UTATA: NUHU WA QURAN NI TOFAUTI NA NUHU WA BIBLIA

0
5K
Ndugu Msomaji:
Siku zote Waislam huwa mnatutambia kuwa, Quran ni kitabu kilichoeleza kila kitu, ni kitabu ambacho kinajitosheleza, kitabu ambacho kimeshuka kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na kuikandia BIBLIA, kuwa haitokanani na Mungu, sasa nitatoa aya mbili kutoka Katika BIBLIA, na kisha aya 2 kutoka ndani ya Quran, kisha nitawauliza swali,
 
GHARIKA ILITOKEA LINI KUTOKANA NA BIBLIA:Mwanzo 7:6 Naye Nuhu alikuwa mtu wa miaka mia sita hapo hiyo gharika ya maji ilipokuwa juu ya nchi.
BIBLIA ambayo mnasema haitokani na Mungu, imesema kuwa, Nuhu, alikuwa ni mwenye Umri wa miaka mia sita (600) GHARIKA lilipotokea, pia ikaeleza miaka ya NUHU baada ya Gharika.
Mwanzo 9:28 Na Nuhu akaishi baada ya ile gharika miaka mia tatu na hamsini.
 
NUHU ALIKUFA NA MIAKA MINGAPI?29 Siku zote za Nuhu zilikuwa miaka mia kenda na hamsini, akafa.
Tunaambiwa na BIBLIA kuwa, Nuhu aliishi miaka mia tatu na hamsini (350) baada ya gharika ya maji, akafa akiwa na miaka mia tisa na hamsini (950) HIYO NDIYO MIAKA ya maisha yote ya NUHU hakuishi zaidi ya miaka hiyo, sasa twende Quran kisha niulize swali.
 
GHARIKA ILITOKEA LINI KUTOKANA NA QURAN?Quran 29 وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَى قَوْمِهِ فَلَبِثَ فِيهِمْ أَلْفَ سَنَةٍ إِلَّا خَمْسِينَ عَامًا فَأَخَذَهُمُ الطُّوفَانُ وَهُمْ ظَالِمُون
َ14. Na bila shaka tulimpeleka Nuhu kwa watu wake na akakaa nao miaka elfu kasoro miaka hamsini, basi mafuriko yakawaangamiza hali walikuwa madhalimu.

فَأَنجَيْنَاهُ وَأَصْحَابَ السَّفِينَةِ وَجَعَلْنَاهَا آيَةً لِّلْعَالَمِين
َ15. Na tukamuokoa yeye na watu wa (ndani ya ) safina, na tukaifanya (iwe mazingatio kwa walimwengu).
 
MADA KAMILI:BIBLIA imesema, Gharika limetokea Nuhu akiwa na miaka 600 Quran inasema, Gharika la Nuhu limetokea akiwa na miaka 950, sawa na miaka ya kufa kwa Nuhu, kwa mujibu wa BIBLIA, Biblia imesema, Nuhu akaishi miaka 350 baada ya Gharika, akafa na miaka 950 sawa na miaka ya gharika la Nuhu wa Ndani wa Quran.
 
MASWALI:-
1. Kwa kuwa ndani ya Quran, Nuhu alikuwa na miaka 950 Ndipo gharika likaja, na Biblia imesema ni miaka 600 gharika lilipokuja, na akafa akiwa na miaka 950 Sasa kwa mujibu wa Quran, Nuhu aliishi miaka mingapi kutoka katika Miaka hiyo 950 ya gharika?
2. au alikufa mwaka huo huo wa Gharika, akiwa na miaka hiyo 950 tuliyoambiwa alikuwa nayo wakati wa gharika ndani ya Quran?
 
NB. Majibu yatokane na Quran, tu kitabu ambacho mnatuambia ni cha Mungu, kama hakijitoshelezi, semeni, niwape ruhusa mtumie hata magazeti, na majarida.
 
Imeratibiwa na Abel Suleiman Shiliwa
Tafuta
Vitengo
Soma Zaidi
NDOA KIBIBLIA
NAJUTA KWA NINI NILIKUBALI KUOLEWA?
Baada ya mwaka mmoja wa ndoa, Merian asema anajuta kwa nini alikubali kuolewa. Merian na Joseph...
Kwa GOSPEL PREACHER 2021-11-23 07:11:44 0 5K
HOLY BIBLE
Is it okay to have sinners who are non-Christians as friends?
Yes, it's okay to have non-Christians as friends.  However, we don't want our friendships...
Kwa MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 05:39:19 0 5K
NEHEMIAH
Book of Nehemiah Explained
Book of Nehemiah “Title”: Nehemiah (“Yahweh has comforted”), is a...
Kwa THE HOLY BIBLE 2022-04-02 06:33:30 0 6K
Injili Ya Yesu Kristo
Chuma hunoa chuma!
Mithali 27:17 “Chuma hunoa chuma; Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake”  ...
Kwa GOSPEL PREACHER 2022-04-01 08:28:39 0 9K
MASWALI & MAJIBU
Je! Kiongozi Wa Dini Anao uwezo Wa Kusamehe Dhambi?
SWALI: Je! Ni sahihi kwenda kumfuata kiongozi wa dini kwa mfano Padre na kumpigia magoti...
Kwa GOSPEL PREACHER 2022-06-13 08:52:55 0 6K