) Mola wako amesema ‘Haya ni sahali Kwangu, na ili Tumfanye muujiza kwa wanaasamu na rehema itokayo Kwetu (ndiyo Tumefanya hivi);’ Na hili ni jambo lililokwisha kuhukumiwa.” Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali” b) MIMBA YA YESU SIKU ZILITIMIA. Luka 2:6-7 “ ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia, akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni” NB: Mwezi wa sita uliotajwa katika Luka 1:26 ni mwezi wenye kuelezea umri wa mimba ya Yohana ndani ya tumbo la Elizabethi. Luka 1: 36 “ Tena tazama jamaa yako Elizabeti naye amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa” NB: Hori iliyotajwa hapa,ina maana ya chombo cha kulishia wanyama kinachokuwa ndani ya zizi. Kwa Kiyunani (Kigiriki) ambayo ndiyo lugha iliyotumika kuandikia Agano Jipya ,chombo hicho kinaitwa “Fatne” kwa Kiingereza kinaitwa “a manger”

    17)ISA (A.S) ATAKAPORUDI ATAKUJA KUVUNJA MISALABA NA KUUA NGURUWE Mkweli Mwaminifu, Juzuu 3-4, uk.20, Hadithi na. 753 “ Haisimami saa ya (kiyama) mpaka akuteremkieni nabii Isa (a.s) mwana wa Maryamu atahukumu (kwa sheria ya Kiislamu) (na) muadilifu, basi atavunja misalaba (ya Wakristo Makanisani) na ataua nguruwe, na ataondosha fedheha au (aibu), na mali itazidi kuwa nyingi sana mpaka hataikubali (ataikataa) mtu (kwa kuogopa kiyama)” .Soma pia katika Sahihi Bukhar, vol. 3, Hadithi na 425,. Al-Lu’lu’war-Marjan, juzuu ya 1,Hadithi na 95 uk.51. The Noble Qur’an uk.757 b)YESU KRISTO ATAKAPORUDI ATAWATUMA MALAIKA ZAKE KUWAKUSANYA WATAKATIFU Luka 24:30-31 “ ndipo itakapoonekana ishara ya mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi, naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.” ONYO LA YESU KRISTO WA NAZARETH Math 24:24 “ kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini hata walio wateule.” (Angalia pia Marko 13:22) Yoh 8:24 “ Kwa hiyo naliwambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye mtakufa katika dhambi zenu.”

    WEWE MTEULE JE UTADANGANYWA NA KUDANGANYIKA KUWA KWELI ISA A.S NDIYE YESU KRISTO? UKIAMINI HIVYO UTAKUWA UMEDANGANYIKA NA UTAKOSA WOKOVU WA MWENYEZI MUNGU!!!!!!!!!! YESU KRISTO, YEYE NI IMMANUEL, MSHAURI WA AJABU, MUNGU MWENYE NGUVU, BABA WA MILELE, MFALME WA AMANI!!!! (ISAYA 9:6, MATH 1:23) HIZI SIYO SIFA ZA Shkhê Êdén Hãzãrd kwa Max Shimba Ministries
    JE YESU WA WAKRISTO NDIYE YULE ISA WA WAISLAM? Mara kwa mara, unaweza kuwasikia Waislamu wakisema kuwa Isa a.s. kama anavyotajwa ndani ya Qur’an tukufu, ndiye Yesu Kristo wa Nazareti, kama anavyotajwa ndani ya Biblia Takatifu. Wanafanya hivyo kwa kulinganisha baadhi ya aya zilizomo ndani ya Biblia Takatifu, na zile zilizomo ndani ya Qur’an. Kwa mfano, wanasema kwa mujibu wa Biblia mama yake Yesu Kristo anaitwa Mariamu. Wanasoma katika Injili ya Marko 6:3-4“Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose na Yuda na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake” . Wanafananisha aya hiyo na ile iliyomo ndani ya Qur’an katika Suratul Al-Maidah, 5:75 “ Masih bin Maryam si chochote ila ni mtume tu……”, Hoja nyingine wanayoitumia ni kusema kwamba eti jina Isa ni katika lugha ya Kiarabu. Jambo hilo siyo kweli. Kwa sababu katika lugha ya Kiarabu, Yesu anaitwa Yasu’a siyo Isa. Na ikumbukwe kuwa Biblia ndicho kitabu kilichotangulia kuwepo duniani miaka ipatayo 1500 kabla ya Qur’an. Hoja yetu kwa Waislamu ni hii nani aliyebadilisha jina Yasu’a kuwa Isa?. Jina Yasu’a linashabihiana zaidi na Jina Yehoshua ambalo hilo ni katika lugha ya Kiebrania, na katika Kiyunani lugha iliyotumika kuandika Agano Jipya anaitwa Iesous (tamka Yesu) tafsiri ya maneno hayo kwa lugha ya Kiswahili ni Mwokozi. Tunasoma hayo katika Math 1:21-23 “ Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana yeye ndiye atakaye waokoa watu wake na dhambi zao. Hayo yote yamekuwa ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa Nabii akisema Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.” Hoja yetu Je Isa a.s naye ni Mwokozi na Imanueli kama alivyo Yesu Kristo? Jambo jingine tunalopaswa kulizingatia tunapoangalia tofauti zao ni kuhusu mama zao. Mama yake Yesu Kristo ni Mariam anayetoka katika ukoo wa Yuda. Tunasoma hayo katika kitabu cha Mwanzo 49:10 “ Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake,Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki,Ambaye mataifa watamtii”. Unabii huu umetimia kwa Yesu Kristo. Tunasoma hayo katika Waebrania 7:14 “Maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambayo Musa hakunena neno lolote juu yake katika mambo ya ukuhani” Lakini tusomapo habari za Isa, yeye mama yake anatoka ukoo wa Imrani. Ambaye ni baba yao Haruni, Miriamu na Musa. Tunayasoma hayo katika Suratul Al-Maryam 19:28 “Ewe dada yake Haruni. Baba yako hakuwa mtu mbaya. Wala mama yako hakuwa hasharati”. fafanuzi unaoifafanua aya hii ya 19:28 uliyomo ndani ya Qur’an, tafsiri ya King Fahd uk. 405, unasomeka hivi “ This Harun (Aaron) is not the brother of Musa (Moses), but he was another pious man at the time of Maryam (Mary)” Tafsiri “Huyu Harun siyo ndugu yake Musa, bali alikuwa ni mtu mwingine tu mcha Mungu, aliyeishi wakati wa kipindi cha Maryam” Kwa mujibu wa Biblia, Haruni ni mtoto wa mzee Amran na mama yao anaitwa Yekobedi na kwao wamezaliwa watoto watatu Haruni, Miriam na mdogo wao Musa. Tunasoma hayo katika kitabu cha Hesabu 26:59 “Na jina la mke wa Amramu aliitwa Yokebedi binti wa Lawi ,ambaye alizaliwa kwake Lawi huko Misri; na huyo Yokebedi akamzalia Amram Haruni,na Musa,na Miriamu umbu lao” Tofauti nyingine ni kuumbwa kwao: 1) ISSA KAUMBWA. Qur’an Suratul Imran, 3:59 “ Bila shaka hali ya Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama hali ya Adam; alimwumba kwa udongo kisha akamwambia: “Kuwa”; basi akawa” Lakini tusomapo kumhusu YESU, YEYE HAKUUMBWA BALI NI NENO LA MUNGU. Yoh 1 : 1,14 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu……..Naye Neno alifanyika mwili akakaa kwetu…….” Mika 5:2 “ Bali wewe, Bethlehem Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israel; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele” Yoh: 8:58 “ Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahim asijakuwako, mimi niko”. Zaidi ya hayo Biblia inatujulisha kuwa yeye ndiye Muumbaji mwenyewe Yoh 1:3 “Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika” Kol 1:16-17 “ Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana ; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake na kwa ajili yake” 2) (A) ISSA A.S : BAADA YA KUONDOKA KWAKE, (KAMA WAISLAMU WANAVYOAMINI), HAJAWAHI KUTOKEA KWA NAMNA YOYOTE ILE. (B) YESU KRISTO: BAADA YA KUONDOKA KWAKE ALIMTOKEA PAUL (SAUL). Mdo 9:4 “ Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Saul, Saul, mbona waniudhi? Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema , Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe” 3) (A) ISSA A.S: ALITABIRI KUJA KWA MUHAMMAD Quran Suratul As Saff , 61:6 “Na (wakumbushe) aliposema (Nabii) Isa bin Maryamu (kuwaambia mayahudi) enyi wana wa Israili! mimi ni mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu. Nisadikishaye yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati. Na kutoa habari njema ya mtume atakayewajia nyuma yangu ambaye jina lake litakuwa Ahmad(Muhammad). Na maana ya majina mawili yote haya ni moja. Maana yake Mwenye kushukuriwa kwa maneno yake mazuri na vitendo vyake vizuri na kila chake kwani vyake vyote ni vizuri).Lakini alipowajia kwa hoja zilizowazi walisema: “ Huu ni udanganyifu uliyo dhahiri”. (B)YESU KRISTO ALIMTUMA ROHO MTAKATIFU KATIKA SIKU YA PENTEKOSTE. Yoh: 14:26 “.Lakini huyo Msaidizi,huyo Roho Mtakatifu,ambaye Baba atampeleka kwa jina langu,atawafundisha yote,na kuwakumbusha yote niliyowaambia”. Katka Kiyunani anaitwa “Paracletos” yaani msaidizi au mfariji Yoh 15:26 “ Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia” Yoh 16:7 “Lakini mimi ninawaambia iliyo kweli; yawafaa nyinyi mimi niondoke,kwa maana mimi nisipoondoka huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu nitampeleka kwenu”. 4) (A) ISSA A.S : JINA LAKE HALINA NGUVU WALA UWEZO WA KUOKOA BALI NI RANGI MBILI Katika Al-Lu’lu’war-Marjani, Juzuu na1, Hadithi na104 uk. 64 “ Hadithi ya Ibn Abbas (r.a) kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema, “Nilimuona Musa (a.s) katika usiku wa Al-Isra, niliopelekwa,naye ni mtu mrefu, mwenye nywele za hudhurungi zimejikunjakunja kama mtu wa Shanua.Na nilimuona Isa (a.s), naye ni mtu wa wastani wa umbo, unaelekea kwenye wekundu na weupe, ana nywele zilizonyooka……” (B) YESU KRISTO: JINA LAKE NI WOKOVU. Mdo 4:9-10,12 “ kama tukiulizwa leo habari ya jambo jema alilofanyiwa yule mtu dhaifu,jinsi alivyoponywa, jueni nyinyi nyote na watu wote wa Israel ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye nyinyi mlimsulubisha, na Mungu alimfufua katika wafu kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu…………………….Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” Baadhi ya aya ndani ya Qur’an zinaeleza kuwa Isa a.s aliwaponya wenye upofu. Ni akina nani hao tutajiwe angalau mmoja? Yesu alimponya kipofu Batromayo. Aya zingine zinasema Isa a.s alifufua wafu. Ni akina nani hao? Yesu alimfufua Lazaro. Jina tulilopewa ni jina moja tu lenye wokovu la Yesu Kristo. Jina la Isa a.s lisilo na wokovu limehusishwaje na jina la Yesu Kristo wa Nazareth lenye wokovu? Mdo 16:31 “ Wakamwambia , Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka wewe pamoja na nyumba yako.” 5) (A) ISSA.A.S : YEYE SIYO MWANA WA MUNGU. Qur’ani Suratul Al An-Am,6:101 “Yeye ndiye Mwumba wa mbingu na ardhi. inamkinikanaje awe na mwana, hali hana mke. Naye ndiye aliye umba kila kitu (sio baadhi yake kavizaa). Naye ni mjuzi wa kila kitu”. Qurani Suratul At-Tawba (Kutubu), 9:30 “Na Mayahudi wanasema “Uzeri ni mwana wa Mwenyezi Mungu” na “Wakristo wanasema “Masihi ni Mwana wa Mwenyezi Mungu” Haya ndiyo wasemayo kwa vinywa vyao (pasi na kuyapima). Wanayaiga maneno ya wale waliokufuru kabla yao, Mwenyezi Mungu awaangamize. Wanageuzwa namna gani hawa! Fundisho la Uwana wa Mungu kama Biblia inavyofundisha, halimo katika mafundisho na itikadi ya dini ya Kiislamu kwa hiyo Isa a.s siyo mwana wa Mungu. (B) YESU KRISTO: YEYE NI MWANA WA MUNGU. Luka 1:30-31,35 “Malaika akamwambia usiogope Mariamu,kwa maana umepata neema kwa Mungu.Tazama utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Malaika akajibu akamwambia,Roho Mtakatifu atakujilia juu yako,na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli;kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu Mwana wa Mungu. Hivyo Isa siyo Mwana Mungu lakini Yesu ni mwana wa Mungu. Kwa hivyo Yesu siyo Isa. 6) (A) ISSA A.S: YEYE SIYO MUNGU ALIYEFANYIKA MWILI. Suratul Al- Maidah,(meza), 5:72-73 Bila ya shaka wamekufuru wale waliosema, “ Mwenyezi Mungu ni Masih (issa)bin Maryam”.(Na hali ya kuwa)Masihi alisema “Enyi wana wa Israel! Mwabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wenu. Kwani anayemshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharimishia Pepo, na mahali pake (patakuwa) ni Motoni. Na madhalimu hawatakuwa na wasaidizi (wa kuwasaidia siku ya Kiama) “Kwa hakika wamekufuru wale waliosema mwenyenzi Mungu ni mmoja katika (wale waungu) watatu (yeye ndiye watatu wao ) hali hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu mmoja ( tu peke yake) na kama hawataacha hayo wasemayo kwa yakini itawakamata wale wanaoendelea na ukafiri miongoni mwao adhabu iumizayo”. (B)YESU YEYE NI NENO LA MUNGU LILILOFANYIKA MWILI: Yoh 1 : 1,14 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu……..Naye Neno alifanyika mwili akakaa kwetu…….” 7) (A) ISSA A.S YEYE HAJAWAHI KUSULUBIWA WALA KUUWAWA Qurani Suratul An-Nisaa (Wanawake) 4:157-158 “Na kwa (ajili ya )kusema kwao sisi tumemuua masihi Isa mwana wa Maryamu, mtume wa Mungu. Hali hawakumuua wala hawakumsulubu bali walibabaishiwa (mtu mwingine wakamdhani nabii Isa.) Na kwa hakika wale waliokhitalifiana katika (hakika)hiyo (ya kumuua nabii Isa) wamo katika shaka nalo (jambo hilo kusema kauwawa]. Wao (kabisa) hawana yakini juu ya (jambo)hili (la kuwa kweli wamemuua nabii isa) isipokuwa wanafuata dhana tu.Na kwa yakini hawakumuua. Bali mwenyenzi Mungu alimnyanyua kwake. Na mwenyenzi Mungu ni mwenye nguvu (na)mwenye hikima. (B)YESU KRISTO: YEYE ALISULUBIWA MSALABANI Yohana 19:18,31,33 “Wakamsulibisha huko,na wengine wawili pamoja,mmoja huku na mmoja huku, na Yesu katikati.Basi Wayahudi, kwa sababu ni Maandalio, miili isikae juu ya misalaba siku ya sabato(maana sabato ile ilikuwa siku kubwa), walimwomba Pilato miguu yao ivunjwe,wakaondolewe. Lakini walipomjia Yesu na kuona ya kuwa amekwisha kufa,hawakumvunja miguu”. 8) (A) ISSA A.S HANA HADHI YA KUABUDIWA NA BINADAMU YEYOTE. Qur’an, Suratul Al-Maidah, 5:116 “ Na (kumbukeni) Mwnyezi Mungu atakaposema: “Ewe Isa bin Maryam! Je ,wewe uliwaambia watu: ‘Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu’?” Aseme (Nabii Isa): “Wewe umetakasika na kuwa na mshirika, hainijuzii mimi kusema ambayo si haki yangu (kuyasema, kwa kuwa ni ya uongo), kama ningalisema bila shaka ungalijua ; unayajua yaliyomo nafsini mwangu, lakini mimi siyajui yaliyomo nafsini mwako; hakika Wewe ndiye ujuaye mambo ya ghaibu. B) YESU ANASTAHILI KUABUDIWA NA WANADAMU NA MALAIKA Math 2: 2 “yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? kwa maana tuliiona nyota yake mashariki nasi tumekuja kumsujudia.” Yoh 9: 35 “ Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; naye alipomwona alisema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu? Naye akajibu akasema, Ni nani, Bwana, nipate kumwamini? Yesu akamwambia Umemwona, naye anayesema nawe ndiye. Akasema, naamini, Bwana, akamsujudia.” Filipi 2:10-11 “ili kwa Jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.” Ebr 1:6 “ Hata tena amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema, Na wamsujudu Malaika wote wa Mungu. 9) (A) ISA HASTAHILI KUWA MWOMBEZI WA WATU KWA MUNGU Sahih Al-Bukhari, vol.6 ,Hadithi no 3, The Noble Qur’an, English Translation uk. 8 “…….Nenda kwa Musa, mtumishi wa Allah ambaye Allah alizungumza naye uso kwa uso na alimpa Torati. Hivyo watakwenda kwake naye atasema ‘ Mimi sistahili kwa jukumu hilo la uombezi, na atataja mauaji aliyoyafanya kwa mtu ambaye si muuaji, na hivyo atajisikia aibu mbele ya Mola wake, naye atasema nendeni kwa Isa, mtumishi wa Allah, Mjumbe wake neno lake na roho iliyotoka kwake. Isa atasema sistahili mimi kubeba jukumu la uombezi…….” B) YESU ANASTAHILI KUWA MWOMBEZI WA WANADAMU KWA MUNGU 1 Tim 2:5 “ Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu;” Ebr 7:24-25 “ bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka.Naye, kwa sababu hii , aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu Hai siku zote ili awaombee. 10) (a) ISA NI NABII MWINGINE TU ASIYE TOFAUTI NA WENGINE Qur’an Suratul Baqarah, (ng’ombe)2:136 “ “Semeni nyinyi (Waislamu waambiwe Mayahudi na Manasara; waambieni): “Tumemwamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyoteremshiwa, na yale yaliyoteremshwa kwa Ibrahimu na Ismail na Is-haqa na Yaaqubu na kizazi (chake Yaaqubu); na waliyopewa Musa na Isa na pia yale waliyopewa Manabii (wengine) kutoka kwa Mola wao; hatutofautishi baina ya yoyote katika hao. (Wote tunawaamini); na sisi tumenyenyekea Kwake.” b) YESU YEYE YU JUU KULIKO VITU VYOTE Efeso 1:20-23 “ aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; juu sana kuliko ufalme wote, na malaika, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; akavitia vitu vyote chini ya miguu yake akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya Kanisa; ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.” 11) (a) ISA ATAKAPORUDI, ATAOA NA KUZAA WATOTO Mishkat Al- Masabih, vol 2 uk.1159, Sahih Muslim, vol. 1 uk 92 “ Isa atakaporudi ataishi miaka arobaini (40), muda ambao atakuwa ameoa na kuzaa watoto, na atafanya ibada ya hija.” b) YESU ATAKAPORUDI ATAKUJA KULINYAKUA KANISA, YAANI BIBI ARUSI Efeso 5:25-26, 32-33 “ Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, Uf 19:7 “ Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana Kondoo imekuja na mkewe amejiweka tayari.akajitoa kwa ajili yake, ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;…..Siri hiyo ni kubwa ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa. Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mmewe.” 12)(a) ISA ATAKUFA BAADA YA KUISHI MIAKA AROBAINI (40) Mishkat Al- Masabih, vol 2 uk. 1159,Sunan Abu Dawud, Hadithi 4310, Sahih Muslim, vol.1, uk.92 , “Isa atakaporudi ataondosha dini zote zisiwepo isipokuwa Uislamu. Atamharibu Masih Dajjal, na ataishi duniani miaka arobaini (40) na kisha atakufa. Na baada ya kufa atazikwa pembeni mwa kaburi la Muhammad.” B) YESU BAADA YA KUFUFUKA YU HAI SIKU ZOTE HAFI TENA Rum 6:9 “ tukijua ya kuwa Kristo akiisha kufufuka katika wafu hafi tena, wala mauti haimtawali tena.” Ebr 7:24-25 “ bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka.Naye, kwa sababu hii , aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu Hai siku zote ili awaombee.” Uf 1:17-18 “ Nami nilipomwona nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, mimi ni wa kwanza na wa mwisho, aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama , ni hai hata milele na milele nami ninazo funguo za mauti na za kuzimu.” 13)(a) ISA ALIPOZALIWA SAUTI YA FARAJA ILITOKA CHINI YA ARDHI Qur’an Suratul Maryam,19:23-24 “ Kisha uchungu ukampeleka katika shina la mtende, (akawa anazaa na huku) anasema: “ Laiti ningekufa kabla ya haya, na ningekuwa niliyesahaulika kabisa.” Mara ikamfikia sauti kutoka chini yake (inamwambia): usihuzunike. Hakika Mola wako amejaalia (ameweka) kijito cha maji chini yako;” Mafundisho ya Kiislamu yanaeleza kuwa huko chini ya ardhi kuna mnyama. Na huyo mnyama anazijua aya za Qur’an. Qur’an katika Suratul Al-Naml, 27:82 “Na kauli (ya kuja kiyama) itakapowathibitikia Tutawatolea mnyama katika ardhi atakayewasemeza kwa sababu watu walikuwa hawaziyakinishi Aya Zetu” b) ALIPOZALIWA YESU SAUTI ZA MALAIKA ZILITOKA JUU Luka 2:13-16 “ Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu na kusema, Atukuzwe Mungu juu mbinguni na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia. Ikawa malaika hao walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji waliambiana, Haya na twendeni mpaka Bethlehemu, tukalione hilo lililofanyika alilotujulisha Bwana. Wakaenda kwa haraka wakamkuta Mariamu na Yusufu, na yule mtoto mchanga amelala horini” (14)(a) ISA HANA UFAHAMU WA MAMBO MBALIMBALI katika Al-Lu’lu’ war- Marjan,kitabu cha 3 Hadithi na 1528 uk.883 “Hadithi ya Abu Huraira (r.a) kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema “Issa Ibn Mariam (a,s) alimwona mtu anaiba akamuuliza umeiba? akasema hapana ,Naapa kwa Allah ambaye hakuna mola isipokuwa yeye .Issa (a.s) akasema nimemuamini Allah na limeniongopea jicho langu”. b) YESU ANAYAJUA YOTE Yohana 1:47-48 “ Basi Yesu akamwona Nathanael anakuja kwake, akanena habari zake “Tazama Mwizraeli kweli kweli hamna hila ndani yake. Nathaeli akamwambia umepataje kunitambua? Yesu akajibu akamwambia, Kabla Filipo hajakuita ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona” Yoh 2:24-25 “ Lakini Yesu hakujiaminisha kwao; kwa kuwa yeye aliwajua wote; na kwa sababu hakuwa na haja ya mtu kushuhudia habari za mwanadamu; kwa maana yeye mwenyewe aliyajua yaliyomo ndani ya mwanadamu” 15) (a) ISA A.S MAMA YAKE ALIKUTWA PEMBEZONI MWA MSIKITI ALIPOLETEWA HABARI ZA KUZALIWA KWAKE. Qur’an Suratul Maryam,19:16-17 “ Na mtaje Mariamu kitabuni humu. Alipojitenga na jamaa zake, (akenda) mahali upande wa mashariki (wa msikiti) na akaweka pazia kujikinga nao. Tukampelekea muhuisha Sharia Yetu (Jibrili)- akajimithilisha kwake (kwa sura ya) binadamu aliye kamili b) YESU KRISTO, MAMA YAKE ALIKUTWA NYUMBANI KWAO NAZARETI Luka 1:26-28 “Mwezi wa sita malaika Gabriel alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti. Kwa mwana mwali Bikira aliyekuwa ameposwa na mtu jina lake Yusufu wa mbari ya Daudi. Na jina lake Bikira huyo ni Mariamu. Akaingia nyumbani kwake akasema, salamu uliyepewa neema Bwana yu pamoja nawe.” 16)(a) MIMBA YA ISA ILIKUWA NI YA SIKU MOJA Qur’an Suratul Maryam,19:21-22 “ (Malaika) akasema: “ Nikama hivyo (unavyosema; lakini) Mola wako amesema ‘Haya ni sahali Kwangu, na ili Tumfanye muujiza kwa wanaasamu na rehema itokayo Kwetu (ndiyo Tumefanya hivi);’ Na hili ni jambo lililokwisha kuhukumiwa.” Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali” b) MIMBA YA YESU SIKU ZILITIMIA. Luka 2:6-7 “ ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia, akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni” NB: Mwezi wa sita uliotajwa katika Luka 1:26 ni mwezi wenye kuelezea umri wa mimba ya Yohana ndani ya tumbo la Elizabethi. Luka 1: 36 “ Tena tazama jamaa yako Elizabeti naye amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa” NB: Hori iliyotajwa hapa,ina maana ya chombo cha kulishia wanyama kinachokuwa ndani ya zizi. Kwa Kiyunani (Kigiriki) ambayo ndiyo lugha iliyotumika kuandikia Agano Jipya ,chombo hicho kinaitwa “Fatne” kwa Kiingereza kinaitwa “a manger” 17)ISA (A.S) ATAKAPORUDI ATAKUJA KUVUNJA MISALABA NA KUUA NGURUWE Mkweli Mwaminifu, Juzuu 3-4, uk.20, Hadithi na. 753 “ Haisimami saa ya (kiyama) mpaka akuteremkieni nabii Isa (a.s) mwana wa Maryamu atahukumu (kwa sheria ya Kiislamu) (na) muadilifu, basi atavunja misalaba (ya Wakristo Makanisani) na ataua nguruwe, na ataondosha fedheha au (aibu), na mali itazidi kuwa nyingi sana mpaka hataikubali (ataikataa) mtu (kwa kuogopa kiyama)” .Soma pia katika Sahihi Bukhar, vol. 3, Hadithi na 425,. Al-Lu’lu’war-Marjan, juzuu ya 1,Hadithi na 95 uk.51. The Noble Qur’an uk.757 b)YESU KRISTO ATAKAPORUDI ATAWATUMA MALAIKA ZAKE KUWAKUSANYA WATAKATIFU Luka 24:30-31 “ ndipo itakapoonekana ishara ya mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi, naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.” ONYO LA YESU KRISTO WA NAZARETH Math 24:24 “ kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini hata walio wateule.” (Angalia pia Marko 13:22) Yoh 8:24 “ Kwa hiyo naliwambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye mtakufa katika dhambi zenu.” WEWE MTEULE JE UTADANGANYWA NA KUDANGANYIKA KUWA KWELI ISA A.S NDIYE YESU KRISTO? UKIAMINI HIVYO UTAKUWA UMEDANGANYIKA NA UTAKOSA WOKOVU WA MWENYEZI MUNGU!!!!!!!!!! YESU KRISTO, YEYE NI IMMANUEL, MSHAURI WA AJABU, MUNGU MWENYE NGUVU, BABA WA MILELE, MFALME WA AMANI!!!! (ISAYA 9:6, MATH 1:23) HIZI SIYO SIFA ZA Shkhê Êdén Hãzãrd kwa Max Shimba Ministries
    0 Kommentare 0 Geteilt 13KB Ansichten 0 Bewertungen
  • QURAN YAMKIRI YESU KUWA NI MUNGU WA KWELI

