UKRISTO NI NINI?

0
5K
Neno Ukristo ni tegemezi ya kutoka kwa Jina "KRISTO". Hivyobasi, Mkristo ni mfuasi wa Kristo. Ni kama unavyoweza sema Mtanzania anatoka Tanzania na/au neno Mtanzania ni tegemezi kutoka Tanzania au Utanzania litakoka kwenye muungano wa U na Tanzania.
 
Lengo la mkristo ni kutafuta ushirika wa karibu na Mungu Baba. Ushirika huo unawezeshwa na kazi aliyoifanya Yesu pamoja na huduma ndani ya maisha ya mkristo ya Roho Mtakatifu.

Mungu Mtakatifu hana ushirika na dhambi. Kati yake na mwanadamu kuna ufa mkubwa wa dhambi. Mwanadamu hujaribu kumfikia Mungu kwa nija nyingi: DINI, matendo mema, sala, n.k., lakini hizi zote hazitoshi. Mwanadamu bado ni mwenye dhambi.
 
MAANA YA UKRISTO:
Ukristo ni imani maalum kulinganisha na nyinginezo, Kwa sababu inasimamia zaidi ushirika na Mungu kuliko matendo ya kidini. Kinyume na kushikilia orodha ya masharti ya fanya haya na usifanye yale, Lengo la mkristo ni kutafuta ushirika wa karibu na Mungu Baba. Ushirika huo unawezeshwa na kazi aliyoifanya Yesu pamoja na huduma ndani ya maisha ya mkristo ya Roho Mtakatifu.
Wakristo huamini ya kuwa biblia ni Neno la Mungu na mafundisho yake ndiyo mamlaka ya mwisho (Timotheo wa pili 3:16, Petro wa pili 1: 20-21). Wakristo huamini juu ya Mungu mmoja akaaye katika utatu, Baba na Mwana (Yesu kristo), na Roho Mtakatifu.
Wakristo huamini ya kuwa biblia ni Neno la Mungu na mafundisho yake ndiyo mamlaka ya mwisho (Timotheo wa pili 3:16, Petro wa pili 1: 20-21). Wakristo huamini juu ya Mungu mmoja akaaye katika utatu, Baba na Mwana (Yesu kristo), na Roho Mtakatifu.
 
MAANA YA DINI:
Dini ni jaribio la mwanadamu kuwa na uhusiano na Mungu. Imani ya kikristo ni uhusiano na Mungu kwa sababu yale ametufanyia kupitia kwa kusulubiwa kwa Yesu Kristo.
WALE WOTE WENYE MASWALI KUHUSU UKRISTO. Tafadhali uliza hapa na utajibiwa kiurefu sana.
UKRISTO SIO DINI BALI NI IMANI MAALUM INAYO SIMAMIA ZAIDI NA KUSHIRIKIANA NA MUNGU KULIKO MATENDO YA KIDINI.
 
Kuna njia moja tu ya kushirikiana na Mungu .
YESU KRISTO NI NJIA YA PEKEE YA KUONDOA DHAMBI.
Alikufa kwa ajili yetu ili tujue upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yetu.
 
IMANI YA KWELI NI IPI?
Imani/Dini ya kweli sio ile ya kuangazia sheria bali ya kanuni. Imani ya kweli ni uhusiano na Mungu. Mambo mawili ambayo dini zote zashikilia ni kwamba mwanadamu kwa njia moja au nyingine ametengwa kutoka kwa Mungu na anahitaji kupatanishwa Naye. Dini za uongo zatafuta kuzuluhisha shida hii kwa kutunza sheria au kanuni. Imani ya kweli yazuluhisha tatizo kwa kutambua kwamba ni Mungu pekee anaweza kurekebisha utengano, na amekwisha fanya. Imani ya kweli yatambua yafuatayo:
• Wote tumetenda dhambi na kwa hivyo tumetenganishwa na Mungu (Warumi 3:23).
• Kama hautarekebishwa, adhabu ya haki ya dhambi ni mauti na utengano na Mungu wa milele baada ya kufa (Warumi 6:23).
• Mungu alikuja kwetu kupitia Kristo Yesu na akafa kwa ajili yetu, akachukua adhabu ambayo tulistahili, na akafufuka kutoka kwa wafu ili adhihirishe kuwa kifo chake kulikuwa dhabihu iliyotosha (Warumi 5:8; 1Wakorintho 15:3-4; 2Wakorintho 5:21)
• Kama tutampokea Yesu kama mwokozi wetu, kuamini kifo chake kama fidia kamili ya dhambi zetu, tumesamehewa, tumeokolewa, kombolewa, patanishwa na kufanywa wenye haki na Mungu (Yohana 3:16; Warumi 10:9-10; Waefeso 2:8-9).
 
MAANA YA UKRISTO KWA KIFUPI
Ukristo ni imani maalum kulinganisha na nyinginezo, Kwa sababu inasimamia zaidi ushirika na Mungu kuliko matendo ya kidini. Kinyume na kushikilia orodha ya masharti ya fanya haya na usifanye yale, Lengo la mkristo ni kutafuta ushirika wa karibu na Mungu Baba kupitia Mwana ambaye ni Yesu. Ushirika huo unawezeshwa na kazi aliyoifanya Yesu pamoja na huduma ndani ya maisha ya mkristo ya Roho Mtakatifu.
Wakristo huamini ya kuwa Biblia ni Neno la Mungu na mafundisho yake ndiyo mamlaka ya mwisho (Timotheo wa pili 3:16, Petro wa pili 1: 20-21). Wakristo huamini juu ya Mungu mmoja akaaye katika utatu, Baba na Mwana (Yesu kristo), na Roho Mtakatifu.

Kwa hivyo, huku dini nyingine zikitaka waumini wao watende mambo Fulani Fulani au wasitende mambo Fulani ukristo ni juu ya kuwa na ushirika na Mungu.

Hivyo Basi, Ukristo ni Ufuasi wa Kristo ambaye ni Mungu. Yesu Kristo ni Mungu.
Max Shimba Ministries
Tafuta
Vitengo
Soma Zaidi
SPIRITUAL EDUCATION
Spirit, Soul, and Body
The Christian doctrine of immortality cannot be understood apart from the right conception of...
Kwa MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 05:38:37 0 5K
JOB
Verse by verse explanation of Job 38
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 31 questions at the...
Kwa THE HOLY BIBLE 2022-04-03 04:20:58 0 5K
GENESIS
Verse by verse explanation of Genesis 3
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 57 questions at the...
Kwa THE HOLY BIBLE 2022-01-01 10:42:04 0 5K
2 CHRONICLES
Verse by verse explanation of 2 Chronicles 19
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 25 questions at the...
Kwa THE HOLY BIBLE 2022-04-02 01:41:14 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
FURAHA YA MUNGU KWA WATENDAKAZI
Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        ...
Kwa GOSPEL PREACHER 2022-01-12 01:28:01 0 5K