MKE WA KAINI KATOKEA WAPI?

0
5K

Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi;

Ukisoma kitabu cha Mwanzo sura 1-4,utaona Mungu akiwa na Adamu na Hawa kama watu wa kwanza kuumbwa na waliokuwepo. Lakini ukiendelea kusoma sura ya 4 baada ya Kaini alipomwua ndugu yake Habili ,utaona Kaini akifukuzwa naye akaenda kuishi kwenye nchi ya Nodi,huko akakutana na mwanamke kisha akamuoa (Mwanzo 4:16-18). Sasa swali linakuja hivi;Huyo mwanamke katokea wapi? Je kulikuwa na watu wengine kabla ya Adamu na Hawa? Umeelewa swali lakini?

Hili ni moja ya maswali yanayoulizwa sana,lakini ebu tujaribu kutafakari hili,na kujaribu kuweka majibu. Sasa,ikumbukwe ya kwamba Biblia tunayoitumia imetokana na taratibu/ustaharabu wa Kiyahudi ambao mwanamke hakuhesabika hasa kwenye jamii,ndio maana unaweza ukaliona hili kwa Dina mtoto wa Yakobo ambaye hatajwi kama kabila la Israeli,bali ndugu zake wale kumi na mbili ndio wanaotajwa (Mwanzo 35:22-26),Au unaweza kuona jambo hili pale Yesu alipowalisha watu elfu tano,wanawake wala watoto hawakuhesabiwa (Mathayo 14:20-21). Hivyo ilikuwa ni desturi ya kutokumwesabu mwanamke na watoto pia.

Kwa desturi hiyo hiyo,watoto wa Adamu wa kike hawakupewa nafasi ya kuhesabika kwa maana Adamu alikuwa na watoto wengine baada ya Kaini na Habili. Hivyo Kaini alimwoa dada yake,maana Adamu aliendelea kuwa na watoto wa kike na wakiume (Mwanzo 5:4). Biblia haikutupa kujua muda ambao Kaini aliishi katika nchi ya Nodi,tunachoelezwa ni kwamba Kaini akakaa katika nchi ya Nodi na akaoa huko. Hivyo inawezekana kuna muda fulani alioutumia Kaini kabla ya kuoa alipokuwa huko Nodi. Kaini alimwoa mmoja wa dada yake kama desturi ya zamani. Kwa maana hata Ibrahimu alimwoa Sara aliyekuwa ni dada yake wa mama mwingine ila baba yao alikuwa mmoja mzee Tera (Mwanzo 20:12)

Tafuta
Vitengo
Soma Zaidi
FORM 1
PHYSICS : FORM 1
List of all topics in Physics for the form 1 class: CLICK HERE TO DOWNLOAD. INTRODUCTION TO...
Kwa PROSHABO ONLINE SCHOOLS 2021-10-31 17:24:56 0 7K
SPIRITUAL EDUCATION
What does it mean that Jesus is the 'first-born' over Creation?
In a letter to the church at Colossae, the Apostle Paul gave an intriguing description of Jesus....
Kwa MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 02:23:01 0 5K
REVELATION
UFUNUO 8
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe.Karibu katika mwendelezo wa kitabu cha Ufunuo, leo kwa...
Kwa GOSPEL PREACHER 2021-10-30 10:32:32 0 6K
1 SAMUEL
Verse by verse explanation of 1 Samuel 14
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 62 questions at the...
Kwa THE HOLY BIBLE 2022-01-26 03:44:36 0 5K
MASTERS
MASTERS
List of all subjects for the students who are taking masters courses.
Kwa PROSHABO ONLINE SCHOOLS 2021-10-09 10:55:41 0 5K