    Mwandishi Abel Suleiman Shiriwa


    Katika vitu ambavyo waislamu huwasumbua vichwa na akili zao, ni kuhusu Uungu wa Yesu, sema vitu vyote lakini ukifika hapo kwenye Uungu wa Bwana Yesu basi mnapotezana, na kitu ambacho kinawafanya waislamu washindwe kukubali kuwa yeye ni Mungu, ni ukosefu wao wa ROHO MTAKATIFU, maana mtu hawezi kukiri kuwa Yesu ni Bwana (Mungu) kama hana ROHO MTAKATIFU, kama yasemavyo maandiko.
    2 Korintho 12: 3 Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika Roho wa Mungu, kusema, Yesu amelaaniwa; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu.


    Kwa hivyo Ndugu yangu Mkristo unapojadiliana na Muislamu kuhusu Habari za Uungu wa Yesu, kamwe hawezi kukubali mpaka ROHO MTAKATIFU auhusike, kinyume na hapao itakuwa ni sawa na kumpigia mbuzi Gitaa, kwa hivyo hoja zake zote zitaegemea katika hali ya Kuutazama mwili kama ambavyo Elisabeti, alimtazama Yesu kama mtu wa kawaida sana ambaye atazaliwa na Mariam, lakini mara baada ya kujazwa na Roho Matakatifu, ndipo alipokiri kuwa Yesu ni Bwana yaani Mungu wake.


    Luka 1: 39 Basi, Mariamu akaondoka siku hizo, akaenda hata nchi ya milimani kwa haraka mpaka mji mmoja wa Yuda,

    40 akaingia nyumbani kwa Zakaria akamwamkia Elisabeti.
    41 Ikawa Elisabeti aliposikia kule kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake; Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu;
    42 akapaza sauti kwa nguvu akasema, Umebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
    43 Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi?


    Hapo tumeona ni namna gani Umuhimu wa ROHO MATAKATIFU, katika kumjua Yesu kuwa ni Mungu, kwa kuwa Waislamu hawana Roho Mtakatifu, kazi yao hasa ni kumtaza Yesu alipoutwaa Mwili wa Kibinadamu, na kuwa na asili ya mtu, na kuuficha Uungu wake katika mwili, ndo maana akawa akiijita Mtume, Mwana, Kuhani, na hata Nabii, sasa leo sina lengo hasa la kuueleza Uungu hasa wa Yesu, kiundani kwa Biblia, bali nataka niitazame Quran namna ambavyo imemkiri Yesu kuwa ni Mungu, kwa kueleza Sifa za Mungu, ambazo Yesu anazo, kwa hivyo nitaeleza SIFA 5 NDANI YA QURAN ambazo zinakiri UUngu wa Yesu.


    (1) Mungu ni mwenye kujua yaliyomo katika nyoyo za watu.
    رَّبُّكُمْ أَعْلَمُ بِمَا فِي نُفُوسِكُمْ إِن تَكُونُواْ صَالِحِينَ فَإِنَّهُ كَانَ لِلأَوَّابِينَ غَفُورًا
    Quran 17:25. Mola wenu anajua sana yaliyomo nyoyoni mwenu, kama mkiwa wema, basi hakika yeye ndiye Mwenye kusamehe wenye kurejea.




    Hapo Quan inatupa habari kuwa MOla au Mungu yeye ni mwenye kujua yaliyomo katika nyoyo za wanadamu, sifa hiyo inamwendea Yesu kwani ni mwenye kujua yaliyomo ndani ya mioyo ya wanadamu.
    Yohana 2: 24 Lakini Yesu hakujiaminisha kwao; kwa kuwa yeye aliwajua wote;
    25 na kwa sababu hakuwa na haja ya mtu kushuhudia habari za mwanadamu; kwa maana yeye mwenyewe alijua yaliyomo ndani ya mwanadamu.
    Kama Waislamu wangelikuwa na Roho Matakatifu, kwa ushahidi huu basi wasingeweza kupinga kuhusu UUngu wa Yesu.


