KWARESMA IPO KIBIBLIA

2
1K

KWARESMA IPO KIMAANDIKO?

 

 

 

Kwaresma ni nini?..Je! Kwaresma ipo katika Maandiko?..Na je ni lazima kufunga Kwaresma?, ni dhambi kuikatisha kwaresma? na je! ni dhambi kuishika kwaresma?

 

Neno Kwaresma limetokana na Neno la kilatini (Quadragesima) lenye maana “YA AROBAINI “… Kwahiyo siku ya 40 ndiyo inayoitwa Kwaresma..Kulingana na mapokeo ya, Madhehebu ya kikristo wanalitumia neno hilo kama kuwakilisha kipindi cha siku 40 cha mfungo kabla ya Pasaka.

 

Madhumini ya Mfungo huo ni kuwaandaa wakristo katika maombi, toba na kujinyenyekeza kwa ajili ya Pasaka ambayo itakuja baada ya siku hizo 40. Mfungo huo kulingana na mapokeo yao ni wa siku 40, lakini kiuhalisia ni zaidi ya siku 46..Kwasababu siku za jumapili huwa hazihesabiwi katika mfungo huo..Kwahiyo zinakuwepo jumapili 6 katika mfungo mzima..na kufanya Idadi ya siku za mfungo kuongezeka mpaka kufikia 46.

 

Mfungo huo pia unahusishwa na Bwana alivyofunga siku 40, akiwa jangwani, akijaribiwa na Ibilisi. Hivyo na wakristo wana jukumu la kufunga siku 40 kama Bwana alivyofunga.

 

JE KWARESMA IPO KIMAANDIKO?

 

Jibu ni La! Hapana sehemu yoyote katika maandiko kuna sharti la kuitimiza Kwaresma..Hayo ni mapokeo..Na mapokeo yapo yaliyo mazuri na yaliyo mabaya..Mazuri ni yale ambayo hayakinzani na Neno la Mungu na mabaya ni yale yanayokinzana na Neno la Mungu na kuwafanya watu wawe wa kidini zaidi, kuliko kuwa wa Kiroho.

 

JE NI DHAMBI KUISHIKA KWARESMA.

 

Katika Biblia ni wajibu wa kila Mkristo “kufunga na kusali”..Mambo hayo yanakwenda pamoja huwezi kusema unasali siku zote halafu hufungi hata mara moja, na pia huwezi kusema unafunga siku zote na husali hata siku moja. Kwahiyo Mfungo ni sharti kwa kila mwamini. Iwe ni mfungo wa wiki moja, wiki 2, siku 30, siku 40 au 50…Ni jambo la sharti. Na mfungo huo mtu auite kwa jina lolote iwe Kwaresma, jubilee, baragumu, au jina lolote lile ambalo mtu atapenda kuliita sio dhambi…

 

Kikubwa na cha msingi..Tendo lolote la kufunga halipaswi kuchukuliwa kidini..Kwamba mtu anafunga tu ili kutimiza sheria za dini yake, kama inavyofanyika leo. Haipaswi mtu kufunga halafu asiwe mwombaji…Wengi wanafunga lakini hata siku moja hawajawahi kutenga kusali hata lisaa limoja…huko ni kufunga kwa kidini ambako kuna matokeao madogo sana au kunaweza kusiwe na matokeo yoyote kabisa ikawa ni bure.

 

Hali kadhalika wakati wa Mfungo sio wakati wa kujichanganya na mambo ya kidunia, ni wakati wa kuwa katika utulivu wa roho na kujitesa nafsi, wakati wa kutubu kikweli kweli na wakati wa kuomba kwa bidii..Ni wakati wa kuongeza bidii sana katika mambo ya kiroho zaidi ya kimwili..Ndio maana unafunga kula..si wakati wa kuupendeza mwili ni wakati wa kuutiisha mwili.

 

Kwahiyo Mfungo huo unaoitwa Kwaresma kama hautafanyika kidini basi una matokeo makubwa sana kwa mhusika.

 

JE NI DHAMBI KUIKATISHA KWARESMA?

 

Mfungo mara nyingi ni kama Nadhiri, kabla ya kuanza kufunga mtu unaweka nadhiri kwamba unafunga siku 40, lakini ukisema unafunga halafu ndani ya mfungo huo unakuwa sio mwaminifu, utakuwa unajipotezea muda tu wewe mwenyewe..Kama umeamua kufunga sharti umalize siku zote na kama huwezi basi usifunge…Maana utakuwa hujafunga kwa Imani, na biblia imesema tendo lolote lisilotokana na Imani ni dhambi (Warumi 14:23)

 

JE NI LAZIMA KUFUNGA KWARESMA?

 

Jibu ni la!..sio lazima kufunga wakati huo unaoitwa Kwaresma…lakini ni wajibu wa kila Mkristo kufunga..Kama hutafunga msimu huo ambao ni rahisi kueleweka na watu wengi…basi hakikisha unatafuta kipindi kingine katikati ya mwaka ambacho utafunga. Na kama ni mkristo kikweli kweli na si wakidini, basi utafunga nawe siku hizo hizo 40 au zaidi. Kwasababu ukilijua lile neno linalosema..

 

Matendo 5:20 “Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni”

 

Kwasababu kama mtu unayemwita wewe wa kidini anakushinda idadi ya siku za kufunga…hapo ni nani wa kidini?…wewe au yeye?..Jibu ni wewe?..kwasababu huwezi kufanya hata anachokifanya yeye..na bado unamwita wa kidini. Sharti ufanye kama yeye tena vizuri zaidi umpite ili uwe na sababu ya kumrekebisha, lakini kama huwezi kumzidi, yeye ndio anayepaswa akurekebishe wewe. Kumbuka pia kwamba ili mfungo wako uwe na nguvu lazima uwe umejazwa Roho Mtakatifu ili akuwezeshe kufunga na kuutisha mwili pasipo Yesu Kristo na nguvu zake hatuwezi kufanya chochote hivyo huna budi kumpokea Yesu Kristo na kupokea kipawa cha Roho wake Mtakatifu hivyo kama hujampokea bado basi fungua moyo wako kwaajili yake naye ataingia na kufanya makao ndani yako 

 

Bwana akubariki

 

BY EV MARTIN LAIZER

Tafuta
Vitengo
Soma Zaidi
1 SAMUEL
Verse by verse explanation of 1 Samuel 27
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 23 questions at the...
Kwa THE HOLY BIBLE 2022-01-26 04:26:05 0 5K
2 SAMUEL
Verse by verse explanation of 2 Samuel 2
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 33 questions at the...
Kwa THE HOLY BIBLE 2022-02-05 09:09:43 0 4K
EXODUS
Verse by verse explanation of Exodus 12
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 136 questions at the...
Kwa THE HOLY BIBLE 2022-01-22 11:33:32 0 5K
EXODUS
Verse by verse explanation of Exodus 1
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 40 questions at the...
Kwa THE HOLY BIBLE 2022-01-21 12:33:38 0 5K
JOSHUA
Book of Joshua Explained
Title: This is the first of the 12 historical books, and it gained its name from the...
Kwa THE HOLY BIBLE 2022-01-25 07:10:22 0 6K