MWANAUME UKIKOSA UNYENYEKEVU MKE ATAKUSHINDA

3
6K

Unyenyekevu ni tabia ya kujishusha na kuvaa kiatu cha aliye chini yako; unavua heshima na utukufu wako, kisha unavaa hali yake aliye chini yako. Kwa mume aliye chini yake ni mkewe.

Yesu kama kichwa cha kanisa ni mfano wetu sisi waume tulio vichwa vya wake zetu katika swala zima la unyenyekevu. Yeye alijishusha akavaa kiatu chetu, na kuanzia hapo ndipo anaanza kutuleta pale alipo anapopenda na anapotaka tuwe sisi Kama mwili wake yaani kanisa lake.(Waefeso 5:22, 23, 25 - 29)

Kujiposea kanisa ambalo ni mwili wake, Yesu alijinyenyekesha kiasi cha kuyasalimu maisha yake. Aliacha utukufu na heshima yake akawa mtumwa kwa ajili ya mwili wake ambalo ndilo kanisa lake.(Wafilipi 2:5 - 8)

Mume, ukitaka mke wako akunyenyekee, basi jinyenyekeze kwanza wewe. Unyenyekevu si udhaifu ni nguvu na ujasiri wa kukabiliana na changamoto kwa yule unayempenda, lakini ni njia ya kuuteka moyo wake ili kumtiisha chini ya mapenzi yako.

Unyenyekevu wako unamleta mkeo chini ya mamlaka yako. Kama unataka ajitiishe chini ya mamlaka yako, wewe acha ubwanyenye, jishushe mpaka pale alipo, vaa hali na hadhi yake, mchukue mikononi mwako, kisha anza kupanda naye juu.

Yesu alijishusha, akawa mnyenyekevu hata mauti ya msalaba. Kwa kuwa sisi tulikuwa wenye dhambi, Yeye alifanyika dhambi ili atutakase, na kwa kuwa tulikuwa chini ya kifungo cha mauti alikufa mauti yetu kisha tukafufuka pamoja naye, tukapaa pamoja naye juu, na tukaketishwa pamoja naye mbinguni.

Mwanaume, wewe kama umeoa, njia nzuri ya kumfanya mkeo awe vile wewe upendavyo inaanza kwa wewe kumkubali na kumpenda vile alivyo yeye ambavyo wewe hupendi. Na huo ni unyenyekevu. Huwezi kufanya hivyo mpaka umevaa kiatu chake.

Yesu hakuwapenda watakatifu, aliupenda ulimwengu uliokuwa wenye dhambi. Hakupenda dhambi zao, alizichukia. Alimpenda mtu lakini alichukia dhambi, lakini ili amfanye vile apendavyo ilimbidi awe dhambi ya yule mtu, ajishushe kutoka katika hali ya mwenye haki mpaka hali ya mwenye dhambi ambayo alikuwa nayo huyu mlimwengu. Akafanyika dhambi ili kwa njia ya mauti amkomboe na kumfanya vile apendavyo.

Hii ni kanuni ya unyenyekevu ili kumleta mwenzi wako pale ulipo ktk hali uliyonayo. Kama hayupo vile upendavyo, vaa kiatu chake, kisha mbebe na kumchukulia udhaifu wake kwa upole wote.

Kumbuka, unyenyekevu ni tunda la Roho Mtakatifu. Hivyo ni lazima uonyeshwe katika hali ya utakatifu.

Tafuta
Vitengo
Soma Zaidi
Injili Ya Yesu Kristo
Je! Mkristo anaweza pagagwa na Mapepo?
Bibilia kwa ukamilifu haitaji kama Mkristo anaweza shikwa na pepo. Ingagwa, kwa vile Mkristo...
Kwa MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 04:05:56 0 5K
HOLY BIBLE
THE HOLY BIBLE
Welcome to Proshabo Online Bible Study (POBS). This is the best platform for you to...
Kwa THE HOLY BIBLE 2022-01-01 08:57:05 0 7K
FORM 1
BASIC MATHEMATICS: FORM 1
List of all topics in Basic Mathematics for form 1 class: CLICK HERE TO VIEW. NUMBERS FRACTIONS...
Kwa PROSHABO ONLINE SCHOOLS 2021-10-09 12:44:29 0 5K
ESTHER
ESTA SURA YA 8, 9 & 10
Jina la YESU KRISTO BWANA wetu lisifiwe. Karibu kwenye mwendelezo wa kitabu cha Esta, leo...
Kwa GOSPEL PREACHER 2022-01-20 02:55:34 0 6K
OTHERS
Husband and wife
1 "Love your wife as Christ loved the Church." (Ephesians 5:25) Risk your life to help or save...
Kwa MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 10:54:43 0 5K