KWANINI MUNGU HUBARIKI MATAIFA YANAYOIBARIKI ISRAELI?

0
5K
Taifa la Israeli pamoja na mji wake mtakatifu wa Yerusalemu, kimsingi ndio unaoshika funguo za maisha ya baadaye na kuratibu kila hitimisho la kidunia kulingana na unabii katika Maandiko matakatifu. Patanisho la wanadamu na Mungu hata kuwaletea wanadamu neema ya kuwa na amani na Mungu lilifanyika Israeli. Kwa upande mwingine, ningeweza kusema kwamba; kutimilika kwa unabii wa maandiko matakatifu, kunahusianishwa moja kwa moja na taifa la Israeli.
 
Ni kwa sababu hiyo basi, chochote kinachotokea katika nchi ya Israeli kinaathiri kwa namna moja au nyingine kile Mungu anachokwenda kufanya kwa mataifa yote ya ulimwengu.
 
Kama kungekuwa na uwezekano wa kulitowesha taifa la Israeli pamoja na nchi yao, basi Biblia ingekuwa haina maana na wala utimilifu wa maandiko usingewezekana. Kumbuka kwamba, uwanja wa matukio yote ya nyakati za mwisho yaliyoandikwa kwenye Biblia ni Israeli. Mfano;
 
§ Vita vya Harmagedon vitapiganwa kwenye bonde la Megido lililoko Israeli UFUNUO 16:14-16, “Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote; kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu mwenyezi. Tazama naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake. Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni.” ZEKARIA 12:11 Biblia inasema” Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu kama maombolezo ya Hadadrimoni katika bonde la MEGIDO”
 
§ Bwana Yesu atakaporudi mara ya pili, ni lazima ashukie kwenye mlima wa Mizeituni nchini Israeli, ZEKARIA 14:4 Biblia inasema, “Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake upande wa mashariki na upande wa magharibi, litakuwapo huko bonde kubwa sana na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini na nusu yake utaondoka kwenda upande wa kusini”
 
§ Wakati wa utawala wa miaka 1000 wa Bwana wetu Yesu Kristo hapa duniani, maskani yake yatakuwa katika mji wa Yerusalemu ulioko Israeli (UFUNUO 20:7-10).
§ Mpinga Kristo na nabii wa uongo watakaojiinua katika kipindi cha dhiki kuu, ni lazima waukanyage mji mtakatifu wa Yerusalemu, UFUNUO 11:2, “Na behewa iliyo nje ya hekalu uiache nje wala usiipime, kwa maana Mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arobaini na miwili.”

Kwa hiyo, kwa kadri tunavyolielewa taifa hili la Mungu kwa mapana na marefu, na ndivyo uelewa wetu wa mambo ya sasa na yajayo unavyozidi kuwa mpana sana.
Tafuta
Vitengo
Soma Zaidi
SPIRITUAL EDUCATION
Why Do Bad Things Happen To Good People?
If God is completely in control, why do our lives sometimes not turn out as planned? If God is...
Kwa MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 02:22:09 0 5K
DEUTERONOMY
Verse by verse explanation of Deuteronomy 1
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 62 questions at the...
Kwa THE HOLY BIBLE 2022-01-24 19:17:34 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
HAKIKA ALIKUWA MWANA WA MUNGU
Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary...
Kwa GOSPEL PREACHER 2022-01-12 01:29:16 0 5K
1 SAMUEL
Verse by verse explanation of 1 Samuel 3
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 32 questions at the...
Kwa THE HOLY BIBLE 2022-01-26 03:20:00 0 5K
1 SAMUEL
Verse by verse explanation of 1 Samuel 1
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 44 questions at the...
Kwa THE HOLY BIBLE 2022-01-26 03:10:53 0 5K