    (2) MUNGU NI NI MWENYE KUONGEZA IDADI YA UWEPO WA WATATU
    Namaanisha kuwa pakiwa na watu wawili au watatu basi Mungu anaongezeka na kuwa wanne, kwa watu watatu, au watano kwa watu wanne, kama isimemavyo Quran
    أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ مَا يَكُونُ مِن نَّجْوَى ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ وَلَا خَمْسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمْ وَلَا أَدْنَى مِن ذَلِكَ وَلَا أَكْثَرَ إِلَّا هُوَ مَعَهُمْ أَيْنَ مَا كَانُوا ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّ اللَّهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ
    Quran 57:7. Je, huoni kwamba Mwenyeezi Mungu anajua viliyomo mbinguni na viliyomo ardhini? Hawashauriani kwa siri watatu ila yeye ni wa nne wao, wala watano ila yeye ni wa sita wao, wala wachache kuliko hao wala zaidi ila yeye huwa pamoja nao popote walipo. Kisha siku ya Kiyama atawaambia waliyoyatenda hakika Mwenyeezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.


    Hapo tunapewa sifa za Mungu, kwa uzuri kabisa, pakiwa na wawili Mungu wa tatu, wakiwa watatu, Mungu wanne, wakiwa wanne, Mungu wa watano, SIFA hizo zinamwendea Yesu Kristo mwenyewe kama alivyosema.


    Mathayo 18: 20 Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.


    Hapa Yesu anatuambia sifa hiyo ya kuwa pamoja na watu wawili au watatu, sifa hiyo ni yake yeye mwenyewe Yesu…. Tatizo la kutokuwa na Roho Mtakatifu kwa waislamu ndiyo maana wanashindwa kutambua kuwa Yesu ni Mungu.


    (3) Mungu yeye ni Nuru ya Mbingu na Nchi.
    اللَّهُ نُورُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ مَثَلُ نُورِهِ كَمِشْكَاةٍ فِيهَا مِصْبَاحٌ الْمِصْبَاحُ فِي زُجَاجَةٍ الزُّجَاجَةُ كَأَنَّهَا كَوْكَبٌ دُرِّيٌّ يُوقَدُ مِن شَجَرَةٍ مُّبَارَكَةٍ زَيْتُونِةٍ لَّا شَرْقِيَّةٍ وَلَا غَرْبِيَّةٍ يَكَادُ زَيْتُهَا يُضِيءُ وَلَوْ لَمْ تَمْسَسْهُ نَارٌ نُّورٌ عَلَى نُورٍ يَهْدِي اللَّهُ لِنُورِهِ مَن يَشَاء وَيَضْرِبُ اللَّهُ الْأَمْثَالَ لِلنَّاسِ وَاللَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ
    Quran 24: 35. Mwenyeezi Mungu ni nuru ya mbingu na ardhi, mfano wa nuru yake ni kama shubaka ndani yake mna taa. Taa ile imo katika tungi, tungi lile ni kama nyota ing'aayo inayowashwa katika mti uliobarikiwa wa mzaituni, si wa mashariki wala magharibi yanakaribia mafuta yake kung'aa ingawa moto haujayagusa, nuru juu ya nuru, Mwenyeezi Mungu humuongoza kwenye nuru yake amtakaye, na Mwenyeezi Mungu hupiga mifano kwa watu, na Mwenyeezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.


    QURAN IMESEMA MUNGU, NI NURU YA MBINGU NA NCHI, SIFA HIYO NI YA YESU, MAANA YESU NI NURU YA ULIMWENGU.
    Yohana 8: 12 Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.


    TENA YESU NI NURU YA MBINGU.
    Matendo 26: 13 Ee Mfalme, ndipo wakati wa adhuhuri njiani naliona nuru inatoka mbinguni ipitayo mwangaza wa jua, ikinimulikia mimi, na wale waliofuatana nami pande zote.
    14 Tukaanguka nchi sote, nikasikia sauti ikisema nami kwa lugha ya kiebrania, Sauli! Sauli! Mbona waniudhi? Ni vigumu kwako kuupiga mateke mchokoo.
    15 Nami nikasema, Wewe u nani, Bwana? Bwana akaniambia, Mimi ni Yesu, ambaye wewe unaniudhi.
    Sifa zote hizo za kuwa Nuru ya Mbingu na aridhi, Yesu, anazo, kwa nini Waislamu wanashindwa kutambua kuwa Yesu ni Mungu? Ni kwa sababu, hawana ROHO MTAKATIFU.


    (4) MWENYEZI MUNGU YEYE NI MWANZO NA WA MWISHO.
    Quran inatupa habari kuwa Mwenyezi Mungu sifa yake yeye ni wa kwanza na pia ni wa Mwisho.
    Quran 57: هُوَ الْأَوَّلُ وَالْآخِرُ وَالظَّاهِرُ وَالْبَاطِنُ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ
    3. Yeye ndiye wa Mwanzo na wa Mwisho, naye ni wa dhahiri, na wa siri, naye ni Mjuzi wa kila


    Hapa Quran inasema yeye, Allah hasemi, mimi ni wa kwanza na mwisho, bali yeye, kuonesha kuwa siyo muhusika wa sifa, sasa Yesu yeye ambaye ndiye Muhusika wa sifa hizo, anasema


    Ufunuo 1: 16 Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking'aa kwa nguvu zake.
    17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,


    Yesu anasema Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, Allah yeye anasema yeye, yeye hii inamwendea Yesu, kwa kuwa ameshatangulia kusema hata kabla ya kuja Quran, kinachowafunga ni Ukosefu wa ROHO MTAKATIFU kwa waislamu.


    (5) MWENYEZI MUNGU YUKO MBINGUNI.
    Quran inaeleza kuwa Mungu yupo mbinguni,
    Quran 67: أَمْ أَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاء أَن يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا فَسَتَعْلَمُونَ كَيْفَ نَذِيرِ
    17. Au je, mnadhani mko salama kwa (Mwenyezi Mungu) alioko mbinguni kuwa yeye hatakuleteeni kimbunga chenye changarawe? basi karibuni mtajua lilivyo onyo langu
    Quran inatambua uwepo wa Mungu kuwepo mbinguni, kwani Allah yeye makao yake ni hapa Duniani, huko Makka ambako waislamu, huenda kuhiji huko, na pia kila swala huelekea kwake, Allah Makka kama alivyoema katika quran 7:29. Kwa hivyo Allah hawezi kuwa mbinguni kwa sababu yeye yupo Duniani, Sifa hiyo ipo kwa Yesu.


    Matendo 1:9 Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao.
    10 Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe,
    11 wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni?


    Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.


    Pengine Waislamu wanaweza kujiuliza Ni vipi Yesu achukuliwe kwenda Mbinguni? Alichukuliwa na nani? Ni wingu ndilo ambalo lilimchukua, kwani Wingu ni gari la Mungu.


    Zaburi 104: 3 Na kuziweka nguzo za orofa zake majini. Huyafanya mawingu kuwa gari lake, Na kwenda juu ya mabawa ya upepo,


    KWA HIVYO NIMEWEKA HIVYO VIPENGELE VICHACHE ILI ANGALAU NIWEZE KUWATOA WAISLAMU GIZANI KUHUSU UUNGU wa Yesu, japo kuwa siyo rahisi wao kukubali kuwa Yesu ni Mungu, hata kama maandiko wanayaona dhahiri, ila kwa sababu hawana ROHO MTAKATIFU, wataendelea kupinga kuwa siyo Mungu, wakati Quran imekubali, na isitoshe mungu wa dunia hii (shetani) amezifunga fahamu na akili zao kwa kumkosa ROHO MTAKATIFU, isiwazunukie Nuru ya Injili ya Kristo aliye Sura yake Mungu.
    2 Korintho 4: 3 Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea;
    4 ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.


    Waislamu Mtafuteni ROHO MTAKATIFU, ili muweze kumjua Yesu na UUngu wake…. Muislamu tambua kuwa Quran imetumika tu kama kibao kukuonesha njia, yaani inakuelekeza pa kumpaa Mungu, ukifika sehemu ukakuta kibao kimekuelekeza kwa mshare, Muhumbili ni kule, wewe usikae kwenye hicho Kibao, hapo siyo Muhimbili, fuata Ramani ya Hicho kibao, utafika Muhimbili, Quran ni kibao, kinakuelekeza kwenye Biblia, huko ndo unampata Mungu wa kweli Yesu.
    QURAN YAMKIRI YESU KUWA NI MUNGU WA KWELI Mwandishi Abel Suleiman Shiriwa Katika vitu ambavyo waislamu huwasumbua vichwa na akili zao, ni kuhusu Uungu wa Yesu, sema vitu vyote lakini ukifika hapo kwenye Uungu wa Bwana Yesu basi mnapotezana, na kitu ambacho kinawafanya waislamu washindwe kukubali kuwa yeye ni Mungu, ni ukosefu wao wa ROHO MTAKATIFU, maana mtu hawezi kukiri kuwa Yesu ni Bwana (Mungu) kama hana ROHO MTAKATIFU, kama yasemavyo maandiko. 2 Korintho 12: 3 Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika Roho wa Mungu, kusema, Yesu amelaaniwa; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu. Kwa hivyo Ndugu yangu Mkristo unapojadiliana na Muislamu kuhusu Habari za Uungu wa Yesu, kamwe hawezi kukubali mpaka ROHO MTAKATIFU auhusike, kinyume na hapao itakuwa ni sawa na kumpigia mbuzi Gitaa, kwa hivyo hoja zake zote zitaegemea katika hali ya Kuutazama mwili kama ambavyo Elisabeti, alimtazama Yesu kama mtu wa kawaida sana ambaye atazaliwa na Mariam, lakini mara baada ya kujazwa na Roho Matakatifu, ndipo alipokiri kuwa Yesu ni Bwana yaani Mungu wake. Luka 1: 39 Basi, Mariamu akaondoka siku hizo, akaenda hata nchi ya milimani kwa haraka mpaka mji mmoja wa Yuda, 40 akaingia nyumbani kwa Zakaria akamwamkia Elisabeti. 41 Ikawa Elisabeti aliposikia kule kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake; Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu; 42 akapaza sauti kwa nguvu akasema, Umebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa. 43 Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi? Hapo tumeona ni namna gani Umuhimu wa ROHO MATAKATIFU, katika kumjua Yesu kuwa ni Mungu, kwa kuwa Waislamu hawana Roho Mtakatifu, kazi yao hasa ni kumtaza Yesu alipoutwaa Mwili wa Kibinadamu, na kuwa na asili ya mtu, na kuuficha Uungu wake katika mwili, ndo maana akawa akiijita Mtume, Mwana, Kuhani, na hata Nabii, sasa leo sina lengo hasa la kuueleza Uungu hasa wa Yesu, kiundani kwa Biblia, bali nataka niitazame Quran namna ambavyo imemkiri Yesu kuwa ni Mungu, kwa kueleza Sifa za Mungu, ambazo Yesu anazo, kwa hivyo nitaeleza SIFA 5 NDANI YA QURAN ambazo zinakiri UUngu wa Yesu. (1) Mungu ni mwenye kujua yaliyomo katika nyoyo za watu. رَّبُّكُمْ أَعْلَمُ بِمَا فِي نُفُوسِكُمْ إِن تَكُونُواْ صَالِحِينَ فَإِنَّهُ كَانَ لِلأَوَّابِينَ غَفُورًا Quran 17:25. Mola wenu anajua sana yaliyomo nyoyoni mwenu, kama mkiwa wema, basi hakika yeye ndiye Mwenye kusamehe wenye kurejea. Hapo Quan inatupa habari kuwa MOla au Mungu yeye ni mwenye kujua yaliyomo katika nyoyo za wanadamu, sifa hiyo inamwendea Yesu kwani ni mwenye kujua yaliyomo ndani ya mioyo ya wanadamu. Yohana 2: 24 Lakini Yesu hakujiaminisha kwao; kwa kuwa yeye aliwajua wote; 25 na kwa sababu hakuwa na haja ya mtu kushuhudia habari za mwanadamu; kwa maana yeye mwenyewe alijua yaliyomo ndani ya mwanadamu. Kama Waislamu wangelikuwa na Roho Matakatifu, kwa ushahidi huu basi wasingeweza kupinga kuhusu UUngu wa Yesu. (2) MUNGU NI NI MWENYE KUONGEZA IDADI YA UWEPO WA WATATU Namaanisha kuwa pakiwa na watu wawili au watatu basi Mungu anaongezeka na kuwa wanne, kwa watu watatu, au watano kwa watu wanne, kama isimemavyo Quran أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ مَا يَكُونُ مِن نَّجْوَى ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ وَلَا خَمْسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمْ وَلَا أَدْنَى مِن ذَلِكَ وَلَا أَكْثَرَ إِلَّا هُوَ مَعَهُمْ أَيْنَ مَا كَانُوا ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّ اللَّهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ Quran 57:7. Je, huoni kwamba Mwenyeezi Mungu anajua viliyomo mbinguni na viliyomo ardhini? Hawashauriani kwa siri watatu ila yeye ni wa nne wao, wala watano ila yeye ni wa sita wao, wala wachache kuliko hao wala zaidi ila yeye huwa pamoja nao popote walipo. Kisha siku ya Kiyama atawaambia waliyoyatenda hakika Mwenyeezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu. Hapo tunapewa sifa za Mungu, kwa uzuri kabisa, pakiwa na wawili Mungu wa tatu, wakiwa watatu, Mungu wanne, wakiwa wanne, Mungu wa watano, SIFA hizo zinamwendea Yesu Kristo mwenyewe kama alivyosema. Mathayo 18: 20 Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao. Hapa Yesu anatuambia sifa hiyo ya kuwa pamoja na watu wawili au watatu, sifa hiyo ni yake yeye mwenyewe Yesu…. Tatizo la kutokuwa na Roho Mtakatifu kwa waislamu ndiyo maana wanashindwa kutambua kuwa Yesu ni Mungu. (3) Mungu yeye ni Nuru ya Mbingu na Nchi. اللَّهُ نُورُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ مَثَلُ نُورِهِ كَمِشْكَاةٍ فِيهَا مِصْبَاحٌ الْمِصْبَاحُ فِي زُجَاجَةٍ الزُّجَاجَةُ كَأَنَّهَا كَوْكَبٌ دُرِّيٌّ يُوقَدُ مِن شَجَرَةٍ مُّبَارَكَةٍ زَيْتُونِةٍ لَّا شَرْقِيَّةٍ وَلَا غَرْبِيَّةٍ يَكَادُ زَيْتُهَا يُضِيءُ وَلَوْ لَمْ تَمْسَسْهُ نَارٌ نُّورٌ عَلَى نُورٍ يَهْدِي اللَّهُ لِنُورِهِ مَن يَشَاء وَيَضْرِبُ اللَّهُ الْأَمْثَالَ لِلنَّاسِ وَاللَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ Quran 24: 35. Mwenyeezi Mungu ni nuru ya mbingu na ardhi, mfano wa nuru yake ni kama shubaka ndani yake mna taa. Taa ile imo katika tungi, tungi lile ni kama nyota ing'aayo inayowashwa katika mti uliobarikiwa wa mzaituni, si wa mashariki wala magharibi yanakaribia mafuta yake kung'aa ingawa moto haujayagusa, nuru juu ya nuru, Mwenyeezi Mungu humuongoza kwenye nuru yake amtakaye, na Mwenyeezi Mungu hupiga mifano kwa watu, na Mwenyeezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu. QURAN IMESEMA MUNGU, NI NURU YA MBINGU NA NCHI, SIFA HIYO NI YA YESU, MAANA YESU NI NURU YA ULIMWENGU. Yohana 8: 12 Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima. TENA YESU NI NURU YA MBINGU. Matendo 26: 13 Ee Mfalme, ndipo wakati wa adhuhuri njiani naliona nuru inatoka mbinguni ipitayo mwangaza wa jua, ikinimulikia mimi, na wale waliofuatana nami pande zote. 14 Tukaanguka nchi sote, nikasikia sauti ikisema nami kwa lugha ya kiebrania, Sauli! Sauli! Mbona waniudhi? Ni vigumu kwako kuupiga mateke mchokoo. 15 Nami nikasema, Wewe u nani, Bwana? Bwana akaniambia, Mimi ni Yesu, ambaye wewe unaniudhi. Sifa zote hizo za kuwa Nuru ya Mbingu na aridhi, Yesu, anazo, kwa nini Waislamu wanashindwa kutambua kuwa Yesu ni Mungu? Ni kwa sababu, hawana ROHO MTAKATIFU. (4) MWENYEZI MUNGU YEYE NI MWANZO NA WA MWISHO. Quran inatupa habari kuwa Mwenyezi Mungu sifa yake yeye ni wa kwanza na pia ni wa Mwisho. Quran 57: هُوَ الْأَوَّلُ وَالْآخِرُ وَالظَّاهِرُ وَالْبَاطِنُ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ 3. Yeye ndiye wa Mwanzo na wa Mwisho, naye ni wa dhahiri, na wa siri, naye ni Mjuzi wa kila Hapa Quran inasema yeye, Allah hasemi, mimi ni wa kwanza na mwisho, bali yeye, kuonesha kuwa siyo muhusika wa sifa, sasa Yesu yeye ambaye ndiye Muhusika wa sifa hizo, anasema Ufunuo 1: 16 Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking'aa kwa nguvu zake. 17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, Yesu anasema Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, Allah yeye anasema yeye, yeye hii inamwendea Yesu, kwa kuwa ameshatangulia kusema hata kabla ya kuja Quran, kinachowafunga ni Ukosefu wa ROHO MTAKATIFU kwa waislamu. (5) MWENYEZI MUNGU YUKO MBINGUNI. Quran inaeleza kuwa Mungu yupo mbinguni, Quran 67: أَمْ أَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاء أَن يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا فَسَتَعْلَمُونَ كَيْفَ نَذِيرِ 17. Au je, mnadhani mko salama kwa (Mwenyezi Mungu) alioko mbinguni kuwa yeye hatakuleteeni kimbunga chenye changarawe? basi karibuni mtajua lilivyo onyo langu Quran inatambua uwepo wa Mungu kuwepo mbinguni, kwani Allah yeye makao yake ni hapa Duniani, huko Makka ambako waislamu, huenda kuhiji huko, na pia kila swala huelekea kwake, Allah Makka kama alivyoema katika quran 7:29. Kwa hivyo Allah hawezi kuwa mbinguni kwa sababu yeye yupo Duniani, Sifa hiyo ipo kwa Yesu. Matendo 1:9 Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao. 10 Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe, 11 wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni. Pengine Waislamu wanaweza kujiuliza Ni vipi Yesu achukuliwe kwenda Mbinguni? Alichukuliwa na nani? Ni wingu ndilo ambalo lilimchukua, kwani Wingu ni gari la Mungu. Zaburi 104: 3 Na kuziweka nguzo za orofa zake majini. Huyafanya mawingu kuwa gari lake, Na kwenda juu ya mabawa ya upepo, KWA HIVYO NIMEWEKA HIVYO VIPENGELE VICHACHE ILI ANGALAU NIWEZE KUWATOA WAISLAMU GIZANI KUHUSU UUNGU wa Yesu, japo kuwa siyo rahisi wao kukubali kuwa Yesu ni Mungu, hata kama maandiko wanayaona dhahiri, ila kwa sababu hawana ROHO MTAKATIFU, wataendelea kupinga kuwa siyo Mungu, wakati Quran imekubali, na isitoshe mungu wa dunia hii (shetani) amezifunga fahamu na akili zao kwa kumkosa ROHO MTAKATIFU, isiwazunukie Nuru ya Injili ya Kristo aliye Sura yake Mungu. 2 Korintho 4: 3 Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; 4 ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu. Waislamu Mtafuteni ROHO MTAKATIFU, ili muweze kumjua Yesu na UUngu wake…. Muislamu tambua kuwa Quran imetumika tu kama kibao kukuonesha njia, yaani inakuelekeza pa kumpaa Mungu, ukifika sehemu ukakuta kibao kimekuelekeza kwa mshare, Muhumbili ni kule, wewe usikae kwenye hicho Kibao, hapo siyo Muhimbili, fuata Ramani ya Hicho kibao, utafika Muhimbili, Quran ni kibao, kinakuelekeza kwenye Biblia, huko ndo unampata Mungu wa kweli Yesu.
    0 Kommentare 0 Geteilt 5KB Ansichten 0 Bewertungen
  • TOFAUTI KUMI NA SABA (17) KATI YA YESU WA WAKRISTO NA ISA WA WAISLAM.

    Mara kwa mara, unaweza kuwasikia Waislamu wakisema kuwa Isa a.s. kama anavyotajwa ndani ya Qur’an tukufu, ndiye Yesu Kristo wa Nazareti, kama anavyotajwa ndani ya Biblia Takatifu. Wanafanya hivyo kwa kulinganisha baadhi ya aya zilizomo ndani ya Biblia Takatifu, na zile zilizomo ndani ya Qur’an. Kwa mfano, wanasema kwa mujibu wa Biblia mama yake Yesu Kristo anaitwa Mariamu. Wanasoma katika Injili ya Marko 6:3-4“Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose na Yuda na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake” . 

    Wanafananisha aya hiyo na ile iliyomo ndani ya Qur’an katika Suratul Al-Maidah, 5:75 “ Masih bin Maryam si chochote ila ni mtume tu……”,

    Hoja nyingine wanayoitumia ni kusema kwamba eti jina Isa ni katika lugha ya Kiarabu. Jambo hilo siyo kweli. Kwa sababu katika lugha ya Kiarabu, Yesu anaitwa Yasu’a siyo Isa. Na ikumbukwe kuwa Biblia ndicho kitabu kilichotangulia kuwepo duniani miaka ipatayo 1500 kabla ya Qur’an.(Qur’an is a post Bible book).

    Hoja yetu kwa Waislamu ni hii nani aliyebadilisha jina Yasu’a kuwa Isa?. Jina Yasu’a linashabihiana zaidi na Jina Yehoshua ambalo hilo ni katika lugha ya Kiebrania, na katika Kiyunani lugha iliyotumika kuandika Agano Jipya anaitwa Iesous (tamka Yesu) tafsiri ya maneno hayo kwa lugha ya Kiswahili ni Mwokozi.

    Tunasoma hayo katika Math 1:21-23 “ Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana yeye ndiye atakaye waokoa watu wake na dhambi zao. Hayo yote yamekuwa ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa Nabii akisema Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.”

    Hoja yetu Je Isa a.s naye ni Mwokozi na Imanueli kama alivyo Yesu Kristo?.

    Jambo jingine tunalopaswa kulizingatia tunapoangalia tofauti zao ni kuhusu mama zao. Mama yake Yesu Kristo ni Mariam anayetoka katika ukoo wa Yuda. Tunasoma hayo katika kitabu cha Mwanzo 49:10 “ Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake,Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki,Ambaye mataifa watamtii”.

    Unabii huu umetimia kwa Yesu Kristo.Tunasoma hayo katika Waebrania 7:14 “Maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambayo Musa hakunena neno lolote juu yake katika mambo ya ukuhani”

    Lakini tusomapo habari za Isa, yeye mama yake anatoka ukoo wa Imrani. Ambaye ni baba yao Haruni, Miriamu na Musa. Tunayasoma hayo katika Suratul Al-Maryam 19:28 “Ewe dada yake Haruni. Baba yako hakuwa mtu mbaya. Wala mama yako hakuwa hasharati”.

    fafanuzi unaoifafanua aya hii ya 19:28 uliyomo ndani ya Qur’an, tafsiri ya King Fahd uk. 405, unasomeka hivi “ This Harun (Aaron) is not the brother of Musa (Moses), but he was another pious man at the time of Maryam (Mary)”

    Tafsiri “Huyu Harun siyo ndugu yake Musa, bali alikuwa ni mtu mwingine tu mcha Mungu, aliyeishi wakati wa kipindi cha Maryam”
    Kwa mujibu wa Biblia, Haruni ni mtoto wa mzee Amran na mama yao anaitwa Yekobedi na kwao wamezaliwa watoto watatu Haruni, Miriam na mdogo wao Musa. Tunasoma hayo katika kitabu cha Hesabu 26:59 “Na jina la mke wa Amramu aliitwa Yokebedi binti wa Lawi ,ambaye alizaliwa kwake Lawi huko Misri; na huyo Yokebedi akamzalia Amram Haruni,na Musa,na Miriamu umbu lao”

    Tofauti nyingine ni kuumbwa kwao: ISSA KAUMBWA. Qur’an Suratul Imran, 3:59 “ Bila shaka hali ya Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama hali ya Adam; alimwumba kwa udongo kisha akamwambia: “Kuwa”; basi akawa”

    Lakini tusomapo kumhusu YESU, YEYE HAKUUMBWA BALI NI NENO LA MUNGU.

    Yoh 1 : 1,14 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu……..Naye Neno alifanyika mwili akakaa kwetu…….”

    Mika 5:2 “ Bali wewe, Bethlehem Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israel; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele”

    Yoh: 8:58 “ Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahim asijakuwako, mimi niko”.

    Zaidi ya hayo Biblia inatujulisha kuwa yeye ndiye Muumbaji mwenyewe

    Yoh 1:3 “Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika”

    Kol 1:16-17 “ Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana ; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake na kwa ajili yake”



    2) (A) ISSA A.S : BAADA YA KUONDOKA KWAKE, (KAMA WAISLAMU WANAVYOAMINI), HAJAWAHI KUTOKEA KWA NAMNA YOYOTE ILE.
    (B) YESU KRISTO: BAADA YA KUONDOKA KWAKE ALIMTOKEA PAUL (SAUL).
    Mdo 9:4 “ Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Saul, Saul, mbona waniudhi? Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema , Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe”



    3) (A) ISSA A.S: ALITABIRI KUJA KWA MUHAMMAD Quran Suratul As Saff , 61:6
    “Na (wakumbushe) aliposema (Nabii) Isa bin Maryamu (kuwaambia mayahudi) enyi wana wa Israili! mimi ni mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu. Nisadikishaye yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati. Na kutoa habari njema ya mtume atakayewajia nyuma yangu ambaye jina lake litakuwa Ahmad(Muhammad). Na maana ya majina mawili yote haya ni moja. Maana yake Mwenye kushukuriwa kwa maneno yake mazuri na vitendo vyake vizuri na kila chake kwani vyake vyote ni vizuri).Lakini alipowajia kwa hoja zilizowazi walisema: “ Huu ni udanganyifu uliyo dhahiri”.


    (B)YESU KRISTO ALIMTUMA ROHO MTAKATIFU KATIKA SIKU YA PENTEKOSTE.
    Yoh: 14:26 “.Lakini huyo Msaidizi,huyo Roho Mtakatifu,ambaye Baba atampeleka kwa jina langu,atawafundisha yote,na kuwakumbusha yote niliyowaambia”. Katka Kiyunani anaitwa “Paracletos” yaani msaidizi au mfariji

    Yoh 15:26 “ Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia”

    Yoh 16:7 “Lakini mimi ninawaambia iliyo kweli; yawafaa nyinyi mimi niondoke,kwa maana mimi nisipoondoka huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu nitampeleka kwenu”.



    4) (A) ISSA A.S : JINA LAKE HALINA NGUVU WALA UWEZO WA KUOKOA BALI NI RANGI MBILI
    Katika Al-Lu’lu’war-Marjani, Juzuu na1, Hadithi na104 uk. 64 “ Hadithi ya Ibn Abbas (r.a) kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema, “Nilimuona Musa (a.s) katika usiku wa Al-Isra, niliopelekwa,naye ni mtu mrefu, mwenye nywele za hudhurungi zimejikunjakunja kama mtu wa Shanua.Na nilimuona Isa (a.s), naye ni mtu wa wastani wa umbo, unaelekea kwenye wekundu na weupe, ana nywele zilizonyooka……”

    (B) YESU KRISTO: JINA LAKE NI WOKOVU. 
    Mdo 4:9-10,12 “ kama tukiulizwa leo habari ya jambo jema alilofanyiwa yule mtu dhaifu,jinsi alivyoponywa, jueni nyinyi nyote na watu wote wa Israel ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye nyinyi mlimsulubisha, na Mungu alimfufua katika wafu kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu…………………….Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo”

    Baadhi ya aya ndani ya Qur’an zinaeleza kuwa Isa a.s aliwaponya wenye upofu. Ni akina nani hao tutajiwe angalau mmoja? Yesu alimponya kipofu Batromayo.

    Aya zingine zinasema Isa a.s alifufua wafu. Ni akina nani hao? Yesu alimfufua Lazaro.

    Jina tulilopewa ni jina moja tu lenye wokovu la Yesu Kristo. Jina la Isa a.s lisilo na wokovu limehusishwaje na jina la Yesu Kristo wa Nazareth lenye wokovu?

    Mdo 16:31 “ Wakamwambia , Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka wewe pamoja na nyumba yako.”



    5) (A) ISSA.A.S : YEYE SIYO MWANA WA MUNGU. 
    Qur’ani Suratul Al An-Am,6:101 “Yeye ndiye Mwumba wa mbingu na ardhi. inamkinikanaje awe na mwana, hali hana mke. Naye ndiye aliye umba kila kitu (sio baadhi yake kavizaa). Naye ni mjuzi wa kila kitu”.

    Qurani Suratul At-Tawba (Kutubu), 9:30 “Na Mayahudi wanasema “Uzeri ni mwana wa Mwenyezi Mungu” na “Wakristo wanasema “Masihi ni Mwana wa Mwenyezi Mungu” Haya ndiyo wasemayo kwa vinywa vyao (pasi na kuyapima). Wanayaiga maneno ya wale waliokufuru kabla yao, Mwenyezi Mungu awaangamize. Wanageuzwa namna gani hawa!

    Fundisho la Uwana wa Mungu kama Biblia inavyofundisha, halimo katika mafundisho na itikadi ya dini ya Kiislamu kwa hiyo Isa a.s siyo mwana wa Mungu.

    (B) YESU KRISTO: YEYE NI MWANA WA MUNGU. Luka 1:30-31,35
    “Malaika akamwambia usiogope Mariamu,kwa maana umepata neema kwa Mungu.Tazama utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Malaika akajibu akamwambia,Roho Mtakatifu atakujilia juu yako,na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli;kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu Mwana wa Mungu.

    Hivyo Isa siyo Mwana Mungu lakini Yesu ni mwana wa Mungu. Kwa hivyo Yesu siyo Isa.



    6) (A) ISSA A.S: YEYE SIYO MUNGU ALIYEFANYIKA MWILI. 
    Suratul Al- Maidah,(meza), 5:72-73 Bila ya shaka wamekufuru wale waliosema, “ Mwenyezi Mungu ni Masih (issa)bin Maryam”.(Na hali ya kuwa)Masihi alisema “Enyi wana wa Israel! Mwabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wenu. Kwani anayemshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharimishia Pepo, na mahali pake (patakuwa) ni Motoni. Na madhalimu hawatakuwa na wasaidizi (wa kuwasaidia siku ya Kiama) “Kwa hakika wamekufuru wale waliosema mwenyenzi Mungu ni mmoja katika (wale waungu) watatu (yeye ndiye watatu wao ) hali hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu mmoja ( tu peke yake) na kama hawataacha hayo wasemayo kwa yakini itawakamata wale wanaoendelea na ukafiri miongoni mwao adhabu iumizayo”.

    (B)YESU YEYE NI NENO LA MUNGU LILILOFANYIKA MWILI:
    Yoh 1 : 1,14 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu……..Naye Neno alifanyika mwili akakaa kwetu…….”



    7) (A) ISSA A.S YEYE HAJAWAHI KUSULUBIWA WALA KUUWAWA
    Qurani Suratul An-Nisaa (Wanawake) 4:157-158

    “Na kwa (ajili ya )kusema kwao sisi tumemuua masihi Isa mwana wa Maryamu, mtume wa Mungu. Hali hawakumuua wala hawakumsulubu bali walibabaishiwa (mtu mwingine wakamdhani nabii Isa.) Na kwa hakika wale waliokhitalifiana katika (hakika)hiyo (ya kumuua nabii Isa) wamo katika shaka nalo (jambo hilo kusema kauwawa]. Wao (kabisa) hawana yakini juu ya (jambo)hili (la kuwa kweli wamemuua nabii isa) isipokuwa wanafuata dhana tu.Na kwa yakini hawakumuua. Bali mwenyenzi Mungu alimnyanyua kwake. Na mwenyenzi Mungu ni mwenye nguvu (na)mwenye hikima.

    (B)YESU KRISTO: YEYE ALISULUBIWA MSALABANI 
    Yohana 19:18,31,33 “Wakamsulibisha huko,na wengine wawili pamoja,mmoja huku na mmoja huku, na Yesu katikati.Basi Wayahudi, kwa sababu ni Maandalio, miili isikae juu ya misalaba siku ya sabato(maana sabato ile ilikuwa siku kubwa), walimwomba Pilato miguu yao ivunjwe,wakaondolewe. Lakini walipomjia Yesu na kuona ya kuwa amekwisha kufa,hawakumvunja miguu”.



    8) (A) ISSA A.S HANA HADHI YA KUABUDIWA NA BINADAMU YEYOTE.
    Qur’an, Suratul Al-Maidah, 5:116 “ Na (kumbukeni) Mwnyezi Mungu atakaposema: “Ewe Isa bin Maryam! Je ,wewe uliwaambia watu: ‘Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu’?” Aseme (Nabii Isa): “Wewe umetakasika na kuwa na mshirika, hainijuzii mimi kusema ambayo si haki yangu (kuyasema, kwa kuwa ni ya uongo), kama ningalisema bila shaka ungalijua ; unayajua yaliyomo nafsini mwangu, lakini mimi siyajui yaliyomo nafsini mwako; hakika Wewe ndiye ujuaye mambo ya ghaibu.

    B) YESU ANASTAHILI KUABUDIWA NA WANADAMU NA MALAIKA
    Math 2: 2 “yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? kwa maana tuliiona nyota yake mashariki nasi tumekuja kumsujudia.”

    Yoh 9: 35 “ Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; naye alipomwona alisema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu? Naye akajibu akasema, Ni nani, Bwana, nipate kumwamini? Yesu akamwambia Umemwona, naye anayesema nawe ndiye. Akasema, naamini, Bwana, akamsujudia.”

    Filipi 2:10-11 “ili kwa Jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.”

    Ebr 1:6 “ Hata tena amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema, Na wamsujudu Malaika wote wa Mungu.





    9) (A) ISA HASTAHILI KUWA MWOMBEZI WA WATU KWA MUNGU
    Sahih Al-Bukhari, vol.6 ,Hadithi no 3, The Noble Qur’an, English Translation uk. 8

    “…….Nenda kwa Musa, mtumishi wa Allah ambaye Allah alizungumza naye uso kwa uso na alimpa Torati. Hivyo watakwenda kwake naye atasema ‘ Mimi sistahili kwa jukumu hilo la uombezi, na atataja mauaji aliyoyafanya kwa mtu ambaye si muuaji, na hivyo atajisikia aibu mbele ya Mola wake, naye atasema nendeni kwa Isa, mtumishi wa Allah, Mjumbe wake neno lake na roho iliyotoka kwake. Isa atasema sistahili mimi kubeba jukumu la uombezi…….”

    B) YESU ANASTAHILI KUWA MWOMBEZI WA WANADAMU KWA MUNGU
    1 Tim 2:5 “ Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu;”
    Ebr 7:24-25 “ bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka.Naye, kwa sababu hii , aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu Hai siku zote ili awaombee.



    10) (a) ISA NI NABII MWINGINE TU ASIYE TOFAUTI NA WENGINE
    Qur’an Suratul Baqarah, (ng’ombe)2:136 “ “Semeni nyinyi (Waislamu waambiwe Mayahudi na Manasara; waambieni): “Tumemwamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyoteremshiwa, na yale yaliyoteremshwa kwa Ibrahimu na Ismail na Is-haqa na Yaaqubu na kizazi (chake Yaaqubu); na waliyopewa Musa na Isa na pia yale waliyopewa Manabii (wengine) kutoka kwa Mola wao; hatutofautishi baina ya yoyote katika hao. (Wote tunawaamini); na sisi tumenyenyekea Kwake.”

    b) YESU YEYE YU JUU KULIKO VITU VYOTE
    Efeso 1:20-23 “ aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; juu sana kuliko ufalme wote, na malaika, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; akavitia vitu vyote chini ya miguu yake akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya Kanisa; ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.”



    11) (a) ISA ATAKAPORUDI, ATAOA NA KUZAA WATOTO
    Mishkat Al- Masabih, vol 2 uk.1159, Sahih Muslim, vol. 1 uk 92 “ Isa atakaporudi ataishi miaka arobaini (40), muda ambao atakuwa ameoa na kuzaa watoto, na atafanya ibada ya hija.”

    b) YESU ATAKAPORUDI ATAKUJA KULINYAKUA KANISA, YAANI BIBI ARUSI
    Efeso 5:25-26, 32-33 “ Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, Uf 19:7 “ Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana Kondoo imekuja na mkewe amejiweka tayari.akajitoa kwa ajili yake, ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;…..Siri hiyo ni kubwa ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa. Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mmewe.”


    12)(a) ISA ATAKUFA BAADA YA KUISHI MIAKA AROBAINI (40)
    Mishkat Al- Masabih, vol 2 uk. 1159,Sunan Abu Dawud, Hadithi 4310, Sahih Muslim, vol.1, uk.92 , “Isa atakaporudi ataondosha dini zote zisiwepo isipokuwa Uislamu. Atamharibu Masih Dajjal, na ataishi duniani miaka arobaini (40) na kisha atakufa. Na baada ya kufa atazikwa pembeni mwa kaburi la Muhammad.”

    B) YESU BAADA YA KUFUFUKA YU HAI SIKU ZOTE HAFI TENA
    Rum 6:9 “ tukijua ya kuwa Kristo akiisha kufufuka katika wafu hafi tena, wala mauti haimtawali tena.”

    Ebr 7:24-25 “ bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka.Naye, kwa sababu hii , aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu Hai siku zote ili awaombee.”

    Uf 1:17-18 “ Nami nilipomwona nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, mimi ni wa kwanza na wa mwisho, aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama , ni hai hata milele na milele nami ninazo funguo za mauti na za kuzimu.”



    13)(a) ISA ALIPOZALIWA SAUTI YA FARAJA ILITOKA CHINI YA ARDHI
    Qur’an Suratul Maryam,19:23-24 “ Kisha uchungu ukampeleka katika shina la mtende, (akawa anazaa na huku) anasema: “ Laiti ningekufa kabla ya haya, na ningekuwa niliyesahaulika kabisa.” Mara ikamfikia sauti kutoka chini yake (inamwambia): usihuzunike. Hakika Mola wako amejaalia (ameweka) kijito cha maji chini yako;”

    Mafundisho ya Kiislamu yanaeleza kuwa huko chini ya ardhi kuna mnyama. Na huyo mnyama anazijua aya za Qur’an.

    Qur’an katika Suratul Al-Naml, 27:82 “Na kauli (ya kuja kiyama) itakapowathibitikia Tutawatolea mnyama katika ardhi atakayewasemeza kwa sababu watu walikuwa hawaziyakinishi Aya Zetu”

    b) ALIPOZALIWA YESU SAUTI ZA MALAIKA ZILITOKA JUU
    Luka 2:13-16 “ Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu na kusema, Atukuzwe Mungu juu mbinguni na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia. Ikawa malaika hao walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji waliambiana, Haya na twendeni mpaka Bethlehemu, tukalione hilo lililofanyika alilotujulisha Bwana. Wakaenda kwa haraka wakamkuta Mariamu na Yusufu, na yule mtoto mchanga amelala horini”



    (14)(a) ISA HANA UFAHAMU WA MAMBO MBALIMBALI 
    katika Al-Lu’lu’ war- Marjan,kitabu cha 3 Hadithi na 1528 uk.883 “Hadithi ya Abu Huraira (r.a) kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema “Issa Ibn Mariam (a,s) alimwona mtu anaiba akamuuliza umeiba? akasema hapana ,Naapa kwa Allah ambaye hakuna mola isipokuwa yeye .Issa (a.s) akasema nimemuamini Allah na limeniongopea jicho langu”.

    b) YESU ANAYAJUA YOTE
    Yohana 1:47-48 “ Basi Yesu akamwona Nathanael anakuja kwake, akanena habari zake “Tazama Mwizraeli kweli kweli hamna hila ndani yake. Nathaeli akamwambia umepataje kunitambua? Yesu akajibu akamwambia, Kabla Filipo hajakuita ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona”

    Yoh 2:24-25 “ Lakini Yesu hakujiaminisha kwao; kwa kuwa yeye aliwajua wote; na kwa sababu hakuwa na haja ya mtu kushuhudia habari za mwanadamu; kwa maana yeye mwenyewe aliyajua yaliyomo ndani ya mwanadamu”



    15) (a) ISA A.S MAMA YAKE ALIKUTWA PEMBEZONI MWA MSIKITI ALIPOLETEWA HABARI ZA KUZALIWA KWAKE.
    Qur’an Suratul Maryam,19:16-17 “ Na mtaje Mariamu kitabuni humu. Alipojitenga na jamaa zake, (akenda) mahali upande wa mashariki (wa msikiti) na akaweka pazia kujikinga nao. Tukampelekea muhuisha Sharia Yetu (Jibrili)- akajimithilisha kwake (kwa sura ya) binadamu aliye kamili


    b) YESU KRISTO, MAMA YAKE ALIKUTWA NYUMBANI KWAO NAZARETI
    Luka 1:26-28 “Mwezi wa sita malaika Gabriel alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti. Kwa mwana mwali Bikira aliyekuwa ameposwa na mtu jina lake Yusufu wa mbari ya Daudi. Na jina lake Bikira huyo ni Mariamu. Akaingia nyumbani kwake akasema, salamu uliyepewa neema Bwana yu pamoja nawe.”



    16)(a) MIMBA YA ISA ILIKUWA NI YA SIKU MOJA
    Qur’an Suratul Maryam,19:21-22 “ (Malaika) akasema: “ Nikama hivyo (unavyosema; lakini) Mola wako amesema ‘Haya ni sahali Kwangu, na ili Tumfanye muujiza kwa wanaasamu na rehema itokayo Kwetu (ndiyo Tumefanya hivi);’ Na hili ni jambo lililokwisha kuhukumiwa.” Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali”


    b) MIMBA YA YESU SIKU ZILITIMIA.
    Luka 2:6-7 “ ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia, akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni”


    NB: Mwezi wa sita uliotajwa katika Luka 1:26 ni mwezi wenye kuelezea umri wa mimba ya Yohana ndani ya tumbo la Elizabethi. Luka 1: 36 “ Tena tazama jamaa yako Elizabeti naye amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa”

    NB: Hori iliyotajwa hapa,ina maana ya chombo cha kulishia wanyama kinachokuwa ndani ya zizi. Kwa Kiyunani (Kigiriki) ambayo ndiyo lugha iliyotumika kuandikia Agano Jipya ,chombo hicho kinaitwa “Fatne” kwa Kiingereza kinaitwa “a manger”



    17)ISA (A.S) ATAKAPORUDI ATAKUJA KUVUNJA MISALABA NA KUUA NGURUWE
    Mkweli Mwaminifu, Juzuu 3-4, uk.20, Hadithi na. 753 “ Haisimami saa ya (kiyama) mpaka akuteremkieni nabii Isa (a.s) mwana wa Maryamu atahukumu (kwa sheria ya Kiislamu) (na) muadilifu, basi atavunja misalaba (ya Wakristo Makanisani) na ataua nguruwe, na ataondosha fedheha au (aibu), na mali itazidi kuwa nyingi sana mpaka hataikubali (ataikataa) mtu (kwa kuogopa kiyama)” .Soma pia katika Sahihi Bukhar, vol. 3, Hadithi na 425,. Al-Lu’lu’war-Marjan, juzuu ya 1,Hadithi na 95 uk.51. The Noble Qur’an uk.757

    b)YESU KRISTO ATAKAPORUDI ATAWATUMA MALAIKA ZAKE KUWAKUSANYA WATAKATIFU 
    Luka 24:30-31 “ ndipo itakapoonekana ishara ya mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi, naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.”


    ONYO LA YESU KRISTO WA NAZARETH
    Math 24:24 “ kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini hata walio wateule.” (Angalia pia Marko 13:22)

    Yoh 8:24 “ Kwa hiyo naliwambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye mtakufa katika dhambi zenu.”


    WEWE MTEULE JE UTADANGANYWA NA KUDANGANYIKA KUWA KWELI ISA A.S NDIYE YESU KRISTO? UKIAMINI HIVYO UTAKUWA UMEDANGANYIKA NA UTAKOSA WOKOVU WA MWENYEZI MUNGU!!!!!!!!!!


    YESU KRISTO, YEYE NI IMMANUEL, MSHAURI WA AJABU, MUNGU MWENYE NGUVU, BABA WA MILELE, MFALME WA AMANI!!!! (ISAYA 9:6, MATH 1:23)
    TOFAUTI KUMI NA SABA (17) KATI YA YESU WA WAKRISTO NA ISA WA WAISLAM. Mara kwa mara, unaweza kuwasikia Waislamu wakisema kuwa Isa a.s. kama anavyotajwa ndani ya Qur’an tukufu, ndiye Yesu Kristo wa Nazareti, kama anavyotajwa ndani ya Biblia Takatifu. Wanafanya hivyo kwa kulinganisha baadhi ya aya zilizomo ndani ya Biblia Takatifu, na zile zilizomo ndani ya Qur’an. Kwa mfano, wanasema kwa mujibu wa Biblia mama yake Yesu Kristo anaitwa Mariamu. Wanasoma katika Injili ya Marko 6:3-4“Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose na Yuda na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake” .  Wanafananisha aya hiyo na ile iliyomo ndani ya Qur’an katika Suratul Al-Maidah, 5:75 “ Masih bin Maryam si chochote ila ni mtume tu……”, Hoja nyingine wanayoitumia ni kusema kwamba eti jina Isa ni katika lugha ya Kiarabu. Jambo hilo siyo kweli. Kwa sababu katika lugha ya Kiarabu, Yesu anaitwa Yasu’a siyo Isa. Na ikumbukwe kuwa Biblia ndicho kitabu kilichotangulia kuwepo duniani miaka ipatayo 1500 kabla ya Qur’an.(Qur’an is a post Bible book). Hoja yetu kwa Waislamu ni hii nani aliyebadilisha jina Yasu’a kuwa Isa?. Jina Yasu’a linashabihiana zaidi na Jina Yehoshua ambalo hilo ni katika lugha ya Kiebrania, na katika Kiyunani lugha iliyotumika kuandika Agano Jipya anaitwa Iesous (tamka Yesu) tafsiri ya maneno hayo kwa lugha ya Kiswahili ni Mwokozi. Tunasoma hayo katika Math 1:21-23 “ Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana yeye ndiye atakaye waokoa watu wake na dhambi zao. Hayo yote yamekuwa ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa Nabii akisema Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.” Hoja yetu Je Isa a.s naye ni Mwokozi na Imanueli kama alivyo Yesu Kristo?. Jambo jingine tunalopaswa kulizingatia tunapoangalia tofauti zao ni kuhusu mama zao. Mama yake Yesu Kristo ni Mariam anayetoka katika ukoo wa Yuda. Tunasoma hayo katika kitabu cha Mwanzo 49:10 “ Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake,Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki,Ambaye mataifa watamtii”. Unabii huu umetimia kwa Yesu Kristo.Tunasoma hayo katika Waebrania 7:14 “Maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambayo Musa hakunena neno lolote juu yake katika mambo ya ukuhani” Lakini tusomapo habari za Isa, yeye mama yake anatoka ukoo wa Imrani. Ambaye ni baba yao Haruni, Miriamu na Musa. Tunayasoma hayo katika Suratul Al-Maryam 19:28 “Ewe dada yake Haruni. Baba yako hakuwa mtu mbaya. Wala mama yako hakuwa hasharati”. fafanuzi unaoifafanua aya hii ya 19:28 uliyomo ndani ya Qur’an, tafsiri ya King Fahd uk. 405, unasomeka hivi “ This Harun (Aaron) is not the brother of Musa (Moses), but he was another pious man at the time of Maryam (Mary)” Tafsiri “Huyu Harun siyo ndugu yake Musa, bali alikuwa ni mtu mwingine tu mcha Mungu, aliyeishi wakati wa kipindi cha Maryam” Kwa mujibu wa Biblia, Haruni ni mtoto wa mzee Amran na mama yao anaitwa Yekobedi na kwao wamezaliwa watoto watatu Haruni, Miriam na mdogo wao Musa. Tunasoma hayo katika kitabu cha Hesabu 26:59 “Na jina la mke wa Amramu aliitwa Yokebedi binti wa Lawi ,ambaye alizaliwa kwake Lawi huko Misri; na huyo Yokebedi akamzalia Amram Haruni,na Musa,na Miriamu umbu lao” Tofauti nyingine ni kuumbwa kwao: ISSA KAUMBWA. Qur’an Suratul Imran, 3:59 “ Bila shaka hali ya Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama hali ya Adam; alimwumba kwa udongo kisha akamwambia: “Kuwa”; basi akawa” Lakini tusomapo kumhusu YESU, YEYE HAKUUMBWA BALI NI NENO LA MUNGU. Yoh 1 : 1,14 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu……..Naye Neno alifanyika mwili akakaa kwetu…….” Mika 5:2 “ Bali wewe, Bethlehem Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israel; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele” Yoh: 8:58 “ Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahim asijakuwako, mimi niko”. Zaidi ya hayo Biblia inatujulisha kuwa yeye ndiye Muumbaji mwenyewe Yoh 1:3 “Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika” Kol 1:16-17 “ Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana ; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake na kwa ajili yake” 2) (A) ISSA A.S : BAADA YA KUONDOKA KWAKE, (KAMA WAISLAMU WANAVYOAMINI), HAJAWAHI KUTOKEA KWA NAMNA YOYOTE ILE. (B) YESU KRISTO: BAADA YA KUONDOKA KWAKE ALIMTOKEA PAUL (SAUL). Mdo 9:4 “ Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Saul, Saul, mbona waniudhi? Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema , Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe” 3) (A) ISSA A.S: ALITABIRI KUJA KWA MUHAMMAD Quran Suratul As Saff , 61:6 “Na (wakumbushe) aliposema (Nabii) Isa bin Maryamu (kuwaambia mayahudi) enyi wana wa Israili! mimi ni mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu. Nisadikishaye yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati. Na kutoa habari njema ya mtume atakayewajia nyuma yangu ambaye jina lake litakuwa Ahmad(Muhammad). Na maana ya majina mawili yote haya ni moja. Maana yake Mwenye kushukuriwa kwa maneno yake mazuri na vitendo vyake vizuri na kila chake kwani vyake vyote ni vizuri).Lakini alipowajia kwa hoja zilizowazi walisema: “ Huu ni udanganyifu uliyo dhahiri”. (B)YESU KRISTO ALIMTUMA ROHO MTAKATIFU KATIKA SIKU YA PENTEKOSTE. Yoh: 14:26 “.Lakini huyo Msaidizi,huyo Roho Mtakatifu,ambaye Baba atampeleka kwa jina langu,atawafundisha yote,na kuwakumbusha yote niliyowaambia”. Katka Kiyunani anaitwa “Paracletos” yaani msaidizi au mfariji Yoh 15:26 “ Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia” Yoh 16:7 “Lakini mimi ninawaambia iliyo kweli; yawafaa nyinyi mimi niondoke,kwa maana mimi nisipoondoka huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu nitampeleka kwenu”. 4) (A) ISSA A.S : JINA LAKE HALINA NGUVU WALA UWEZO WA KUOKOA BALI NI RANGI MBILI Katika Al-Lu’lu’war-Marjani, Juzuu na1, Hadithi na104 uk. 64 “ Hadithi ya Ibn Abbas (r.a) kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema, “Nilimuona Musa (a.s) katika usiku wa Al-Isra, niliopelekwa,naye ni mtu mrefu, mwenye nywele za hudhurungi zimejikunjakunja kama mtu wa Shanua.Na nilimuona Isa (a.s), naye ni mtu wa wastani wa umbo, unaelekea kwenye wekundu na weupe, ana nywele zilizonyooka……” (B) YESU KRISTO: JINA LAKE NI WOKOVU.  Mdo 4:9-10,12 “ kama tukiulizwa leo habari ya jambo jema alilofanyiwa yule mtu dhaifu,jinsi alivyoponywa, jueni nyinyi nyote na watu wote wa Israel ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye nyinyi mlimsulubisha, na Mungu alimfufua katika wafu kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu…………………….Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” Baadhi ya aya ndani ya Qur’an zinaeleza kuwa Isa a.s aliwaponya wenye upofu. Ni akina nani hao tutajiwe angalau mmoja? Yesu alimponya kipofu Batromayo. Aya zingine zinasema Isa a.s alifufua wafu. Ni akina nani hao? Yesu alimfufua Lazaro. Jina tulilopewa ni jina moja tu lenye wokovu la Yesu Kristo. Jina la Isa a.s lisilo na wokovu limehusishwaje na jina la Yesu Kristo wa Nazareth lenye wokovu? Mdo 16:31 “ Wakamwambia , Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka wewe pamoja na nyumba yako.” 5) (A) ISSA.A.S : YEYE SIYO MWANA WA MUNGU.  Qur’ani Suratul Al An-Am,6:101 “Yeye ndiye Mwumba wa mbingu na ardhi. inamkinikanaje awe na mwana, hali hana mke. Naye ndiye aliye umba kila kitu (sio baadhi yake kavizaa). Naye ni mjuzi wa kila kitu”. Qurani Suratul At-Tawba (Kutubu), 9:30 “Na Mayahudi wanasema “Uzeri ni mwana wa Mwenyezi Mungu” na “Wakristo wanasema “Masihi ni Mwana wa Mwenyezi Mungu” Haya ndiyo wasemayo kwa vinywa vyao (pasi na kuyapima). Wanayaiga maneno ya wale waliokufuru kabla yao, Mwenyezi Mungu awaangamize. Wanageuzwa namna gani hawa! Fundisho la Uwana wa Mungu kama Biblia inavyofundisha, halimo katika mafundisho na itikadi ya dini ya Kiislamu kwa hiyo Isa a.s siyo mwana wa Mungu. (B) YESU KRISTO: YEYE NI MWANA WA MUNGU. Luka 1:30-31,35 “Malaika akamwambia usiogope Mariamu,kwa maana umepata neema kwa Mungu.Tazama utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Malaika akajibu akamwambia,Roho Mtakatifu atakujilia juu yako,na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli;kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu Mwana wa Mungu. Hivyo Isa siyo Mwana Mungu lakini Yesu ni mwana wa Mungu. Kwa hivyo Yesu siyo Isa. 6) (A) ISSA A.S: YEYE SIYO MUNGU ALIYEFANYIKA MWILI.  Suratul Al- Maidah,(meza), 5:72-73 Bila ya shaka wamekufuru wale waliosema, “ Mwenyezi Mungu ni Masih (issa)bin Maryam”.(Na hali ya kuwa)Masihi alisema “Enyi wana wa Israel! Mwabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wenu. Kwani anayemshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharimishia Pepo, na mahali pake (patakuwa) ni Motoni. Na madhalimu hawatakuwa na wasaidizi (wa kuwasaidia siku ya Kiama) “Kwa hakika wamekufuru wale waliosema mwenyenzi Mungu ni mmoja katika (wale waungu) watatu (yeye ndiye watatu wao ) hali hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu mmoja ( tu peke yake) na kama hawataacha hayo wasemayo kwa yakini itawakamata wale wanaoendelea na ukafiri miongoni mwao adhabu iumizayo”. (B)YESU YEYE NI NENO LA MUNGU LILILOFANYIKA MWILI: Yoh 1 : 1,14 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu……..Naye Neno alifanyika mwili akakaa kwetu…….” 7) (A) ISSA A.S YEYE HAJAWAHI KUSULUBIWA WALA KUUWAWA Qurani Suratul An-Nisaa (Wanawake) 4:157-158 “Na kwa (ajili ya )kusema kwao sisi tumemuua masihi Isa mwana wa Maryamu, mtume wa Mungu. Hali hawakumuua wala hawakumsulubu bali walibabaishiwa (mtu mwingine wakamdhani nabii Isa.) Na kwa hakika wale waliokhitalifiana katika (hakika)hiyo (ya kumuua nabii Isa) wamo katika shaka nalo (jambo hilo kusema kauwawa]. Wao (kabisa) hawana yakini juu ya (jambo)hili (la kuwa kweli wamemuua nabii isa) isipokuwa wanafuata dhana tu.Na kwa yakini hawakumuua. Bali mwenyenzi Mungu alimnyanyua kwake. Na mwenyenzi Mungu ni mwenye nguvu (na)mwenye hikima. (B)YESU KRISTO: YEYE ALISULUBIWA MSALABANI  Yohana 19:18,31,33 “Wakamsulibisha huko,na wengine wawili pamoja,mmoja huku na mmoja huku, na Yesu katikati.Basi Wayahudi, kwa sababu ni Maandalio, miili isikae juu ya misalaba siku ya sabato(maana sabato ile ilikuwa siku kubwa), walimwomba Pilato miguu yao ivunjwe,wakaondolewe. Lakini walipomjia Yesu na kuona ya kuwa amekwisha kufa,hawakumvunja miguu”. 8) (A) ISSA A.S HANA HADHI YA KUABUDIWA NA BINADAMU YEYOTE. Qur’an, Suratul Al-Maidah, 5:116 “ Na (kumbukeni) Mwnyezi Mungu atakaposema: “Ewe Isa bin Maryam! Je ,wewe uliwaambia watu: ‘Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu’?” Aseme (Nabii Isa): “Wewe umetakasika na kuwa na mshirika, hainijuzii mimi kusema ambayo si haki yangu (kuyasema, kwa kuwa ni ya uongo), kama ningalisema bila shaka ungalijua ; unayajua yaliyomo nafsini mwangu, lakini mimi siyajui yaliyomo nafsini mwako; hakika Wewe ndiye ujuaye mambo ya ghaibu. B) YESU ANASTAHILI KUABUDIWA NA WANADAMU NA MALAIKA Math 2: 2 “yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? kwa maana tuliiona nyota yake mashariki nasi tumekuja kumsujudia.” Yoh 9: 35 “ Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; naye alipomwona alisema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu? Naye akajibu akasema, Ni nani, Bwana, nipate kumwamini? Yesu akamwambia Umemwona, naye anayesema nawe ndiye. Akasema, naamini, Bwana, akamsujudia.” Filipi 2:10-11 “ili kwa Jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.” Ebr 1:6 “ Hata tena amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema, Na wamsujudu Malaika wote wa Mungu. 9) (A) ISA HASTAHILI KUWA MWOMBEZI WA WATU KWA MUNGU Sahih Al-Bukhari, vol.6 ,Hadithi no 3, The Noble Qur’an, English Translation uk. 8 “…….Nenda kwa Musa, mtumishi wa Allah ambaye Allah alizungumza naye uso kwa uso na alimpa Torati. Hivyo watakwenda kwake naye atasema ‘ Mimi sistahili kwa jukumu hilo la uombezi, na atataja mauaji aliyoyafanya kwa mtu ambaye si muuaji, na hivyo atajisikia aibu mbele ya Mola wake, naye atasema nendeni kwa Isa, mtumishi wa Allah, Mjumbe wake neno lake na roho iliyotoka kwake. Isa atasema sistahili mimi kubeba jukumu la uombezi…….” B) YESU ANASTAHILI KUWA MWOMBEZI WA WANADAMU KWA MUNGU 1 Tim 2:5 “ Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu;” Ebr 7:24-25 “ bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka.Naye, kwa sababu hii , aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu Hai siku zote ili awaombee. 10) (a) ISA NI NABII MWINGINE TU ASIYE TOFAUTI NA WENGINE Qur’an Suratul Baqarah, (ng’ombe)2:136 “ “Semeni nyinyi (Waislamu waambiwe Mayahudi na Manasara; waambieni): “Tumemwamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyoteremshiwa, na yale yaliyoteremshwa kwa Ibrahimu na Ismail na Is-haqa na Yaaqubu na kizazi (chake Yaaqubu); na waliyopewa Musa na Isa na pia yale waliyopewa Manabii (wengine) kutoka kwa Mola wao; hatutofautishi baina ya yoyote katika hao. (Wote tunawaamini); na sisi tumenyenyekea Kwake.” b) YESU YEYE YU JUU KULIKO VITU VYOTE Efeso 1:20-23 “ aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; juu sana kuliko ufalme wote, na malaika, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; akavitia vitu vyote chini ya miguu yake akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya Kanisa; ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.” 11) (a) ISA ATAKAPORUDI, ATAOA NA KUZAA WATOTO Mishkat Al- Masabih, vol 2 uk.1159, Sahih Muslim, vol. 1 uk 92 “ Isa atakaporudi ataishi miaka arobaini (40), muda ambao atakuwa ameoa na kuzaa watoto, na atafanya ibada ya hija.” b) YESU ATAKAPORUDI ATAKUJA KULINYAKUA KANISA, YAANI BIBI ARUSI Efeso 5:25-26, 32-33 “ Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, Uf 19:7 “ Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana Kondoo imekuja na mkewe amejiweka tayari.akajitoa kwa ajili yake, ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;…..Siri hiyo ni kubwa ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa. Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mmewe.” 12)(a) ISA ATAKUFA BAADA YA KUISHI MIAKA AROBAINI (40) Mishkat Al- Masabih, vol 2 uk. 1159,Sunan Abu Dawud, Hadithi 4310, Sahih Muslim, vol.1, uk.92 , “Isa atakaporudi ataondosha dini zote zisiwepo isipokuwa Uislamu. Atamharibu Masih Dajjal, na ataishi duniani miaka arobaini (40) na kisha atakufa. Na baada ya kufa atazikwa pembeni mwa kaburi la Muhammad.” B) YESU BAADA YA KUFUFUKA YU HAI SIKU ZOTE HAFI TENA Rum 6:9 “ tukijua ya kuwa Kristo akiisha kufufuka katika wafu hafi tena, wala mauti haimtawali tena.” Ebr 7:24-25 “ bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka.Naye, kwa sababu hii , aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu Hai siku zote ili awaombee.” Uf 1:17-18 “ Nami nilipomwona nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, mimi ni wa kwanza na wa mwisho, aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama , ni hai hata milele na milele nami ninazo funguo za mauti na za kuzimu.” 13)(a) ISA ALIPOZALIWA SAUTI YA FARAJA ILITOKA CHINI YA ARDHI Qur’an Suratul Maryam,19:23-24 “ Kisha uchungu ukampeleka katika shina la mtende, (akawa anazaa na huku) anasema: “ Laiti ningekufa kabla ya haya, na ningekuwa niliyesahaulika kabisa.” Mara ikamfikia sauti kutoka chini yake (inamwambia): usihuzunike. Hakika Mola wako amejaalia (ameweka) kijito cha maji chini yako;” Mafundisho ya Kiislamu yanaeleza kuwa huko chini ya ardhi kuna mnyama. Na huyo mnyama anazijua aya za Qur’an. Qur’an katika Suratul Al-Naml, 27:82 “Na kauli (ya kuja kiyama) itakapowathibitikia Tutawatolea mnyama katika ardhi atakayewasemeza kwa sababu watu walikuwa hawaziyakinishi Aya Zetu” b) ALIPOZALIWA YESU SAUTI ZA MALAIKA ZILITOKA JUU Luka 2:13-16 “ Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu na kusema, Atukuzwe Mungu juu mbinguni na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia. Ikawa malaika hao walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji waliambiana, Haya na twendeni mpaka Bethlehemu, tukalione hilo lililofanyika alilotujulisha Bwana. Wakaenda kwa haraka wakamkuta Mariamu na Yusufu, na yule mtoto mchanga amelala horini” (14)(a) ISA HANA UFAHAMU WA MAMBO MBALIMBALI  katika Al-Lu’lu’ war- Marjan,kitabu cha 3 Hadithi na 1528 uk.883 “Hadithi ya Abu Huraira (r.a) kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema “Issa Ibn Mariam (a,s) alimwona mtu anaiba akamuuliza umeiba? akasema hapana ,Naapa kwa Allah ambaye hakuna mola isipokuwa yeye .Issa (a.s) akasema nimemuamini Allah na limeniongopea jicho langu”. b) YESU ANAYAJUA YOTE Yohana 1:47-48 “ Basi Yesu akamwona Nathanael anakuja kwake, akanena habari zake “Tazama Mwizraeli kweli kweli hamna hila ndani yake. Nathaeli akamwambia umepataje kunitambua? Yesu akajibu akamwambia, Kabla Filipo hajakuita ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona” Yoh 2:24-25 “ Lakini Yesu hakujiaminisha kwao; kwa kuwa yeye aliwajua wote; na kwa sababu hakuwa na haja ya mtu kushuhudia habari za mwanadamu; kwa maana yeye mwenyewe aliyajua yaliyomo ndani ya mwanadamu” 15) (a) ISA A.S MAMA YAKE ALIKUTWA PEMBEZONI MWA MSIKITI ALIPOLETEWA HABARI ZA KUZALIWA KWAKE. Qur’an Suratul Maryam,19:16-17 “ Na mtaje Mariamu kitabuni humu. Alipojitenga na jamaa zake, (akenda) mahali upande wa mashariki (wa msikiti) na akaweka pazia kujikinga nao. Tukampelekea muhuisha Sharia Yetu (Jibrili)- akajimithilisha kwake (kwa sura ya) binadamu aliye kamili b) YESU KRISTO, MAMA YAKE ALIKUTWA NYUMBANI KWAO NAZARETI Luka 1:26-28 “Mwezi wa sita malaika Gabriel alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti. Kwa mwana mwali Bikira aliyekuwa ameposwa na mtu jina lake Yusufu wa mbari ya Daudi. Na jina lake Bikira huyo ni Mariamu. Akaingia nyumbani kwake akasema, salamu uliyepewa neema Bwana yu pamoja nawe.” 16)(a) MIMBA YA ISA ILIKUWA NI YA SIKU MOJA Qur’an Suratul Maryam,19:21-22 “ (Malaika) akasema: “ Nikama hivyo (unavyosema; lakini) Mola wako amesema ‘Haya ni sahali Kwangu, na ili Tumfanye muujiza kwa wanaasamu na rehema itokayo Kwetu (ndiyo Tumefanya hivi);’ Na hili ni jambo lililokwisha kuhukumiwa.” Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali” b) MIMBA YA YESU SIKU ZILITIMIA. Luka 2:6-7 “ ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia, akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni” NB: Mwezi wa sita uliotajwa katika Luka 1:26 ni mwezi wenye kuelezea umri wa mimba ya Yohana ndani ya tumbo la Elizabethi. Luka 1: 36 “ Tena tazama jamaa yako Elizabeti naye amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa” NB: Hori iliyotajwa hapa,ina maana ya chombo cha kulishia wanyama kinachokuwa ndani ya zizi. Kwa Kiyunani (Kigiriki) ambayo ndiyo lugha iliyotumika kuandikia Agano Jipya ,chombo hicho kinaitwa “Fatne” kwa Kiingereza kinaitwa “a manger” 17)ISA (A.S) ATAKAPORUDI ATAKUJA KUVUNJA MISALABA NA KUUA NGURUWE Mkweli Mwaminifu, Juzuu 3-4, uk.20, Hadithi na. 753 “ Haisimami saa ya (kiyama) mpaka akuteremkieni nabii Isa (a.s) mwana wa Maryamu atahukumu (kwa sheria ya Kiislamu) (na) muadilifu, basi atavunja misalaba (ya Wakristo Makanisani) na ataua nguruwe, na ataondosha fedheha au (aibu), na mali itazidi kuwa nyingi sana mpaka hataikubali (ataikataa) mtu (kwa kuogopa kiyama)” .Soma pia katika Sahihi Bukhar, vol. 3, Hadithi na 425,. Al-Lu’lu’war-Marjan, juzuu ya 1,Hadithi na 95 uk.51. The Noble Qur’an uk.757 b)YESU KRISTO ATAKAPORUDI ATAWATUMA MALAIKA ZAKE KUWAKUSANYA WATAKATIFU  Luka 24:30-31 “ ndipo itakapoonekana ishara ya mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi, naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.” ONYO LA YESU KRISTO WA NAZARETH Math 24:24 “ kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini hata walio wateule.” (Angalia pia Marko 13:22) Yoh 8:24 “ Kwa hiyo naliwambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye mtakufa katika dhambi zenu.” WEWE MTEULE JE UTADANGANYWA NA KUDANGANYIKA KUWA KWELI ISA A.S NDIYE YESU KRISTO? UKIAMINI HIVYO UTAKUWA UMEDANGANYIKA NA UTAKOSA WOKOVU WA MWENYEZI MUNGU!!!!!!!!!! YESU KRISTO, YEYE NI IMMANUEL, MSHAURI WA AJABU, MUNGU MWENYE NGUVU, BABA WA MILELE, MFALME WA AMANI!!!! (ISAYA 9:6, MATH 1:23)
    0 Kommentare 0 Geteilt 13KB Ansichten 0 Bewertungen
  • UPONYAJI WA MAGONJWA.

    Chanzo cha magonjwa: Magonjwa yanatokana na mtu kufanya dhambi. Ndiyo maana Yesu alipomponya mtu aliyekuwa mngonjwa alimwonya akisema, “…Angalia umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi” Yn 5:14. Mtu akiwa amefanya dhambi anapoumwa na kupimwa ugonjwa unaonekana. Iwapo akipimwa vipomo vyote na ugonjwa hauonekani yamkini ni pepo wachafu wamemwingia. “Mara huenda akachukua pamoja naye pepo wengine walio waovu kuliko yeye mwenyewe nao huingia na kukaa humo; na mtu Yule hali yake huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya” Mt 12:45.

    Wakati mwingine sii kila mtu anayeumwa amefanya dhambi, bali ni matokeo ya ugonjwa katika mwili, unaotokana kukosa lishe ya mlo wa kila siku (Utapia mlo). Mapungufu katika mwili wa mwanadamu yanaweza yakawa ni kusudi la Mungu, ijapokuwa si yote. “Bwana akamwambia, Ni nani aliyekifanya kinywa cha mwanadamu? Au ni nani amfanyaye mtu kuwa bubu au kiziwi, au mwenye kuona, au kuwa kipofu? Si mimi, Bwana? Kut 4:11.

    Kuponywa kwa dawa.

    Kwa kawaida kuna njia ambayo imekuwa ikitumika ya kutibu mangonjwa ambayo ni kutibu kwa kutumia dawa. Tiba za dawa zimekuwapo kwa ajili ya kutibu magonjwa mbalimbali. Mtu anapokuwa mgonjwa kuna hatua ya kuchukua, kwanza anaenda hospitali au kupelekwa kutona na hali yake hajiwezi. Daktari anampima na kufahamu ugonjwa alio nao, halafu anamwandikia dawa na maelekezo ya kuzitumia. Kama hatazingatia maelekezo na kuzitumia haiwezekani akapona. Hapa tunaweza kuona mgonjwa ili apone ni lazima azingatie maelekezo aliyopewa na daktari. Lakini baadhi ya magonjwa hayana tiba kama UKIMWI (HIV Aids). Hata hivyo usikate tamaa mwamini Mungu anaweza kukuponya kwa njia ya kumwomba. Atakuponya kwa neema, na rehema, kwa uwezo na nguvu zake.VIlevile kuna kanuni na maelekezo ya kufuata ili Mungu akuponye

    UPONYAJI WA MUNGU. Una maelekezo na kanuni za kufuata:

    1. Kutubu na kuziacha dhambi: “Azifichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema” Mit 28:13. “Twajua ya kwamba Mungu hawasikii wenye dhambi;bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake huyo humsikia” Yn 9:31.

    2. Kuishi maisha ya utakatifu: Ndio maana Mungu amesema; “Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako. Na Bwana atakuondolea ugonjwa wote…” Kumb 7:12, 15. Katika maandiko haya tunaona Mungu alisema na baba zetu ya kwamba kwa upande wetu tunapozishika na kuzitenda hukumu zake (Sheria zake). Na kwa upande wake yeye ndipo hutuondolea ugonjwa wote. Kwa sababu Mungu aliwaapia baba zetu akisema, nitakutimizia agano na rehema. Kwa kiapo chake anathibitisha atafanya yale aliyoahidi katika Agano alilolifanya na baba zetu. Mahali pengine tunasoma:

    “Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote,…Mche Bwana, ukajiepushe na uovu, Itakuwa afya mwilini pako. Na mafuta mifupani mwako. Mwanangu, sikiliza maneno yangu; Tega sikio lako, uzishike kauli zangu. Kwa maana ni uhai kwa wale wazipatao, Na afya ya mwili wao wote”Mit 3:5,7,8.

    3.Kumwamini Mungu na neno lake: Ndiyo maana Mungu alisema “Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita roho yangu haina furaha naye.” Ebr 10:38. Kutokana na andiko hili, linaonyesha lazima mtu awe mwenye haki ndipo aweze kuishi kwa imani. Pia lazima kwanza kuamini moyoni na kuwa na uhakika Mungu atakuponya kama neno linavyosema,“Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana (wazi) ya mambo yasiyoonekana” Ebr 11:1
    4. Kuishi maisha ya unyenyekevu: “Dhabihu za Mungu ni mioyo iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka Ee Mungu hutaudharau. “Huwaponya waliopondeka moyo, Na kuwaganga jeraha zao” Zab 51:17; 147:3. Mungu anahitaji watu waliovunjika na kupondeka moyo ili awaponye. Maana ya kuvunjika na kupondeka moyo ni kunyenyekea chini ya Mungu na kujua yeye ni mwenye uwezo na nguvu zote; kutokuwa na kiburi na kujiona wewe ni bora kuliko wengine, kutokuonee na kunyanyasa wengine, kutokujivunia ulivyo nayo na kujisifia kwa yale unayoyafanya na kutokudharau wengine au kuwapuuza. “Amdharauye mwenzake afanya dhambi;…” Mit 14:21. Yesu Kristo yeye ni mfano kwetu, alikuwa ni mnyenyekevu aliacha enzi na mamlaka aliyokuwa nayo mbinguni akaja duniani kwa namna ya mtumwa hakutaka makuu na fahari, alimtii Mungu.

    5. Kuomba kwa imani: “Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa , tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba”Yoh 5:14-15. Haya maandiko yanafundisha ni muhimu kujua kwamba tunapomwomba Mungu anatuskia, tunapoomba sawaswa na mapenzi yake (neno lake). Pia kujua tulichoomba tunacho tayari. Kama umemwomba Mungu akuponye unajua umepona, hii ni imani katika Mungu. Ndiyo maana Yesu alifundisha akisema, “Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaoombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu” Mk 11:24.

    6. Kuomba kwa bidii: Kuomba kwa bidii bila kukata tamaa hadi Bwana akuponye kabisa. Iwapo umeomba lakini bado Bwana hajakuponya, endelea kunyenyeke na kumlilia tena na tena mpaka Bwana akuponye. Kuomba kwa bidii ni mfano wa mwanariadha anayeshindana na wanariadha kwa kukimbia. Mwanariada anayeshinda ni kwa sababu amekimbia kwa bidii na kupewa zawadi. Kuna mifano ya kufuata ya watumishi wa Mungu waliomwomba Mungu kwa bidii tena na tena wakajibiwa, mmojapo ni Eliya;
    “Naye Eliya akapanda juu mpaka kilele cha Karmeli; akasujudu kifudifudi; akainama uso mpaka magotini. Akamwambia mtumishi wake, kwea sasa ukatazame upande wa bahari. Akakwea na kutazama, akasema, hakuna kitu. Naye akanena, enenda tena mara saba. Ikawa mara ya saba akasema, tazama, wingu linatoka katika bahari, nalo ni dogo kama mkono wa mtu. … Ikawa muda si muda, mbingu zikawa nyeusi kwa mawingu na upepo, ikawa mvua nyingi…” 1Fal 18:42-45. Hapa maandiko yanaonyesha jinsi Eliya alimwomba Mungu mara ya kwanza na mara ya pili, wingu la mvua halikutokea lakini hakukata tamaa aliendelea kuomba mpaka mara ya saba wingu likaonekana na mvua ikanyesha. Na mwingine aliyeomba kwa bidii na kujibiwa ni Elisha baada ya kumtuma Gehazi mtumishi wake kumfufua mtoto.

    “Na Gehazi akawatagulia, akaiweka ile fimbo juu ya mtoto; lakini hapakuwa na sauti wala majibu. Basi Elisha alipofika nyumbani, tazama, mtoto amekwisha kufa, amelazwa kitandani pake. Basi akaingia ndani akajifungia mlango, yeye na Yule mtoto wote wawili, akamwomba Bwana... Kisha akarudi, akatembea nyumbani, huko Na huko mara moja; akapanda akajinyoosha juu yake; Na Yule mtoto akapiga chafya mara Saba, Na mtoto akafumbua macho yake.” 2 Fal 4:31-35. Elisha naye alimtuma mtumishi wake Gehazi akaiweke fimbo juu mtoto abaye alikuwa amekufa ili afufuke, wala hakufufuka, lakini Elisha hakukata tamaa alikwenda mwenyewe akamwomba Mungu mara ya kwanza na mara ya pili na mtoto akafufuka.

    7. Kumshukuru Mungu: “Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.” 1The 5:18. Katika maisha yetu ni muhimu tumshukuru Mungu kwa ajili ya mema yote anayotutende kila siku.

    Mungu ni mwaminifu.
    Yale yote aliyoyaahidi katika neno lake hakika atayafanya kama alivyosema; “Mimi sitalihalifu agano langu, sitalibadili Neno lililotoka midomoni mwangu.” Zab 89:34. “Nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu” Kut 20:6. “Maana Kama vile mvua ishukavyo, Na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; Bali huinywesha ardhi, Na kuizalisha Na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, Na mtu alaye chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure Bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma” Isa 55:10-11.

    USHUHUDA. Hapa ninatoa ushuhuda wa mtu ambaye Bwana amemponya mara nyingi kwa magonjwa tofauti. Siri ya uponyaji wake ni kwamba yeye ni mtakatifu amejilinda na kuepuka dhambi. kumbuka dhambi ni kizuizi cha uponyaji wa Mungu kwako. Amekuwa ni mwenye imani na unyenyekevu, amevunjika na kupondeka moyo. Wakati mwingine anapomwomba Mungu huanguka kifulifuli akimsihi Mungu. Hakika mtu kama huyu atasikilizwa kwa sababu anao ujasiri, hana dhambi inayomhukumu ndani ya moyo wake.

    Ndio maana imeandikwa “Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri (bila dhambi), ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.” Ebr 4:16. Mtu anapodumu katika maisha ya kumpendeza Mungu anapata neema au upendeleo kujibiwa maombi. Wakati mwingine hata kabla ya kuomba hujibiwa. “Na itakuwa kwamba, kabla ya kuomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia.” Isa 65:24. “….maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba.” Mt 6:8.
    UPONYAJI WA MAGONJWA. Chanzo cha magonjwa: Magonjwa yanatokana na mtu kufanya dhambi. Ndiyo maana Yesu alipomponya mtu aliyekuwa mngonjwa alimwonya akisema, “…Angalia umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi” Yn 5:14. Mtu akiwa amefanya dhambi anapoumwa na kupimwa ugonjwa unaonekana. Iwapo akipimwa vipomo vyote na ugonjwa hauonekani yamkini ni pepo wachafu wamemwingia. “Mara huenda akachukua pamoja naye pepo wengine walio waovu kuliko yeye mwenyewe nao huingia na kukaa humo; na mtu Yule hali yake huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya” Mt 12:45. Wakati mwingine sii kila mtu anayeumwa amefanya dhambi, bali ni matokeo ya ugonjwa katika mwili, unaotokana kukosa lishe ya mlo wa kila siku (Utapia mlo). Mapungufu katika mwili wa mwanadamu yanaweza yakawa ni kusudi la Mungu, ijapokuwa si yote. “Bwana akamwambia, Ni nani aliyekifanya kinywa cha mwanadamu? Au ni nani amfanyaye mtu kuwa bubu au kiziwi, au mwenye kuona, au kuwa kipofu? Si mimi, Bwana? Kut 4:11. Kuponywa kwa dawa. Kwa kawaida kuna njia ambayo imekuwa ikitumika ya kutibu mangonjwa ambayo ni kutibu kwa kutumia dawa. Tiba za dawa zimekuwapo kwa ajili ya kutibu magonjwa mbalimbali. Mtu anapokuwa mgonjwa kuna hatua ya kuchukua, kwanza anaenda hospitali au kupelekwa kutona na hali yake hajiwezi. Daktari anampima na kufahamu ugonjwa alio nao, halafu anamwandikia dawa na maelekezo ya kuzitumia. Kama hatazingatia maelekezo na kuzitumia haiwezekani akapona. Hapa tunaweza kuona mgonjwa ili apone ni lazima azingatie maelekezo aliyopewa na daktari. Lakini baadhi ya magonjwa hayana tiba kama UKIMWI (HIV Aids). Hata hivyo usikate tamaa mwamini Mungu anaweza kukuponya kwa njia ya kumwomba. Atakuponya kwa neema, na rehema, kwa uwezo na nguvu zake.VIlevile kuna kanuni na maelekezo ya kufuata ili Mungu akuponye UPONYAJI WA MUNGU. Una maelekezo na kanuni za kufuata: 1. Kutubu na kuziacha dhambi: “Azifichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema” Mit 28:13. “Twajua ya kwamba Mungu hawasikii wenye dhambi;bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake huyo humsikia” Yn 9:31. 2. Kuishi maisha ya utakatifu: Ndio maana Mungu amesema; “Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako. Na Bwana atakuondolea ugonjwa wote…” Kumb 7:12, 15. Katika maandiko haya tunaona Mungu alisema na baba zetu ya kwamba kwa upande wetu tunapozishika na kuzitenda hukumu zake (Sheria zake). Na kwa upande wake yeye ndipo hutuondolea ugonjwa wote. Kwa sababu Mungu aliwaapia baba zetu akisema, nitakutimizia agano na rehema. Kwa kiapo chake anathibitisha atafanya yale aliyoahidi katika Agano alilolifanya na baba zetu. Mahali pengine tunasoma: “Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote,…Mche Bwana, ukajiepushe na uovu, Itakuwa afya mwilini pako. Na mafuta mifupani mwako. Mwanangu, sikiliza maneno yangu; Tega sikio lako, uzishike kauli zangu. Kwa maana ni uhai kwa wale wazipatao, Na afya ya mwili wao wote”Mit 3:5,7,8. 3.Kumwamini Mungu na neno lake: Ndiyo maana Mungu alisema “Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita roho yangu haina furaha naye.” Ebr 10:38. Kutokana na andiko hili, linaonyesha lazima mtu awe mwenye haki ndipo aweze kuishi kwa imani. Pia lazima kwanza kuamini moyoni na kuwa na uhakika Mungu atakuponya kama neno linavyosema,“Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana (wazi) ya mambo yasiyoonekana” Ebr 11:1 4. Kuishi maisha ya unyenyekevu: “Dhabihu za Mungu ni mioyo iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka Ee Mungu hutaudharau. “Huwaponya waliopondeka moyo, Na kuwaganga jeraha zao” Zab 51:17; 147:3. Mungu anahitaji watu waliovunjika na kupondeka moyo ili awaponye. Maana ya kuvunjika na kupondeka moyo ni kunyenyekea chini ya Mungu na kujua yeye ni mwenye uwezo na nguvu zote; kutokuwa na kiburi na kujiona wewe ni bora kuliko wengine, kutokuonee na kunyanyasa wengine, kutokujivunia ulivyo nayo na kujisifia kwa yale unayoyafanya na kutokudharau wengine au kuwapuuza. “Amdharauye mwenzake afanya dhambi;…” Mit 14:21. Yesu Kristo yeye ni mfano kwetu, alikuwa ni mnyenyekevu aliacha enzi na mamlaka aliyokuwa nayo mbinguni akaja duniani kwa namna ya mtumwa hakutaka makuu na fahari, alimtii Mungu. 5. Kuomba kwa imani: “Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa , tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba”Yoh 5:14-15. Haya maandiko yanafundisha ni muhimu kujua kwamba tunapomwomba Mungu anatuskia, tunapoomba sawaswa na mapenzi yake (neno lake). Pia kujua tulichoomba tunacho tayari. Kama umemwomba Mungu akuponye unajua umepona, hii ni imani katika Mungu. Ndiyo maana Yesu alifundisha akisema, “Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaoombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu” Mk 11:24. 6. Kuomba kwa bidii: Kuomba kwa bidii bila kukata tamaa hadi Bwana akuponye kabisa. Iwapo umeomba lakini bado Bwana hajakuponya, endelea kunyenyeke na kumlilia tena na tena mpaka Bwana akuponye. Kuomba kwa bidii ni mfano wa mwanariadha anayeshindana na wanariadha kwa kukimbia. Mwanariada anayeshinda ni kwa sababu amekimbia kwa bidii na kupewa zawadi. Kuna mifano ya kufuata ya watumishi wa Mungu waliomwomba Mungu kwa bidii tena na tena wakajibiwa, mmojapo ni Eliya; “Naye Eliya akapanda juu mpaka kilele cha Karmeli; akasujudu kifudifudi; akainama uso mpaka magotini. Akamwambia mtumishi wake, kwea sasa ukatazame upande wa bahari. Akakwea na kutazama, akasema, hakuna kitu. Naye akanena, enenda tena mara saba. Ikawa mara ya saba akasema, tazama, wingu linatoka katika bahari, nalo ni dogo kama mkono wa mtu. … Ikawa muda si muda, mbingu zikawa nyeusi kwa mawingu na upepo, ikawa mvua nyingi…” 1Fal 18:42-45. Hapa maandiko yanaonyesha jinsi Eliya alimwomba Mungu mara ya kwanza na mara ya pili, wingu la mvua halikutokea lakini hakukata tamaa aliendelea kuomba mpaka mara ya saba wingu likaonekana na mvua ikanyesha. Na mwingine aliyeomba kwa bidii na kujibiwa ni Elisha baada ya kumtuma Gehazi mtumishi wake kumfufua mtoto. “Na Gehazi akawatagulia, akaiweka ile fimbo juu ya mtoto; lakini hapakuwa na sauti wala majibu. Basi Elisha alipofika nyumbani, tazama, mtoto amekwisha kufa, amelazwa kitandani pake. Basi akaingia ndani akajifungia mlango, yeye na Yule mtoto wote wawili, akamwomba Bwana... Kisha akarudi, akatembea nyumbani, huko Na huko mara moja; akapanda akajinyoosha juu yake; Na Yule mtoto akapiga chafya mara Saba, Na mtoto akafumbua macho yake.” 2 Fal 4:31-35. Elisha naye alimtuma mtumishi wake Gehazi akaiweke fimbo juu mtoto abaye alikuwa amekufa ili afufuke, wala hakufufuka, lakini Elisha hakukata tamaa alikwenda mwenyewe akamwomba Mungu mara ya kwanza na mara ya pili na mtoto akafufuka. 7. Kumshukuru Mungu: “Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.” 1The 5:18. Katika maisha yetu ni muhimu tumshukuru Mungu kwa ajili ya mema yote anayotutende kila siku. Mungu ni mwaminifu. Yale yote aliyoyaahidi katika neno lake hakika atayafanya kama alivyosema; “Mimi sitalihalifu agano langu, sitalibadili Neno lililotoka midomoni mwangu.” Zab 89:34. “Nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu” Kut 20:6. “Maana Kama vile mvua ishukavyo, Na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; Bali huinywesha ardhi, Na kuizalisha Na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, Na mtu alaye chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure Bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma” Isa 55:10-11. USHUHUDA. Hapa ninatoa ushuhuda wa mtu ambaye Bwana amemponya mara nyingi kwa magonjwa tofauti. Siri ya uponyaji wake ni kwamba yeye ni mtakatifu amejilinda na kuepuka dhambi. kumbuka dhambi ni kizuizi cha uponyaji wa Mungu kwako. Amekuwa ni mwenye imani na unyenyekevu, amevunjika na kupondeka moyo. Wakati mwingine anapomwomba Mungu huanguka kifulifuli akimsihi Mungu. Hakika mtu kama huyu atasikilizwa kwa sababu anao ujasiri, hana dhambi inayomhukumu ndani ya moyo wake. Ndio maana imeandikwa “Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri (bila dhambi), ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.” Ebr 4:16. Mtu anapodumu katika maisha ya kumpendeza Mungu anapata neema au upendeleo kujibiwa maombi. Wakati mwingine hata kabla ya kuomba hujibiwa. “Na itakuwa kwamba, kabla ya kuomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia.” Isa 65:24. “….maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba.” Mt 6:8.
    Love
    1
    0 Kommentare 2 Geteilt 9KB Ansichten 0 Bewertungen
  • KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

    Yakupasa kuwa makini sana usisahau kuishi maisha ya ukamilifu. Unaweza kusahau mambo mengine, lakini jambo hili la ukamilifu yakupasa kukumbuka wakati wote. Tafakari kila wakati je wewe ni mkamilifu.

    Ni muhimu kuishi a ukamilifu kwa sababu hujui saa wala wakati ambao utaondoka hapa duniani. Siku ile ya mwisho inakuja ghafla ambayo kanisa litanyakuliwa ni siku ambayo hakuna anayeijua. Waliotayari katika ukamilifu hao ndio watakaonyakuliwa. Wale ambao si wakamilifu wataachwa na kuhukumu na kutupwa katika ziwa la moto

    Kuliko utengwe na uso wa Mungu milele ni bora kuhakikisha kila wakati unaishi katika ukamilifu.

    Hakikisha wewe ni mkamilifu katika mambo yote ya Mungu na kwa wanadamu. Kwa sababu hiyo yakupasa kumpendeza Mungu na wanadamu, ndipo utakuwa umepata kibali mbele za Mungu.

    Hakikisha wewe ni mkamilifu wakati ukiwa umelala, unatembea, unakula, unapoongea na watu, unaposafiri, unapokuwa katika shughuli zako mbalimbali.

    Ndugu, tambua ya kwamba Mungu anakupenda amekupa nafasi moja tu. Hii ni nafasi ya pekee na kwa neema ya Mungu Baba yetu. Shetani na Malaika zake ambao walimwasi Mungu hawajapewa nafasi kama sisi wanadamu, ndio maana ninasema ni kwa neema ya Mungu ametupa nafasi.

    Kuishi bila kuwa mkamilifu ni hasara kubwa kuliko hasara zote ambazo mwanandamu anaweza kuzipata hapa duniani. Ndio maana Yesu alisema "... itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?" Marko 8:36.

    Ninakushauri tumia muda wako wote huku ukiwa unadumu katika ukamilifu.
    Jilinde na kuutunza ukamilifu wako katika Mungu. Kumbuka nafasi uliopewa ni moja tu ukiipoteza hakuna nyingine, kwa hiyo ni muhimu kuutumia muda vizuri ambao Mungu amekupa kuishi hapa duniani.

    Ndugu! usomaye maneno haya nakutakia baraka za Bwana ziwe pamoja nawe. Amen.
    KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU. Yakupasa kuwa makini sana usisahau kuishi maisha ya ukamilifu. Unaweza kusahau mambo mengine, lakini jambo hili la ukamilifu yakupasa kukumbuka wakati wote. Tafakari kila wakati je wewe ni mkamilifu. Ni muhimu kuishi a ukamilifu kwa sababu hujui saa wala wakati ambao utaondoka hapa duniani. Siku ile ya mwisho inakuja ghafla ambayo kanisa litanyakuliwa ni siku ambayo hakuna anayeijua. Waliotayari katika ukamilifu hao ndio watakaonyakuliwa. Wale ambao si wakamilifu wataachwa na kuhukumu na kutupwa katika ziwa la moto Kuliko utengwe na uso wa Mungu milele ni bora kuhakikisha kila wakati unaishi katika ukamilifu. Hakikisha wewe ni mkamilifu katika mambo yote ya Mungu na kwa wanadamu. Kwa sababu hiyo yakupasa kumpendeza Mungu na wanadamu, ndipo utakuwa umepata kibali mbele za Mungu. Hakikisha wewe ni mkamilifu wakati ukiwa umelala, unatembea, unakula, unapoongea na watu, unaposafiri, unapokuwa katika shughuli zako mbalimbali. Ndugu, tambua ya kwamba Mungu anakupenda amekupa nafasi moja tu. Hii ni nafasi ya pekee na kwa neema ya Mungu Baba yetu. Shetani na Malaika zake ambao walimwasi Mungu hawajapewa nafasi kama sisi wanadamu, ndio maana ninasema ni kwa neema ya Mungu ametupa nafasi. Kuishi bila kuwa mkamilifu ni hasara kubwa kuliko hasara zote ambazo mwanandamu anaweza kuzipata hapa duniani. Ndio maana Yesu alisema "... itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?" Marko 8:36. Ninakushauri tumia muda wako wote huku ukiwa unadumu katika ukamilifu. Jilinde na kuutunza ukamilifu wako katika Mungu. Kumbuka nafasi uliopewa ni moja tu ukiipoteza hakuna nyingine, kwa hiyo ni muhimu kuutumia muda vizuri ambao Mungu amekupa kuishi hapa duniani. Ndugu! usomaye maneno haya nakutakia baraka za Bwana ziwe pamoja nawe. Amen.
    Love
    1
    2 Kommentare 0 Geteilt 2KB Ansichten 0 Bewertungen
Gesponsert
[Repenting + Holiness = Entering Heaven / Kutubu + Utakatifu = Kuingia Mbinguni].